Si kweli. Tunaona changamoto sana kwa hawa waliosoma Kayumba na kubahatika kufika level za kimataifa kwenye kazi za kimataifa.
-
Wengine walifanikiwa kufika level hizo kwa Connection tu. Kwa mfano nafanya kazi na Mtanzania mwenzangu kwenye International Organizational nchini Nambia, huyu Mdada amepata kazi kwenye hiyo Organization kwa sababu tu Ndugu yake ni Balozi wa Namibia.
-
Imemlazimu kufanya short course kuanzia Lugha mpaka Communications Skills na nyinginezo kwa sababu yeye mwenyewe anajionea aibu.
-
Hizo International school zinawajenga watoto vizuri sana hata kwa KUFIKIRI na kujiamini na mzazi ukiwa msimamizi mzuri wa mtoto wako atafika mbali sana na atakuwa very presentable kwa fadhila za International Schools.
-
It is very serious issue sisi tulio kwenye International Organization tunaona mengi na tunaona changamoto ya Mfumo wetu wa elimu na Africa kwa Ujumla.
-
Ukiona Kayumba yupo kwenye hizi Organization na anafanya vyema ujue huyo kaji mix sana na anapenda kujifunza vitu mbalimbali au ana exposure ya maisha.
-
Kwanza sisi wabongo hata kuongea hatujui, sijui kwa nini ! Sio English wala Kiswahili, hatujui kuongea na wala hatufikirii tunachongea.
-
Ukitaka kuona hilo angalia wasanii wetu wanavyojibu maswali, angalia wachezaji mpira wakihojiwa akiwemo Samatha, zero kabisa, njoo kwenye ngazi za viongozi, zero kabisa, sio Kiswahili wala English.
-
Msanii anaejua kuongea vyema Kiswahili na English ni Sepetu na Vanesi na Kiongozi ni Mkapa na January tu.
-
Shida ipo sana eneo hili na ndio maana once it comes about International Interviews , yaani WATZD huwa ni wa mwisho na hapo unakuta mtu ana vyeti vizuri na pass Marks zake.