Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mimi sizikubali sana hizo international school kwasababu mkifika Chuo kikuu,hakuna Significance difference ya wale waliosoma St.Kayumba na waliosoma International.
 
Kwanini uwaze kupunguza instead of training.., kama mwalimu ambae tayari anaujuzi ni rahisi kumtrain kuliko useme upunguze uajiri wapya,
... wachache sana ni trainable; most of them ni wa kuondoa kabisa kwenye mfumo kama lengo ni kufikia level za IST. Kumbuka mbwa nzee mbinu mpya hafundishiki.
 
Hao hao walimu unaowadharau na jizo grade zao ndio waliokufikisha hapo ulipo,
Na ndo maana hata thinking capacity yako ni finyu mno
... acha kujichanganya; "walimu hao hao na grade zao ndio walionifikisha hapa; na ndio maana thinking capacity yangu ni finyu mno"! Connect statement ya kwanza na conclusion halafu jitafakari thinking capacity yako ikoje! Sijui unakubali na unakataa nini!
 
Mimi sizikubali sana hizo international school kwasababu mkifika Chuo kikuu,hakuna Significance difference ya wale waliosoma St.Kayumba na waliosoma International.
... wazee wa takwimu! Hebu weka matokeo ya utafiti wako hapa tuyaone Chief.
 
Mtu ukiwa na hela ya kueleweka ama kama unataka kuwekeza kweli kwa watoto wako, wasomeshe international schools au shule zenye mitaala ya kimataifa.

Hizi shule zenye mitaala ya kimataifa zinawajenga watoto kwenye analytical skills, reasoning, logic, creativity, competence na mambo kama hayo.

Ukikutana na mtoto wa darasa la 6 wa hizi shule, reasoning yake ama analytical skills zake ni sawa na kijana wa form six wa necta schools.

Shule hizi hazilengi kuona mtoto anapata nini au maksi gani darasani bali kuibua talents nyingine alizonazo mtoto sio hizi za necta ambazo zimejikita kwenye ufaulu tu wa mwanafunzi.

Ukitaka kuwekeza kwenye elimu ya kweli kwa mwanao na kama uwezo upo peleka mwanao shule zenye mitaala ya kimataifa.
Tatizo la Elimu ya Tanzania ni Mitaala.
ni kweli kabisa kama unataka mtoto wako aelimike na awe na akili zinazotakiwa katika ulimwengu wa sasa inatakiwa asisome hii mitaala yetu,Mtoto anayesoma Shule ya awali yenye kutumia mtaala wa Montesory uwezi mlinganisha na mtoto anesoma vidudu shule za kawaida mitaani...alikadhalika Uwezi mlinganisha kijana anaesoma Seminary na kikilisto na hawa wengine ilo lipo wazi
 
Wazazi tusake hela jamani watoto wetu wakasome kwenye shule bora, mwezi wa 7 nilikutana na binti mmoja hapa Johannesburg akiwa anajiandaa kurudi Tanzania kwa sababu ya restrictions za covid-19. Huyu bunti amesoma primary na secondary Aga Khan international school ambapo wanatumia mtaala wa Cambridge. Baada ya hapo akaja kujiunga Stellenbosch University iko cape town (1 ya top 3 universities hapa SA).

Anakotoka hela ipo sio kidogo na hapo chuo ada kwa mwaka ni around 20m za kitanzania plus accommodation na extras nyingine. Binti anajiamini huku akijua anachokifanya,anachukua degree ya Mambo kilimo na economics na akimaliza mwakani ana job offer Canada.

Naendelea kuzisaka hela mwanangu at least apite njia kama ile, makapuku tunanyongwa kielimu ndiyo maana wanasiasa hawapeleki watoto zao shule za kawaida za serikali. Pesa tu ya kugharamia elimu bora ndiyo ticket ya kumfanya mwanao aje akae kwenye high table ya maisha.
Primary na secondary Aga Khan Tanzania?
 
Primary na secondary Aga Khan Tanzania?
"Primary Tanzania Ila secondary nadhani iko Kenya."View attachment 1603656
Screenshot_20201018_063620_com.android.chrome.jpg
 
Usinikumbushe mapito niliyo pitia.
Ile naanza na form five tu mwalimu wa kemia mzungu,mmarekani na Mjapani,hesabu ni mchina wa kimarekani na Mhindi,nageukia Fizikia nakutana na mzee Ngui sijui kabila gani masikini muda wote ni kufoka tu. Halelujaaa DS hii hapa na mzee Mwangoka anafundisha kwa kinyakyusa na stori zake za Tukuyu na kufukuzwa chuo kikuu kwa migomo...
Ikawa mwanzo mwisho ni kumeza tu....
Umesoma tukuyu day?

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
😂😂😂😂😂😂😂
cariha aaa
.... whaaaaat! cariha you are not serious! Yaani mwalimu wa shule ya msingi Kimanzichana FIV (F-F-D-D-D-F-F) plus Teacher's Certificate Grade IIIA apewe mafunzo ya kuwa level ya mwalimu wa IST? Na hayo mafunzo atapatiwa na college zipi? Hizi hizi tunazozijua?
 
Naunga mkono hoja.
Kulipa ada ya milioni 40 kwa mwaka sio kazi ndogo,halafu badae akimaliza chuo aje kuhangaika kupata kazi ya mshahara wa laki 4 inakuwa hasara.
ukihesabu hiyo milioni 40 mara miaka 6 unajenga nyumba ngapi?
Unaona asset ni nyumba tu?

Mtoto anayesomeshwa IST haji kufanya kazi na wewe.

Wengi wanafungua kampuni zao au wapo kwenye international organizations.
 
sasa kwani waliosoma shule za kawaida wanashindwa au wanazuiliwa kufungua kampuni zao?assets ziko za aina nyingi hiyo nyumba nimetolea mfano tu
Unaona asset ni nyumba tu?

Mtoto anayesomeshwa IST haji kufanya kazi na wewe.

Wengi wanafungua kampuni zao au wapo kwenye international organizations.
 
Kuwa mjumbe wa Bodi wa Shule kumenisaidia kufahamu mengi juu ya hizi shule za serikali.Hizi shule za serikali siku hizi zimejaa siasa na mihemuko. Syllabus haifuatwi,kuna wataalamu wa elimu wanaojiita wakuu wa shule na maafsa elimu wa halmashauri kutwa kubuni vitu vya ajabu ajabu mara;

Wanafunzi wanakatazwa kusoma masomo mengine wasome Civics na Kiswahili eti wapate 'D' mbili za cheti.

Kuna baadhi wanaambiwa waache kabisa kusoma somo la hisabati. Wengine wanakatazwa walimu wasifundishe badala yake wawape wanafunzi mitihani na wasolve! Jumlisha mitihani ya inter- school, pre - mock,Mock,pre NECTA ,Terminal,Mid-term nk. Kunawafanya walimu wasifundishe kabisaa.

Maagizo ya mara kwa mara toka kwa wabunifu wa wilayani na ubunifu wa mkuu wa Shule yasiyofuata na kuzingatia syllabus sio tu yanapunguza maana ya mtaala pia malengo yaliyokusudiwa.
sawa
 
Mtaala kuubadilisha inawezekana ila changamoto ni:
1.Wanaopaswa kuubadilisha wanajua wabadilishe nini? Wako na hiyo elimu?
2. Gharama za kuuendesha huo mtaala kama: vifaa vya kufundishia, ziara za ndani na nje ya nchi za kimasomo wazazi watazimudu?
3. Serikali inaouwezo wa kuweka miundo mbinu n.k?
4. Wazazi wana uwezo wa kugharamia ada na michango mingine? Iwapo sasa hakuna ada ila uniforms zinawashinda wazazi mfano viatu n.k?
Ongezea na kingine kuwalipa walimu wa kimataifa kutoka ulaya wataweza?
 
Mkuu hapa nikusahihishe kidogo.
Ulichokiona wewe hapa ni kusifia tu hizo shule na huyo mwanafunzi lakini umesahau kuwasifia wazazi wake kuwa wana pesa.
Kwa mfano chukulia mtu aliyesoma hizi saint kayumba hadi form 6 halafu ukampeleka kusoma university huko Cape town unafikiri atashindwa kutoboa au kupata kazi huko canada?
Kitu ulichoshindwa kujua hapo ni kwamba kilichomfanya hapo apate kazi canada sio kwa vile ameelewa sana elimu ila ni connection tu iliyosababishwa na kujuana na watu wa aina mbalimbali.
Wazazi tusake hela jamani watoto wetu wakasome kwenye shule bora, mwezi wa 7 nilikutana na binti mmoja hapa Johannesburg akiwa anajiandaa kurudi Tanzania kwa sababu ya restrictions za covid-19. Huyu bunti amesoma primary na secondary Aga Khan international school ambapo wanatumia mtaala wa Cambridge. Baada ya hapo akaja kujiunga Stellenbosch University iko cape town (1 ya top 3 universities hapa SA).

Anakotoka hela ipo sio kidogo na hapo chuo ada kwa mwaka ni around 20m za kitanzania plus accommodation na extras nyingine. Binti anajiamini huku akijua anachokifanya,anachukua degree ya Mambo kilimo na economics na akimaliza mwakani ana job offer Canada.

Naendelea kuzisaka hela mwanangu at least apite njia kama ile, makapuku tunanyongwa kielimu ndiyo maana wanasiasa hawapeleki watoto zao shule za kawaida za serikali. Pesa tu ya kugharamia elimu bora ndiyo ticket ya kumfanya mwanao aje akae kwenye high table ya maisha.
 
Ukitaka kuanza safari, agana na nyonga.. Mtoto ili atoke nursery mpaka amalize chuo kikuu, ana miaka kama 20 ya kusoma.
Je wewe mzazi una uhakika kipato chako kitakuwa mwake kwa miaka hii 20? Kama huna uhakika, mpeleke shule za umma.. Come rain, come sun, mtoto anakuwa na uhakika wa masomo.
 
Back
Top Bottom