Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

huo uwezo wataupimaje na kukuamini wakupe hiyo kazi?kama hizi shule za english medium tu wanaaminika walimu wa kutoka kenya na uganda
Utaifa wa mwalimu si kigezo bali uwezo wake. Kumbuka gharama kubwa za ada ndizo hipelekea mishahara minono.
 
Kama Trump mwenyewe hawezi kujieleza lakini ndo Rais wa taifa kubwa duniani,tafuta pesa mzee mengine yote yatakuja yenyewe..ushawahi kumsikia mzee Bakhresa akiongea? au marehemu Mengi? hawawezi kuongea sentensi tatu ukazielewa direct bila ya kudhania walichomaanisha.
 
Mkuu umewaza kwa mapana sana ni kitu ambacho hata mimi nimekifikiria.
 
Sylabus enyewe majanga. Hata wangefuata hiyo sylabus nukta kwa nukta bado haiondoi kukaririshwa! Hao maafisa elimu na waalimu ni product ya sylabus ya kukaririsha unategemea nini? Hadi Universities Hali ni hiyo hiyo.
 
If it's true then that was a fools errand.
 
Acha uoga.

Kati ya watoto 100 wanaosoma huko uma ni 10 tu wanaotoka na elimu stahiki..na hao ni akili zao binafsi, 90 huudhuria tu kuitika jina na kuhesabu namba.
 
Unajifariji tu. Scholarship unapata lakini haina maana kuwa ubora wako uko kama wa graduate wa IST. Walimu wanafundisha hapo chuo kikuu lakini hawezi kujieleza kwa Kiingereza.
Kuna mkuu mmoja alikuwa anatoa maagizo kwa wachina, Aisee kile kiingereza chake anatakiwa aoongee mtoto wa la nne B.
 
Unazungumziaje shule za seminary ambazo wanatumia necta? Kama lengo ni kuwa international mkataa kwao ni mtumwa. Upo wapi uzalendo?

Hata niwe bilionea mwanangu atasoma seminary - uru seminary, st James, maua seminary these are the best seminary schools in Tanzania.
Mbali na passmark kupata selection tu ni ishu.
 
Mfumo mzima wa elimu nchini ni wa ajabu.
Haufai kufuatwa
 
Mkuu kuna world scholars kibao ambao hawajakanyaga hizo international schools na wanaheshimika kwenye field zao. Nafikiri hizo shule zimeanzishwa purposely kwa ajili ya watoto wa mabalozi kwenye nchi husika, hakuna jipya...
Unadhani.....
 
Nina mashaka kama umesoma. Ungekuwa umesoma na kuelimika ungegundua mwanzisha mada hakusema kuwa wote wanaosoma huko kajamba nani wanaishia pabaya ila ameongelea zaidi wenye chance kubwa.
 
Mkuu umewaza kwa mapana sana ni kitu ambacho hata mimi nimekifikiria.
Nnachoamini hapo kama wewe ni masikini na ukapata pesa nyingi msomeshe mwanao international school kwa sababu mwanao atakuwa mtu mwenye connection kwa sababu marafiki zake wengi ni kutoka familia zenye pesa kwahiyo suala la ajira litakuwa ni uhakika
 
Hapa nimehakikisha kabisa wewe ni wale waliosoma shule za kukariri. Focus yako iko kwenye kupass mitihani wakati mwenzako anaongelea kitu kingine kabisa. Shule nyingi za Bongo zimejikita kwenye kukaririsha wanafunzi ili wa pass mtihani kwa gharama yoyote lakini unakuta hawana upeo wa kuchambua mambo.... kama wewe!
 
Kichwa kwenye kumeza au? Kichwa gani kwa maana huyo kichwa atatoka na one kali halafu atakutana chuo kimoja na yule aliyepata division three na wote watapata mkopo na wote watasoma chuo kwenye carriers zao na wote watamaliza na kupata cheti.
Sasa hapa najiuliza faida ya kuwa kichwa ni nini hasa na je? Kuna faida ganinya kuwa na special schools?
 
Nnachoamini hapo kama wewe ni masikini na ukapata pesa nyingi msomeshe mwanao international school kwa sababu mwanao atakuwa mtu mwenye connection kwa sababu marafiki zake wengi ni kutoka familia zenye pesa kwahiyo suala la ajira litakuwa ni uhakika
Sasa kinachosahaulika hapo pesa zangu ndio zitakuwa zimemsaidia sio hizo shule.
Kwani kuna wale watoto wa kiarabu wanaomiliki biashara ya mabus na magorofa pale kariakoo pia walisoma kwenye shule hizo?
 
Hatujui kuongea wala kuandika Kiswahili na kiingereza kwa ufasaha. Huu nao ni ukweli usiopingika. Au wazee wetu hawakuwekeza katika lishe bora, hence vizazi vyetu vimekuwa below average.

Je, hao waliosoma International schools wamelisaidia vipi taifa? Wametoa mchango gani tofauti na hawa kina sisi St. Kayumba? Maana tusiangalie elimu ya darasani wakati taifa bado lipo nyuma sana na tuna mchanganyiko wa wasomi wa shule mbovu na za kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…