MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

Hizi taaratibu zikianza katikati huko zinapotea.

Unakumbuka ya Lucky Vicent?
Ndio nakumbuka Dear, ile ajari ndio ilisababisha serikali itowe Amri gari ziende garage Kila mwezi na zilipelekwa kweri, naona yule Waziri alipoondoka na utaratibu ukafa
 
Ndio nakumbuka Dear, ile ajari ndio ilisababisha serikali itowe Amri gari ziende garage Kila mwezi na zilipelekwa kweri, naona yule Waziri alipoondoka na utaratibu ukafa
Ndiyo kama hivyo...
Imetokea hii Wataanza tena..baadaye Hauoni wakiendelea...
 
R.I.P Moyo unauma Maskini pole kwa wazazi maumivu yake makali mno. Majeruhi nawaombea uponaji mwema.

Magari mengi ya shule mabovu mno.
 
Njia inaelekea ni ya maporomoko kuinama,

Poleni

Ova
 
Uzembe Uzembe Uzembe Uzembe Uzembe.
Utasikia tunaanza kuisingizia bahati mbaya.
Utasikia kesho jeshi la polisi linaanza operation maalum dhidi ya haya magari.

Watoto wamekufa bila hatia bali uzembe wa mababa zao, mama zao na kaka zao.
 
Gari nyingi sana za shule ni mbovu. Na mamlaka zimekaa kimya. Naona maafa yanaweza kuongezeka. Tujiulize gari y shule inayozunguka hpo mjini inapata ajari kirahis namna hiyo.
Gari nyingi watoto wanabebana licha ya waz kulipia usafiri yaani ni Kazi kwelikweli.
 
Seat belt kwa dereva au abiria wa nyuma,
Maana kwa kawaida nchi yetu seat belt ni kwa dereva na mtu mbele


#Pole kwa wafiwa
Seat belt itoke wapi magari haya asilimia kubwa ni mabovu. Mamlaka zimafanya kaz kwa matukio.
 
Reactions: Lax
RPC na RTO wa huo mkoa muda huu hawapaswi kuwapo kazini.
Traffic polisi waliokuwa barabarani route zote basi lilimopita muda huu hawapaswi kuwepo shuleni.

Mmiliki wa shule anapaswa kuwa jela na shule kufungiwa kabisa maisha.

Adhabu hizi ndio zitafanya watu wazidishe umakini kwenye kazi zao.
 
Duh! taarifa mbaya sana hii...

Lakini hadi sasa najiuliza hiyo ajali imekuaje imeua watu wengi hivyo, ukitazama picha ni kama impact sio kubwa na gari imeingia kidogo tu katika korongo...
 
Duh! taarifa mbaya sana hii...

Lakini hadi sasa najiuliza hiyo ajali imekuaje imeua watu wengi hivyo, ukitazama picha ni kama impact sio kubwa na gari imeingia kidogo tu katika korongo...
Inaonekana kule upande ilipoangukia imejibamiza kwa nguvu na body likarudi huku upande wa dereva na kuwabana ukiangalia kwa makini.

Wapunzike kwa amani Marehemu wote waliotangulia kwenye ajali hiyo na maheruhi Mungu awasimamie wapate kupona haraka. [emoji17]
 
Seatbelts zinaweza kusaidia sana. Lakini ukiangalia school buses za wenzetu huwa hazina seatbelts. Watoto wengine wadogo sana. Lakini barabarani wana sheria ambazo zinayapa magari ya wanafunzi. Mfano gari ya wanafunzi ikisimama kupakia wanafunzi, gari zingine zote zinasimama.
 
Ni uchungu kwa kweli asubuhi unamwandaa mtoto aende shule ghafla unaenda kumwangalia mochwari. Mungu awape uvumilivu wazazi wa hawa watoto jmn. Roho zao zipumzike mahali pema.
 
...Mabasi ya hizi shule kubwakubwa kila mwaka wanapoteza wanafunzi. Iko shida pahala; vyombo vya dola vifanye uchunguzi wa kina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…