Tetesi: Muda wowote kuanzia sasa Samia ataachana na DP World!

Achague mawili kuufuta au marekebisho kupitia wananchi na Sio wabunge.
Waislamu someni mkataba muuelewe acheni porojo za kuegemea dini.
Kama ni dini mbona waislamu ndio wanajenga reli na ndio wanaojenga bwawa la umeme.
Udini upo wapi.
Kinaangaliwa kesho yetu na usalama nchi na raslimali zetu.
 
Wanaomdanganya wanamshauri aendelee nao.
 
Ahsante kwa kuwakumbusha ila hapa tatizo sio waislam bali ni watu wachache waliongwa tende na harua ndio wanataka kuvuruga nchi kwa kisingizio cha dini kama ni dpw ndiye amepenyeza hiyo kitu basi amebugi.
 
Na uvccm na cccm itatoka barabarni kumpongeza rais kwa ujasiri huo wa kufuta mkataba huo na azimio litafanywa bungeni kumpongeza kwa hatua hyo

Kama itatokea Hilo Basi ndo hvyo
Wajinga kweli jamaa, hahaha
 
Tulishajua nia yako nini, ongelea mkataba mambo ya chadema wasukuma tupa kule.
 
Kwnn wasiwekeze Mombasa Kisha Dar wakabiziwe TEC ili tuone ufanisi bad miaka kadhaa?
 
Uongo mtupu, hakuna kurahisisha wala nini bali ni watu wanatafuta uraji.
 
Rais wetu akiachana mkataba bandari huo 2025 binafsi mimi sihitaji mgombea urais Dr.Samia nimevutiwa sanq utawala wake wa haki hasa maridhiano. Aachee tu na mkataba mimi nataka apate kura zaidi 90%
 
Ametangaza Kuachana na DP WORLD kama ulivyoandika???
 
Ahsante kwa kuwakumbusha ila hapa tatizo sio waislam bali ni watu wachache waliongwa tende na harua ndio wanataka kuvuruga nchi kwa kisingizio cha dini kama ni dpw ndiye amepenyeza hiyo kitu basi amebugi.
Kuna magati sita ya TPA yanahitaji uwekezaji pia kuna bandari nzima ya Bagamoyo inakuja mwaka huu, hivyo kama DPW mmoja anawekewa mizengwe namna hii vipi kuhusu wawekezaji wa magati namba tisa mpaka kumi na mbili wa pale bandarini. Vipi kuhusu uwekezaji mzima wa Bagamoyo utakuwa vipi?.

Siasa zetu za kambale kila mmoja majini ana ndevu zinatujaza ujinga mwingi tu bila ya kutusaidia kwa namna yoyote ile. Haya ya bandari ni maswala ya kitaalam sana lakini kwa sababu watanzania siku zote hatuheshimu utaalam kwa sababu ya elimu zetu za kuungaunga hatuwezi kuona namna tunavyopoteza muda kwenye mijadala yetu isiyo na tija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…