Tetesi: Muda wowote kuanzia sasa Samia ataachana na DP World!

Tetesi: Muda wowote kuanzia sasa Samia ataachana na DP World!

Ni ngumu kutokea..., haya maziwa yameshamwagika wapo radhi hata kuwauwa ngombe wote ili kuficha kilichotokea....

Hawa sio watu wa kurudi nyuma na kukubali walikosea
Nashawishika mno, kukubaliana nawe kwenye dhana hii.

Kinachoweza kufanyika ni kujaribu kutafuta njia za kupoza tu, kama vile kufanyiwa marekebisho baadhi ya vifungu tata.

Kuachana moja kwa moja na hujuma hii ya DP World kwa sasa haiwezekani. Wamekwishatufikisha mbali sana.

Au pengine ili nieleweke vizuri: Njia pekee iliyopo sasa ya kuachana moja kwa moja na DP World, ni kuondoa hizi takataka zote zilizohusika katika hujuma hiyo, ikiwa ni pamoja na mwasisi mkuu wa hujuma hiyo.
Huo utakuwa ni mshindo mkubwa sana tunaoweza kuutegemea utokee ghafla, siyo hivi kwa kusemezana vimaneno maneno hapa na pale.
 

-Tanzania unlawfully expropriated Ntaka Hill nickel project, tribunal finds, awards miner $109m​

-Indiana Resources (ASX:IDA) wins $160M from Tanzania in World Bank dispute​

-The Hong Kong arm of Standard Chartered Bank has won a US$185 million ICSID award against Tanzania in a dispute over rights under a power purchase agreement which has already spawned three other arbitrations at the centre
-Symbion

Tanzania inapoteza pesa nyingi sana kutokana na hii mikataba, hiyo ni mifano tuu, kuna kesi nyingi sana tumepoteza na sasa tunalipa, rushwa na incompetency ya serikali ni kubwa sana, bandari itakuwa balaa tupu itakuwa ni sawa na alichofanya Mangungo kwa watu wake, ujinga unatumaliza
US Dollar 109,000,000= Tanzanian Shilling 273,211,031,710
Bado walioenda kwenye kesi ...per diem, nauli, matayarisho na mwiho upigaji lazima uwepo...kuinflate vitu; na gharama za kesi yenyewe kwa mahakama..........350,000,000,000 appro
 
Mimi binafsi sipendi upuuzi wa pale Bandarini na natamani ibinafsishwe .

Kuliko kuachana na DP World Bora vifungu vinavyozozaniwa virekeboshwe...
Ni kwasababu Tanzania hatuna utaratibu wa kuhifadhi "classified Documents" na baadae kuzifanya kuwa Open kwa public.

Tungeweza kufahamu khasa hayati JPM alikuwa na msimamo upi kuhusu bandari ya DSM na uendeshaji wake.

Na kama kulikuwa na maamuzi fulani ni kwa vipi maamuzi hayo yamegeuzwa likiwemo suala la sheria za rasilimali za taifa.

The damage is too big to repair.
 
Yani asiachane na DP w pekee mikataba yote ya ki mwijaku na ya baba levo hatuitaki SISI kama walipa kosi
 
Kwenye hii issue ya Bandari, tatizo ni Warabu. Kama uwekezaji huu ungeingiwa na nchi nyingine yeyote mfano uingereza, Marekani au hata China isingekuwa hali kama ilivyo sasa. Ndio maana hata maelezo ya watu muda wote wanasema kumpa Bandari Mwarabu lakini mikataba kibao mingine tuliyoingia huko nyuma hatujawahi kusema kumkabidhi Mmarekani 123.. Au kumpa Mchina 123 ..ila Mwarabu anatajwa kwa race yake.
 
Be the first to know... muda wowote kuanzia sasa Rais Samia atauzima rasmi mjadala unaochukua sura mpya kila siku nao si mwingine bali ni DP World!

Vyanzo vyangu toka ndani ya Chama na Serikali vinabainisha joto la mjadala linaelekea pabaya hivyo busara imetumika kufunika kombe mwanaharamu apite!

Hongera samia kwa usikivu kumbe zile R nne zinatoka moyoni!
Usikivu gani wakati bado ni story tu za vijiwe vya kahawa? Lakini hata akiachana nao atakuwa ametuthibitishia kwamba ni kiongozi asiyejua anafanya nini yaani unasaini utapeli kama huu bila kuelewa contents zake! Je kama sio utapeli huo kuvujishwa si tungeuzwa? Je hatosaini utapeli mwingine wa kutuuza na tukauzwa bila kufahamu kama hatatokea mzalendo wa kutung'ata sikio?

Hata akiuacha bado atakuwa hajafanya la maana bali atakuwa ameogopa nguvu ya umma wa watanganyika. Lakini pia tujiulize hata akiachana nao kaumiza watu wangapi kulinda utapeli huo? Pesa ngapi imetumika kutetea utapeli huo? Ni kwa kiasi gani mihimili yetu muhimu ya dola hasa mahakama na bunge imedhalilishwa ili kutetea utapeli huo? Kiujumla hatakiwi kupongezwa kwa usikivu anatakiwa kushitakiwa kwa jaribio la kuigawa Tanganyika kwa waarabu.
 
Tatizo halipo kwa mama bali ni kikundi cha sukuma gang kina muingiza kwenye matatizo makusudi ili mwaka 2025 akataliwe
Kati ya mama Abdul na Mbarawa sukuma gang ni yupi? Maana wao ndo walisaini utapeli huo mam yenu nchi imemshinda aacha kutafuta visingizio vya kusingizia wasio husika
 
Be the first to know... muda wowote kuanzia sasa Rais Samia atauzima rasmi mjadala unaochukua sura mpya kila siku nao si mwingine bali ni DP World!

Vyanzo vyangu toka ndani ya Chama na Serikali vinabainisha joto la mjadala linaelekea pabaya hivyo busara imetumika kufunika kombe mwanaharamu apite!

Hongera samia kwa usikivu kumbe zile R nne zinatoka moyoni!
Wameweza kurudisha kile kianzio? Au wamesamehewa? Vipi zile MOU nyingine 31? This Might be too good to be true!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Be the first to know... muda wowote kuanzia sasa Rais Samia atauzima rasmi mjadala unaochukua sura mpya kila siku nao si mwingine bali ni DP World!

Vyanzo vyangu toka ndani ya Chama na Serikali vinabainisha joto la mjadala linaelekea pabaya hivyo busara imetumika kufunika kombe mwanaharamu apite!

Hongera samia kwa usikivu kumbe zile R nne zinatoka moyoni!
Samahani,hizoR nne ndo zipi!?
 
Mama Samia piga U turn uachane na huu ujinga ufute na mikesi hii ya kihuni tukuunge mkono. Still you can be one of the best president ever in Tanzania! Go mama!
Duh!

Kweli JF haiwezi kuishiwa vituko!
Unakutana na vituko hata uskotegemea kuvikuta.
 
Kwa kifupi alichopost huyo mtu ni kichekesho/ utani sio uhalisia.

Hakuna mkataba au uwekezaji unaovunjwa
Mimi nimecheka tu, mkuu 'Lord', sikutaka kuanzisha mjadala hata kidogo wakati huu.

Mwandame huyo huyo aliyesababisha uliyo andika wewe, na kunifanya mimi niangue kicheko (cha kejeli).
 
Back
Top Bottom