MUFTI umeongea sana kuhusu Amani nchini lakini Bila kuzungumzia Haki usia wako unapwelea

MUFTI umeongea sana kuhusu Amani nchini lakini Bila kuzungumzia Haki usia wako unapwelea

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Ndugu Mufti Zubeir
Kwa muda mrefu umezungumzia sana suala la amani nchini lakini huwa huzungumzii Haki, Pamoja na ujumbe wako wa amani hata hivyo kutokuzungumzia haki kunaufanya ujumbe wako upwelee.

Dini ya Kiislamu inataka amani lakini inakataza dhulma. Mafundisho ya kiislamu yanasema kuwa "Usidhulumu na wa wala usidhulumiwe". Sasa ndugu Mufti haya mafunzo wewe huwa huyafundishi, wewe umekalia amani, amani, amani. Sote tunataka amani lakini mbona wewe mwenzetu Haki huipi uzito?.

Wewe unafahamu amani na haki ni kama pande mbili za sarafu moja, lakini wewe umeshikilia upande mmoja tu wa amani, lakini suala la haki umelipa kisogo.

Rai yangu ni kwamba, kama unataka ujumbe wako usikilizwe na awananchi na wauzingatie, basi tetea haki hapo utakuwa na moral authority ya kuzungumzia amani. La sivyo ndugu Sheikh Mkuu nasikitika kwamba ujumbe wako wa amani yake wananachi tunayona kama ujumbe wa kisiasa zaidi kwa maslahi ya CCM.
 
Kuzungumzia amani bila kutanguliza kuwepo kwa haki ni sawa na kuweka mkokoteni mbele ya punda ukitegemea mkokoteni ndiyo uvute punda. Mufti hakuutendea haki Uislamu na Waislamu kwani amebariki dhuluma na uonevu unaofanywa na CCM na Serikali yake kwa wapinzani hasa kwenye chaguzi zote.
 
Mufti ni msaka fursa wala hana lolote, huwezi kuona Rais ameenda kwenye kongamano ambao Shelkh Ponda sababu ataenda kuambiwa ukweli
 
Analinda maslahi yake binafsi kwanza kuliko ya mamilioni ya Watanzania. Ni hulka ya binadamu wengi wasio na imani thabiti wa dini zote na wasio na dini. Vigumu kuwapata watu kama Traore.
Hapo atakuwa kaachiwa kama 50M za Iddi apigie dembe CCM
 
Hakuna waislam hapo zaidi ya Shelkh Ponda hawa ni wasaka fursa tupu
Chadema mna mashehe na maaskofu wa ajabu ajabu
Mfano Askofu Mwamakula hana kanisa kabisa ulizia yeyote jengo la kanisa anakosali liko wapi? Hana ni kuzurura tu na Chadema kuponea posho za tonetone hana waumini ambao labda mngetarajia wawe wapiga kura wenu

Shehe ponda hana hata jengo la msikiti anakosalisha hana waumini kuwa atawasaidia kuwapa wapiga kura
 
Shehe ponda hana hata jengo la msikiti anakosalisha hana waumini kuwa atawSaidia kuwapa wapiga kura
UWT mnajifariji sn
 
Chadema mna mashehe na maaskofu wa ajabu ajabu
Mfano Askofu Mwamakula hana kanisa kabisa ulizia yeyote jengo la kanisa anakosali liko wapi? Hana ni kuzurura tu na Chadema kuponea posho za tonetone hana waumini ambao labda mngetarajia wawe wapiga kura wenu

Shehe ponda hana hata jengo la msikiti anakosalisha hana waumini kuwa atawasaidia kuwapa wapiga kura
Siku zenu za kuiba rasilimali za umma ziko mwisho(kama bado hujakusanya pesa za kutosha fanya haraka kukusanya zaidi),huwezi kutaka amani huku unadhuluma haki za wananchi.Kweli shoka lipo shinani.
 
Ameshaonja utamu wa hela za loyo tua huyu,halafu hawa jamaa kiongozi hata akiwa mbovu kiasi gani,as longer as anatokea dini yao wao humuunga mkono tu.
 
Mufti ajibu maswali ya Babu Wassira kuna HAKI hapo?

Bila HAKI hakuna AMANI.
 
Azungumzie haki apokonywe posho,hayo maneno yenyewe kaandikiwa Lumumba kapewa kama script
 
Huyu Mufti ni sawa na Mary Chatanda wa UWT au Mohamed Ali Mohamed wa UVCCM. Wote ni wenyeviti wa matawi ya CCM.
Hawezi kuhubiri chochote kinachoweza weka taswira mbaya kwa CCM.
 
Azungumzie haki apokonywe posho,hayo maneno yenyewe kaandikiwa Lumumba kapewa kama script
Sheikh alishajiamulia bora ya tumbo lake linalolishwa na CCM kuliko kumtumikia Allah.

Land Cruiser lenye full ac, full tank, driver na nyumba ya maana Masaki. Ataimba mapambio ya kidumu chama cha mapinduzi mpaka mwisho wa uhai wake.

Huwa wanakwenda mbali zaidi na kupotosha mpaka Aya za Quran kuhalalisha mapambio yao.
 
Back
Top Bottom