MUFTI umeongea sana kuhusu Amani nchini lakini Bila kuzungumzia Haki usia wako unapwelea

MUFTI umeongea sana kuhusu Amani nchini lakini Bila kuzungumzia Haki usia wako unapwelea

Ndugu Mufti Zubeir
Kwa muda mrefu umezungumzia sana suala la amani nchini lakini huwa huzungumzii Haki, Pamoja na ujumbe wako wa amani hata hivyo kutokuzungumzia haki kunaufanya ujumbe wako upwelee.

Dini ya Kiislamu inataka amani lakini inakataza dhulma. Mafundisho ya kiislamu yanasema kuwa "Usidhulumu na wa wala usidhulumiwe". Sasa ndugu Mufti haya mafunzo wewe huwa huyafundishi, wewe umekalia amani, amani, amani. Sote tunataka amani lakini mbona wewe mwenzetu Haki huipi uzito?.

Wewe unafahamu amani na haki ni kama pande mbili za sarafu moja, lakini wewe umeshikilia upande mmoja tu wa amani, lakini suala la haki umelipa kisogo.

Rai yangu ni kwamba, kama unataka ujumbe wako usikilizwe na awananchi na wauzingatie, basi tetea haki hapo utakuwa na moral authority ya kuzungumzia amani. La sivyo ndugu Sheikh Mkuu nasikitika kwamba ujumbe wako wa amani yake wananachi tunayona kama ujumbe wa kisiasa zaidi kwa maslahi ya CCM.
Kaandikiwa hotuba na mi ccm huyo
 
Sheikh alishajiamulia bora ya tumbo lake linalolishwa na CCM kuliko kumtumikia Allah.

Land Cruiser lenye full ac, full tank, driver na nyumba ya maana Masaki. Ataimba mapambio ya kidumu chama cha mapinduzi mpaka mwisho wa uhai wake.

Huwa wanakwenda mbali zaidi na kupotosha mpaka Aya za Quran kuhalalisha mapambio yao.
Wapuuzi sana
 
Chadema mna mashehe na maaskofu wa ajabu ajabu
Mfano Askofu Mwamakula hana kanisa kabisa ulizia yeyote jengo la kanisa anakosali liko wapi? Hana ni kuzurura tu na Chadema kuponea posho za tonetone hana waumini ambao labda mngetarajia wawe wapiga kura wenu

Shehe ponda hana hata jengo la msikiti anakosalisha hana waumini kuwa atawasaidia kuwapa wapiga kura
Huu hapa msukule mwingine!!

Mtume Muhammad na Yesu Kristo walikuwa na majengo wapi? Nani alikwambia Imani na ibada ni majengo??

Kula ubwabwa ukalale wewe Imamu wa Msikiti
 
Back
Top Bottom