speech
JF-Expert Member
- Mar 4, 2022
- 484
- 1,266
Ila ameiomba serikali, sio kitu kibaya, serikal inaweza kukubali ombi lake au kukataaa...Swali, Je ni jukumu la Serikali kufanya masuala ya dini?
Pili,Kuomba Serikali ifanye sio vibaya maana ni ombi.
===
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amekemea ufisadi, akihimiza jamii kulinda maadili, umoja na mshikamano, huku akiwaomba viongozi wa Serikali na wadau kusaidia upatikanaji wa darubini ya kukusanya taarifa za mwandamo wa mwezi ili kumarisha uhakika wa taarifa.
View attachment 2596212
Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi ambacho waumini wa Kislamu duniani hufunga kwa siku 30 kabla ya kusherehekea siku hiyo kupitia taarifa rasmi va mwandamo wa mwezi huo.
Hata hivyo, kabla ya kusherehekea, kifaa hicho (moon sighting machine) ndio hutumika kupata uhakika wa mwandamo wa mwezi huo kimani ili kuondoa utata au mabishano miongoni mwa waumini hao.
Sheikh Zubeir amesema hayo leo Jumanne Aprili 22, 2023 katika swala ya Eid EI- Fitr iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Wilaya ya Kinondoni, jijini hapa, ikihudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mabalozi, mawaziri na watu mashuhuri.
Chanzo: Mwananchi
Sion sabbu ya kukemea, au kumkosoa mufti... Kwa sabbu sio kila unachoomba lazima upate
Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app