Mufti Zubeir: Serikali inunue chombo cha kutazamia mwezi
Ombeni ule utaratibu wa kufidia sikukuu zinazoangukia weekend urudi kama enzi ya Mzee Rukhsa.
Ile ilikuwa balaa, , mzee ruksa sijui aliwaza nini, nakumbuka nikiwa nasoma kuna wiki zilikatika siku nne za kazi zote hatuendi shule kwa ajili ya utaratibu ule ,yani kama tupo mid term leave .
Ulikuwa ni utaratibu wa kivivu sana .
 
Waislamu wanafungq kwa kuuona mwezi na wanafungua kwa kuuona mwezi ila sio kwa kuutafuta.Maana kwa darubini na vifaa vya kisayansi unaweza kuuona wakati wowote maana mwezi wenyewe upo muda wote.Pia serikali mkiitegemea kwa masuala ya dini ndio mnaipa nguvu ya kuwapangia kila kitu.Bakwata na nyinyi muwe na uungwana kidogo.Serikali imewapa chuo kikuu MUM,imewajengea msikiti mkubwa pale Kinondoni Shamba bado tu mnaifuata fuata?
 
Ila ameiomba serikali, sio kitu kibaya, serikal inaweza kukubali ombi lake au kukataaa...

Sion sabbu ya kukemea, au kumkosoa mufti... Kwa sabbu sio kila unachoomba lazima upate

Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app
kwa hiyo na TEC, CPTC na CCT nao wawe wanaombaomba kusaidiwa mambo yao? Why always BAKWATA kuombaomba/kutaka serikali iwafanyie mambo fulani ya dini yao wakati wanafahamu katiba ya nchi inatamka nini kuhusu dini na serikali?
 
Huenda serikali haikutaka watu wapumzike kazi ijumaa. Yote yawezekana chini ya bakwata ya serikali.
 
Tanzania ni nchi sekula which means haituhusu sisi kulipa kodi ili serikali inunue kifaa kwa ajili ya dini yoyote Km ambapo haituhusu kulipa kodi wajenge kanisa au msikiti. Km Raisi atatoa kw mshahara wake Km alivyonunua magoli ya mpira sawa ila haituhusu msituletee dini kw agenda za serikali, muhimu ni public things for all Km usafiri bora, afya bora, shule bora, ulinzi bora wa watu na watoto na kudhibiti uhalifu, ubakaji na mengineo. Wewe kuomba serikali inunue iko kifaa no diff than Samaki Samaki iombe speaker za disco; religion like sexuality is private not public goods so mtukome
 
Wanahaki ya KUOMBA kutoka Serikalini , Bakwata ni branch ndani ya ofisi ya Rais
 
Kauli sahihi ingelikuwa serikali iwatafutie wafadhili wa kuwapatia hicho kifaa kama walivyowapatia wafadhili wa kujenga huo msikiti. Wapo tele... wasiombe tende na nyama tuu
wajitafutie wenyewe, kuna taasisi nyingi nazo zikianza kuombaomba bora serikali iunde wizara ya kushughulikia mambo ya dini, na huko itakuwa imevunja katiba ya nchi
 
Hii nchi ni kama imezaliwa upya. Miaka yoote watu walikuwa wanafungua hata ikiwa mwezi umeonekana nchi jirani. Eti leo hii hadi kiongozi auone ndio atangaze eid! Nchi hii, Kazi kwelikweli!
 
Bakwata changisheni waumini wenu mnunue hicho chombo, serikali haina dini
 
Sijajua kama mmeishataja bei ya hicho kifaa.

Kama bado, je hicho kifaa kinauzwa bei gani ili tuone kama ni pesa ndefu mpaka kununuliwa na serikali au waumini wachache tu wanaweza kujichanga na kukinunua!
 
Mbona inasemekana lazima mwezi uonwe na macho makavu siyo mashine, by the way tukiamua kuchangishana wenyewe kwa wingi wetu hatuwezi kununua cha kwetu badala ya serikali
Mna amini nyie wengi? Mbona sensa ya 2012 mkagomea kisa ilitaka kujua wingi wenu?

Nyie hamfiki hata milioni 20
 
Zikitengwa pesa zilizolipwa na hao top 10 vipi utakua happy?
zikitengwaje? mbona hueleweki, na kwanini niumie na pesa ya private person? tunaongelea pesa ya public, kodi za wakristo na waislam kwenda kununua kitu cha dini moja. vipi kuhusu ile nyingine? mbona liko wazi tu?
 
Sijajua kama mmeishataja bei ya hicho kifaa.

Kama bado, je hicho kifaa kinauzwa bei gani ili tuone kama ni pesa ndefu mpaka kununuliwa na serikali au waumini wachache tu wanaweza kujichanga na kukinunua!
HILI LIFAHAMIKE KWANZA.

NAKAZIA
 
Back
Top Bottom