Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Punguza jazba basi, wamekusikia.
 
Upo sahihi lakini Kuna hako kajamaa kanaitwa dini Sasa. Utasikia " tutaishi kwa shida na raha mpaka kifo kitutenganishe"
Huyu dada alopigwa risasi amefanya kosa gani?
Hapo mpaka umpate mtu anayewajua au mwandishi wa habari za uchunguzi kama Ile case ya jamaa alomchoma mkewe kule kigamboni
 
Kwahyo ndoa inakengeusha
There you're! Mimi ni muumini wa ndoa, watu (mwanaume na mwanamke) waliokidhi vigezo kuishi pamoja katika ndoa maana ndio msingi wa familia na taifa bora.

Lakini ni ukweli watu wengi wameharibikiwa kiakili sababu ya ndoa. Tatizo hakuna mbadala wa ndoa; inabidi kuingia na kujifunza namna ya sahihi ya kuishi vinginevyo kuharibikiwa au hata kifo inahusu!

In summary, ndoa ni tamu ikienda sawa; ndoa itakuzingua usipoenda nayo kwa akili.
 
Commitment hawataki na kubaki bachelor hawataki.
 
Hao watoto Watakuwa kwa Taabu sana Psychologically , Especially huyo mkubwa na kama watakulia mazingira ya hapa Bongo , watakuwa stigmatized then Traumatized , Sijui hatua gani zinachukuliwa kuwalea watuto hao Kisaikolojia
Baadhi ya mali zitauzwa; Watafunguliwa trust fund ambayo itatumika kuwasomesha mpaka university. Atateuliwa ndugu wa kuishi na watoto mpaka hapo watakapojiweza wenyewe. Kwa kipindi chote hicho baba atakuwa jela kutumikia kifungo.
 
Watu wakifikia hatua ya kutoelewana, wengine huwa wanasema wabaki kuishi pamoja ili watoto wasiteseke ila kiuhalisia watoto huwa wanateseka humo humo ndoani. Unakuta wazazi wanapigana mbele ya watoto,unakuta mama anatukanwa mbele ya watoto, wazazi wanalewa mbele ya watoto,wazazi ngumi zinazidi hadi wanachaniana nguo na kubaki uchi mbele ya watoto. Hapo watoto hawateseki??. Ndio maana kuna msemo unasema" kama unawapenda watoto wako,mpende mke/ mumeo kwanza". Kama upendo baina ya wazazi umeisha,watoto lazima wateseke haijalishi wazazi wameachana au wanaishi pamoja, na uzuri watoto hasa wadogo wana hisia za juu, wanafahamu kila kitu kinachoendelea hata wazazi wakikosana watoto wanajua bila hata kuambiwa. Ubora wa ndoa ukipungua, watoto lazima waathirike tu haijalishi.
 
Baadhi ya mali zitauzwa; Watafunguliwa trust fund ambayo itatumika kuwasomesha mpaka university. Atateuliwa ndugu wa kuishi na watoto mpaka hapo watakapojiweza wenyewe. Kwa kipindi chote hicho baba atakuwa jela kutumikia kifungo.
Haya mambo yatafanywa na ndugu wa kibongo au ndugu kutoka nchi gani??.
 
Wanawake nao wanatakiwa waache Psychological torture.
Wanaume wanapitia mengi sana kwenye utafutaji wao.
Sio rahisi kama hawajampokea Kristo Yesu mioyoni mwao. Afya ya akili ya mtu hususani uimara wa kudhibiti hisia kali unategemea sana Afya ya Kiroho ya mtu.

Na Afya ya Kiroho haijengwi kwa Dini bali kuwa ndani ya Kristo Yesu.

MATHAYO 5
38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;

39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.

40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.

41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.

YOHANA 8
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
 
Upo sahihi lakini Kuna hako kajamaa kanaitwa dini Sasa. Utasikia " tutaishi kwa shida na raha mpaka kifo kitutenganishe"

Hapo mpaka umpate mtu anayewajua au mwandishi wa habari za uchunguzi kama Ile case ya jamaa alomchoma mkewe kule kigamboni
Hizo dini pia ndo zinasema watu wawe waaminifu,wapendane,waheshimiane etc.Kama wanandoa wangefuata mafundisho yao ya kidini kuhusu ndoa,wangeishi vizuri tu hadi kifo kiwatenganishe. Shida wanachagua mafundisho ya kufuata na ya kutokufuata. Mfano mzuri fundisho la " usizini" watu wanajifanyaga hawalioni. Watu waache unafiki,kama ndoa yenu inaendeshwa kwa sheria za dini, basi fateni sheria zote,kama inaendeshwa kidunia basi ipelekeni kidunia kwenye kila kipengele. Sio mnaendesha ndoa mnavyotaka halafu yakiwashinda ndo mnakumbuka mstari wa " mpaka kifo kitutenganishe".ilihali mstari wa " usizini au usimtendee mwenzako usivyotaka kutendewa" hamkuukumbuka.
 
Lakini pia watu wamekuwa wapenda mali zaidi kuliko utu. Kama mume na make wamejenga nyumba Moja si ya kwao ? Wanagombea nn??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…