Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Wanandoa mnapochokana, vyema kuachana kwa amani

Hata kama mna watoto pamoja, bora Mama awe hai na Baba awe hai, hao watoto watawatembelea kwa utaratibu utakaowekwa kisheria

Vinginevyo wanandoa wengi watauana kwa risasi ama sumu 🙌

Afya ya akili
Usikute sababu ya kufikia maamuzi hayo ni baada ya mchizi kujua hao watoto sio wakwake.
 
Wanasema majuto mjukuu, labda itumike hela kuizima hiyo kesi

Otherwise jamaa atafungwa.

Usipokuwa na moyo wa uvumilivu na kuachilia mambo, Kila siku watu watauana, hasa wanapohisi wake/waume zao ni malaika.

Kwamba hawawezi kukoseana
Babu kwa usalama wake itabidi tu afungwe wala asijaribu kutemper na kesi ili aachiwe huru. Imagine ndugu wote wanajua umemuua mkeo kwa risasi, watoto pia wanajua umemuua mama yao utaishi nani? Labda uende katavi ndani ndani ukaanza maisha ama sivyo utaishi uraiani kama uko jela tu.

Hasira ni hasara kwelikweli.
 
Hata mimi nilitaka kuuliza mbona

Unafikiri huyo jamaa alikuwa hana akili? Silaha alikabidhiwa vipi wakati inajulikana kichaa hapewi rungu? Watu wote huwa wanaakili zinazowatosha kutimiza mahitaji yao ila wakichokozwa ndyipo wanabadilika sa na kuwa roho ngumu, huwezi juwa huyo mkewe kamuudhi nini.
Uwezo wa ku control hasira nao n moja ya sifa za mtu mwenye akl tmam
 
Hii ndo utamaduni wa hapa Bongo,watu wanaoa/ kuolewa ili kuweka heshima kwenye jamii lakini muda huo huo wanaendelea na maisha yao na wapenzi wao wengine. Ile kujitoa kwa asilimia 100 kwa ajili ya ndoa hawataki,cha muhimu ndoa kwenye makaratasi ionekane ipo hata kama mioyoni haipo. Na jamii yetu haiangalii ndoa ina hali gani, cha muhimu msiachane. Ndo maana kauli za " vumilia,ndoa ndo zilivyo,hakuna mwanaume/ mwanamke wa peke yako" zimetamalaki.
Kila siku mi nazungumzia humu tabia ya watu kujifanya wanaoa/wanaolewa halafu wanaendelea na maisha yao mengine.

Kama mtu huwezi commitment baki bachelor wala sio kosa la jinai. Matatizo mengi ya ndoa yanaanzia kwenye kukosa commitment, Uchepukaji, kuficha mali, kutokushiriki kuzalisha mali za familia, kiburi, dharau, majivuno etc etc. Yote yana chanzo kimoja tu.

Ndoa inapaswa kuendeshwa kwa mapenzi na choice!
 
Oooh inasikitisha sana kwa kuukatisha uhai wa mtu.

Kunawakati dunia inasononesha sana kila kukicha na shida kubwa ni kuwa wapo watu hawakubali kuwa wao ni wafu watarajiwa.

Ki ubinadam tu,jombaa kafanya tukio hilo kutokana na hasira tofauti na hapo HAKUNA,lakini kwanini AMEUA?

Sawa,

Je,kwanini alishika siraha akiwa na hasira?

Ingalikuwa huenda mimi ni hakimu wa kesi yake wallah ningeenda pale sijui ndio ofisini kwake kiwa nimebebelea mzinga wa NYAGI kwa sababu ningetoa hukumu bila huruma.

Hili kosa ni moja kati ya makosa yanayofikirisha sana.Kisa ndoa?,kwahiyo tusioane au?

Brother Mbaga Jr inasikitisha sana jombaa,imagine mtu slafia kifungoni kisa nyuchi Ingawa haya maneno yako yamenifikirisha kiasi👇.
Muuliwa mchaga, muuaji mchaga, mwenyekiti mchaga 😂
Unataka kusema sisi(tisionachakupoteza)panatufaa au ni vile tumekata tamaa na maisha🤔?

Zaidi ya zaidi dear Mallerina unakumbuka post ya yule dada.isije ikawa ndio huyu alikuwa aking’ang’ania kuondoka kweye nyumba mzee baba akaona sio vibaya atumie trigger.

Yote ya yote ikifika hatu watu mkishindwana ni vyema muachane kwa wema.

Imagine sumu wanazoziweka katika mioyo yao hao watoto zinawingi ujazo gani?


Haya au tuseme wale watu laana ya kumwaga damu za waTanganyika inawarudia wao wenyewe🤔?

Baada ya hapo niishie kusema nimegundua uzuri na ubaya wa ndoa unasababidhwa na wanandoa wenyewe,kwa uelewa wangu.

Domino moja ikidondoshwa na nyingine zinafuata.
F69CE615-A6B6-4943-8355-597023A8ACF9.jpeg
Hivyo mliopo kwenye ndoa,hili tukio na mengine mengi yaliyopita na yakawe funzo kwenu na hata sisi amba tunatarajia kutoa laki 3 zetu.

MUNGU AIPUMZISHE SALAMA ROHO YA MAREHEMU.Amina
 
Back
Top Bottom