Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Duuh hao nao hawapendani mke ameshapata mchepuko.
Huenda sio mchepuko lkn pesa ya mwanamke huwa haiguswi mkuu.

Labda uwe na mke anayejitambua sana mara moja moja akupige tafu endapo umeyumba.
Vinginevyo siku zote wanaume ndio mtaji wa familia na jamii.
 
Umenena vyema bro
 
Hao sindio wanasemaga haki sawa hapo unataka waka teteenini mkuu.
 
Solidality ya nini mwanaume katoa sharti ya kukabidhiwa kadi au waachane ,kama hataki waachane ,mwanaume anao uhakika wa kumpata atakaye mpatia kadi na mwanamke anao uhakika wa kumpata ambaye haitaji kadi.
 
Matumizi mabaya kabisa ya mahakama ,wanaume wapo wengi huyo mwanamke kama hataki kutoa kadi akatafute mwanaume ambaye hajisumbui na kadi ya mwanamke wapo wengi,na wanawake wako wengi huyo mwanaume akatafute wapo wengi wanataka mwanaume wa kumpa hata nyumba sio kadi tu.Tusichoshane
 
Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Unaona sawa mwanamke kupeleka mshahara wake Kanisani.
 
Duuuh, umenikumbusha mjeshi mmoja alimtimbia kakobe chachi ilikuwa kizaazaa, mjeshi yupo misheni dafur sudan huku mke kila kitu kapeleka mwenge
 
Huenda sio mchepuko lkn pesa ya mwanamke huwa haiguswi mkuu.

Labda uwe na mke anayejitambua sana mara moja moja akupige tafu endapo umeyumba.
Vinginevyo siku zote wanaume ndio mtaji wa familia na jamii.
Motivational speakers bana.
 
Mwanamke akimlea mume wake wa ndoa iyo inaubaya gani?

Kwa mujibu wa mada iliyopo jamvini Mama hachangii chochote na anafanya kazi. Sasa apo ameoa au anaishi na hawara yake?
 
Uliyemquote hukumuelewa
 
Tatizo hamjalipima hili kwa upana ,Mimi kwa mawazo yangu naona jamaa anampenda mke wake na anaumia Sana mke wake kupeleka pesa kwa Hawa matapeli wachungaji uchwara.

Bora huyo mwanamke angekua anafanyia hizo pesa kwenye Mambo hata ya familia ya kwao ,kumbuka Wana watoto vipi huyo mama amewaza hatma ya watoto hapo baadae ,si Bora hizo pesa angesaidiana na mmewe kuwawekezea watoto.

Jamaa kutaka Atm ni Kama kumwokoa na ujinga alio nao.
Na hapo wakiachana ambaye anaenda kuwa na maisha magumu ni mwanamke maana tayar matapel washamkamata akil zake haambiw kitu Wala kusikia.

Inauma Sana upo na mwenzio wote mungu kawabarik kipato kidogo alafu mwingine anakichezea tu kwa kugawa kwa wachungaji feki.

Huyo mwanamke angekua anasaidia hata watoto wake tu huyo Jamaa asingekua na shida na Atm yake ,yaan kila kitu mwanaume sidhan km ndoa za watumishi waliooana zipo namna hiyo ,mkisaidiana hata love inakngezeka .
Swala la atm ni love tu ,mwez fulan anaweza enda na atm zote mbili mwanamke na mkapanga bajet kwa pamoja ,mwez mwingine akaenda yeyote ,ni swala la upendo tu na kusikilizana .
Narudia Tena huyo mwanamke anaenda kuishi maisha ya taabu Sana kwa kutaka sifa za huko makanisan na bahat mbaya amezalishwa hivyo hata Kama atapata bwana Basi yeye ndie anaenda kugharamika vibaya mno na mwisho wa siku atakuja jiona mjinga wa mwisho maana hakuna atakachokua amekikwepa hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…