Nimesoma UZI wote nikasoma comment za wadau nikasoma majibu ya muomba ushauri kupitia comment za watu nimebaini mambo kadhaa
1. Huyu ndugu kuna asilimia 87% hii issue siyo ya kweli ila tu anataka uzi uende na tuchat chat hapa.
2. Asilimia 13% zilizobakia kama ni za kweli basi ndugu huyu amesharidhia jambo hilo na ameshafanya maamuzi, kwa kuwa ushauri unaotolewa kumuunga hoja ndiyo anaoona huo ni sahihi, ila wa kumpinga na yeye anataka kukuhoji kwa nini umeshauri hivo.
3. Kama ni kweli na hajafanya uamuzi toeni ushauri kwa kujuwa tunadeal na mtu wa level gani na uwezo wake wa kufikiri ni wa chini sana.
Kuna sehemu amesema mama yake mkubwa alimwambia aende kuishi kwake coz bado mdogo.
Kwa hiyo anatoka kwa mama mkubwa anakwenda kwa shemeji na mke wake, na mke aliyeolewa kwa ushauri wa shemeji mtu.
USHAURI WANGU TU KWAKE AFANYE LILE ANALOONA KWAKE NI RAHISI NA LITAMPA FURAHA, MAANA HAPA DUNIAN TUNATAFUTA FURAHA KWA KILA JAMBO.