Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Adam hana wazazi, ni udongo uliopuliziwa pumzi. Yesu ndo mtoto wa maajabu anaye mama na baba wa kufikirika.
Umeona jinsi gani tumevurugwa ndugu yangu. Kumbuka Mungu kwenye biblia alisema amemfanya Adam kwa mfano wake. Ila Mtoto wake wa pekee ni Yesu. Yaani mtoto wa pekee angetakiwa kuwa Adam maana ndio kamuumba kwa mfano wake
 
Adam hana wazazi, ni udongo uliopuliziwa pumzi. Yesu ndo mtoto wa maajabu anaye mama na baba wa kufikirika.

Viumbe vyote vinazaliwa tena ni kwa matokeo ya mimba ambayo hutungwa kutokana na tendo maalumu la mwanamke na mwanamume sasa hiyo theory ya kupuliziwa udongo kiumbe kitokee unaona inakuja kweli?
 
Kumbukeni nilivyowambia nitakwenda na nitarudi, kama kweli mnanipenda mngefurahi na kushangilia maana nakwenda kwa baba: na baba yangu ni mkuu kuliko mimi°
Yesu anasema Mungu ni Mkuu kuliko yeye.
Yesu kasema au mwandishi ndio kasema,? na kama Yesu ndie kasema hayo Ww kwa nini unamwita Mungu. Au ni Mungu mdogo?
 
Kwa nini unaingiza suala la Waafrika wakati huko Ulaya, Marekani na Asia kumejaa dini ya Ukristo na nyingine nyingi!
Kwasababu wao ni dini zao haina shida kwao
 
Mungu ana mtoto, halafu akamtuma aje duniani kwa watu wenye dhambi, halafu yule mtoto akajitoa muhanga ili wale wenye dhambi wasamehewe yaani tena wasamehewe na Baba yake inaingia kweli akilini
 
Waafrika wengi bado wanaamini Brian Deacon ni yesu na picha zake wamepamba ndani, hawajui yule ni Raia wa Uingereza aliyelipwa pesa kucheza filamu ya yesu na kwa sasa anaendelea na kazi zake nyingine
 
Kwahiyo Mungu kazaa ndugu yangu maana Tunajua Tulio na Watoto ni Sisi Viumbe wake. Na Je Adam ni Mtoto wa Nani kulingana na Maandiko maana Kama Yesu ni mwanae wa Pekee Adam hana Wazazi
Mungu anazaa na alimzaa yesu kabla ya chochote kuwepo, Yesu ndio MWANZO. Adam aliumbwa, hakuzaliwa.
Nikupe siri moja ambayo huijui kwamba Yesu alishiriki uumbaji wa Adam.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Aisee kila mtu atabeba mzigo.wake msijidanganye kabisaaa ety kafa kwa ajili.ya dhambi zetu
Yni uue,uzini,uibe hlf useme kuna mtu kashanitubia dhambi zangu its non sense

Sasa mbona mnaenda makanisani ili msamehewe dhambi zenu? Na ubaya zaidi ety Pastor au Padri ndie anaesamehe dhambi wakati yy hpo anamichepuko kibao

kusema ukweli wakristo jitafakarini bhna mumeingizwa chaka na iyo imani yenu
Kabla ya Yesu kuja duniani, Mungu alikuwa anazungumza moja kwa moja na mwanadamu, baada ya kuja Yesu Mungu na mwanadamu wanazungumza kupitia Yesu Kristo.

Ndio msingi wa watu kuomba msamaha kila siku, sababu kama binadamu kukosea ni jambo lililo gumu kukwepeka kwa hiyo kila siku unaomba upatanisho na Mungu. Andiko sikupi sababu hata ukipewa hutaamini.
 
Yesu amesoma biblia au alishushiwa injili?
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu. Yesu alisoma torati iliyoandikwa na manabii kama Isaya, kwa hiyo jibu kwa swali lako ni NDIYO
 
Mungu anazaa na alimzaa yesu kabla ya chochote kuwepo, Yesu ndio MWANZO. Adam aliumbwa, hakuzaliwa.

Ndugu yangu unajua Kwamba Kuzaa Ni Sifa Ya Kiumbe. Huoni kama Unamtukana Mungu tusi kubwa Sana Kusema Anazaa. Maana Yake Yesu ana Mama Yake si Ndio?amabye Yupo huko alipo Ambaye si Mariam

Nikupe siri moja ambayo huijui kwamba Yesu alishiriki uumbaji wa Adam.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app

Umetoa Wapi haya Kwamba Alishiriki. Wakati Mungu Hashirikiani na Viumbe wake katika Uumbaji
 
Unatakiwa kujiuliza pia kwanini alikataliwa na Wanadamu. Mungu anaweza Kutuma Kitu halafu wewe ukakikataa kwa Akili ya Kawaida!? Halafu unamsifia Kwamba hakuna linaloshindikana kwake

Usimpambe pambe Tu. Mzaliwa wa Kwanza Wa Viumbe wakati hapo hapo mnasema ni Mungu. Mungu anakuwaj tena kiumbe

Mbona nabii yona unayemuamini wewe alikataa wito wa Mungu wa kwenda kuhubiri ninawi, Andiko linafafanuliwa na andiko. Lete maandiko kwamba Mungu hazai na hana mwana tujue mbivu na mbichi leo.
 
Habari za humu ndani!

Nawakaribisheni watu wote wakristo, waislamu, na watu wa dini zote kabisa katika majibu ya maswali ambayo yamekuwa yakiwatatiza sana kuhusu Uungu na Ubinadamu wa Yesu Kristo.

Maswali ya msingi kama;
1. Yesu ni nani? Ni Mungu au ni mwanadamu?
2. Kwa nini anaitwa mwana wa Mungu? Alifanyikaje mwana wa Mungu? Je Mungu anazaa? Mungu ana mke?
3. Nini maana ya kusema Mungu alizaliwa? Alizaliwa na nani?
4. Mungu anaishi wapi? Mbinguni ama Duniani? Je hapo alipoziumba mbingu na nchi alikuwa wapi kabla? Nini maana ya mbingu na nchi?
5. Mungu ana watoto? Watoto wake ni kina nani? Wanapatikanaje?
6. Kwa nini Yesu alikufa kwa ajili ya wanadamu? Je aliuwawa au aliamua kufa mwenyewe? Alifufukaje? Nini uthibitisho yupo hai leo? Ni kaburi wazi? Au ni zaidi ya hilo?
7. Ni wakati gani mtu anaokoka? Ni mambo gani yanatakiwa kuaminiwa ili mtu kuokoka?
8. Umeokoka? Uliamini nini? Unaweza kuelezea kwa maneno rahisi nini maana ya kuokoka?

Kumfahamu Yesu Kristo ndio ufunguo wa kufahamu mambo yote ya Mungu.

Huwezi kujifunza hili kwa dondoo/tips au memes. Hata masomo ya darasani huajifunzi na kufaulu kwa namna hiyo.

Kujifunza kunahitaji nidhamu na uvumilivu. Lazima uwe tayari na kusikiliza mpaka mwisho. Kwa miaka mingi Biblia imeonekana kama kitabu ambacho ni complex na chenye mkanganyiko lakini complexity na mikanganyiko hiyo ipo kwenye fahamu za wasomaji na si kwenye biblia. Kwa sababu ya watu kutokufundishwa kwa usahihi na kutumia kimakosa biblia.

Maswali yote hapo juu na mengine mengi yanajibiwa kwa ufasaha kabisa katika series za masomo ya audio yaliyo katika website yenye link hii https://kainosmedia.org/mafundisho/hapo-mwanzo-part-1/

Anza na somo la kwanza Hapo Mwanzo: Kuelezea “Yesu ni Mungu” (In The Beggining: Explaining “Jesus is God”) zipo sehemu 6. Tafadhali zisikilize zote kwa umakini kabisa. Nakuhakikishia ufahamu wako hautakuwa kama mwanzo tena.

Baada ya kusikiliza karibu kwa swali pale ambapo hujaelewa vizuri.

Furahia shule yako.
 
Umeona jinsi gani tumevurugwa ndugu yangu. Kumbuka Mungu kwenye biblia alisema amemfanya Adam kwa mfano wake. Ila Mtoto wake wa pekee ni Yesu. Yaani mtoto wa pekee angetakiwa kuwa Adam maana ndio kamuumba kwa mfano wake

Hahahahah unafurahisha sana kwamba mtoto wa pekee angetakiwa kuwa Adam. Soma maandiko ndugu uyaelewe na siyo kuja na majibu yako kichwani. Yesu ndio mwana pekee wa Mungu. Yesu ndio MWANZO. Amekuwepo kabla ya Adam na nikupe siri moja ambayo huijui,
Yesu alishiriki uumbaji wa Adam
 
Wakolosai : 1 : 15 - naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
Wakolosai : 1 : 16 - Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
vizuri sana
Enheeee yesu kazaliwa na nani?
 
Kijana naona unaendeleza tabia yako ya kukimbia maswali. Swali nililo anza nalo ni kuwa wapi Yesu alisema yeye ni mwana wa mungu au yeye ni Mungu.

Mkanukuu andiko toka kwa Luka, nikawataka mthibitishe huyo Luka amewahi kumuona Yesu kama hajamuona hayo maneno ameyapata wapi.

Kisha turudi huku.
Tabia yako naijua vizuri , unataka andiko ukilitewa unaanza thibitisha kama Luka amemuona Yesu , Kuna kipindi nilikuuliza hafs alimuona muhammad , na Pia niikuuliza Muhammad alimuona Issa? kama hakuwahi kuwaona habari alizitoa wapi?
Ukiacha Hypocrisy ndio utaweza jadili na watu
1 Yohana 2:22Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana.

Issue ya Yesu kuwa Mungu mnajibiwa kila kukicha ila mnakaza shingo
Koran 3:135.....na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu?........
Math 9:6Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo duniani wa kuwasamehe watu dhambi.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”
  • John10 27Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata. 28Mimi nawapa uhai wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu
    • Psalm 95: 6Njoni tusujudu na kumwabudu; tumpigie magoti Mwenyezi-Mungu, Muumba wetu! 7 Maana yeye ni Mungu wetu,nasi ni watu wa kundi lake,ni kondoo wake anaowachunga........
  • John 10:30 Mimi na Baba, tu mmoja.”31Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie. 32Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?” 33Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa ajili ya kazi njema, ila kwa sababu ya kumkufuru Mungu! Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe ni binadamu tu.
  • John 5:8Kwa sababu ya maneno haya, viongozi wa Wayahudi walizidi kutafuta njia ya kumuua Yesu; si kwa kuwa aliivunja Sheria ya Sabato tu, bali pia kwa kuwa alisema kwamba Mungu ni Baba yake, na hivyo akajifanya sawa na Mungu.
  • John 20:28Thoma akamjibu, “Bwana wangu na Mungu wangu!” 29Yesu akamwambia, “Je, unaamini kwa kuwa umeniona?
 
Akhi kweli Mungu hawezi kufa wala hajawahi kufa

Unahitaji kujua ukweli wa Mungu na utendaji wake kazi kwako, unatakiwa kujua Kristo ni nani na Yesu ni nani

Unatakiwa kujua kwanini Mungu aliamua kuja kwetu kupitia Kristo na ukishajua utasema kweli YESU NI MUNGU

Ukihitaji maelezo mazuri nitarudi baada ya kazi
Unajua sio kama nawaponda ila ukweli unajulikana
Hebu soma verse hii hlf utwambie Yesu ni Mungu
Yohana 20:17 NEN

Yesu akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”
 
Mbona nabii yona unayemuamini wewe alikataa wito wa Mungu wa kwenda kuhubiri ninawi,

Mimi siamini Hao Manabii unaowaamini wewe ndugu yangu. Na Ukiona Hivyo kwamba Yona Kamgomea Mungu basi Huyo Mungu hana Uwezo mana Hata Viumbe wake wanamgomea.

Kwa Akili Timamu huwezi sema Mungu hashindwi kitu Chochote kwake kinawezdkana Halafu uje Uniletee Stori za Nabij Yona Alimgomea Mungu.

Andiko linafafanuliwa na andiko. Lete maandiko kwamba Mungu hazai na hana mwana tujue mbivu na mbichi leo.

Mungu hazai ukimpa Hiyo Sifa Basi Baba Yako na Mama Yako Pia Ni Mungu si Wanazaa bhana. Nyie kila Siku mnaimba Hafafani na Yeyote ila Mnampa Sifa Ya Kuzaa Mungu akishazaa Basi Hana Tofauti na Wewe NA wanyama Wengine wanaozaa pia.

Unakimbilia Maandiko yako wakati Hata Huko hakuna Andiko linalosema Mungu kazaa
 
Back
Top Bottom