Habari za humu ndani!
Nawakaribisheni watu wote wakristo, waislamu, na watu wa dini zote kabisa katika majibu ya maswali ambayo yamekuwa yakiwatatiza sana kuhusu Uungu na Ubinadamu wa Yesu Kristo.
Maswali ya msingi kama;
1. Yesu ni nani? Ni Mungu au ni mwanadamu?
2. Kwa nini anaitwa mwana wa Mungu? Alifanyikaje mwana wa Mungu? Je Mungu anazaa? Mungu ana mke?
3. Nini maana ya kusema Mungu alizaliwa? Alizaliwa na nani?
4. Mungu anaishi wapi? Mbinguni ama Duniani? Je hapo alipoziumba mbingu na nchi alikuwa wapi kabla? Nini maana ya mbingu na nchi?
5. Mungu ana watoto? Watoto wake ni kina nani? Wanapatikanaje?
6. Kwa nini Yesu alikufa kwa ajili ya wanadamu? Je aliuwawa au aliamua kufa mwenyewe? Alifufukaje? Nini uthibitisho yupo hai leo? Ni kaburi wazi? Au ni zaidi ya hilo?
7. Ni wakati gani mtu anaokoka? Ni mambo gani yanatakiwa kuaminiwa ili mtu kuokoka?
8. Umeokoka? Uliamini nini? Unaweza kuelezea kwa maneno rahisi nini maana ya kuokoka?
Kumfahamu Yesu Kristo ndio ufunguo wa kufahamu mambo yote ya Mungu.
Huwezi kujifunza hili kwa dondoo/tips au memes. Hata masomo ya darasani huajifunzi na kufaulu kwa namna hiyo.
Kujifunza kunahitaji nidhamu na uvumilivu. Lazima uwe tayari na kusikiliza mpaka mwisho. Kwa miaka mingi Biblia imeonekana kama kitabu ambacho ni complex na chenye mkanganyiko lakini complexity na mikanganyiko hiyo ipo kwenye fahamu za wasomaji na si kwenye biblia. Kwa sababu ya watu kutokufundishwa kwa usahihi na kutumia kimakosa biblia.
Maswali yote hapo juu na mengine mengi yanajibiwa kwa ufasaha kabisa katika series za masomo ya audio yaliyo katika website yenye link hii
https://kainosmedia.org/mafundisho/hapo-mwanzo-part-1/
Anza na somo la kwanza Hapo Mwanzo: Kuelezea “Yesu ni Mungu” (In The Beggining: Explaining “Jesus is God”) zipo sehemu 6. Tafadhali zisikilize zote kwa umakini kabisa. Nakuhakikishia ufahamu wako hautakuwa kama mwanzo tena.
Baada ya kusikiliza karibu kwa swali pale ambapo hujaelewa vizuri.
Furahia shule yako.