Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani


hapana siji na story za tunda usibeti.

huoni kama hilo tunda lilikuwa ni la muhimu sana mpaka wewe sasa hivi unajiamulia tu utoe ndogo au uichunge!!!

maana kabla njia ilikuwa ni moja tu,hakuna hata anayejua hata kama inaliwa.
 
MPAKA SASA UPO NEUTRAL

kaka robert kadri unavyozidi kusoma naona unafunguka kuwa tu mkweli kama sisi mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na nguvu zote hayupo.
Wanazunguka zunguka sana kukiri kwamba Mungu hayupo.

Yani wana jaribu kutafuta tafuta sababu za kuonesha Mungu Yupo lakini wanakwama.

Hawawezi kukubali kwamba Mungu hayupo.
 
Huwezi ukasema ni hiyari wakati usipofanya anavyotaka yeye anakuchoma moto. Anatulazimisha
Ni hiyari, QUR'AN inasema 'na tumemjaalia/mpa binaadam njia mbili,imma afuate njia ya kukufuru au ya kushukuru'..ni kama kwenye misosi tu uchague pilau nyama choma au bia,gongo nk..
 
Kama moto hakuna basi hakukuwa na sababu ya Yesu kufa msalabani, haya ni maandiko yanayothibitisha uwepo wa moto hivyo ni vyema ujue hivyo kuwa baada ya maisha ya duniani kuna kwenda motoni au mbinguni

Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.

Matayo 3:12

bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

Waebrania 10:27

Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;

Marko 9:47

Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,

Matayo 13:49

na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Matayo 13:50

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Ufunuo 21:8
 
Ukishiba unaanza kukufuru, Mungu yupo ni wajibu wetu tumtii, tumpende, tumwabudu na tumtukie

Malipo ya dhambi ni mauti
 
Mzee wa kazi kumbe ukitulia unaandika madini sana..
 
anafanana na binadamu mkuu
 
Source ya mawazo hayo ni ipi ? kama hakuna source wala ushahidi bali ni mawazo yako basi yatakosa nguvu kwa maana mtu yeyote anaweza kuja na mawazo tofauti na yako akiwa amebuni baada ya kushiba kande.
 
Haloo, nimeishia njiani siwezi kumalizia kusoma huo ni upotoshaji namim sitaki kupotea kama wewe, maana yako nishaijua yaan huna tofauti na serikali kuhusu suala la bandari wako katkat kurudi nyuma hawawezi kwenda mbele nako imekuwa ngumu, ko ata wewe na wenzio najua hauko peke yako... yaani mnajifariji kwakuwa mmejikinai kwa kutenda maovu ndipo sa huoni pa kukimbilia ko mmeamua kujitaftia namna ya kujifurahisha katika dhambi, lakini ukweli ni kwamba nafsi lazima inakushtaki tu, ushauri wangu....mungu anasamehe kabisaaa na unaanza maisha mapya...
 
Hivi wewe naomba nikuulize, iv unajua kwanini upo hai/umeletwa duniani ili iweje! ukinijibu hilo naungana nawewe kwenye imani yako
 
Umesema kwasasa ni wapiii?
 
Why people wanalazimisha uwepo wa Mungu while ukifikiria kwa undani kuna vitu unaona kabisa havipo sawa ... wat daz it mean? Ina maana mimi pekee ndie mwenye ubongo mbovu au mim nafikiria tofaut na wengine au shida ni ipi hasa mpaka nakuwa tofauti na wengine kwenye kufikiria haya mambo?
 
Kwanini umeamua kusema hayo? Mbona ni Mungu mwenyewe anayekuambia kuwa moto ameandaliwa shetani na wafuasi wake? Kwani wewe umeamua kuwa mfuasi wa shetani? Kwanini hutaki kufanya toba na kumrudia Mola wako?

Hakika anasema tumwelekee kwa toba, ibada, sadaka na zaka. Mungu wetu ni mwema sana. Tukimfuata hakika tutaufikia ufalme wake wa furaha na amani.
 
Bado hujaionja furaha ya kuwa ndani ya Yesu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…