Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Atheist sio dini
 
Mungu muumba mbingu na nchi anawezaje kuwa Pendo, Kwenye Dunia yenye Uovu, Mabaya, Magonjwa na Majanga ya asili kama radi, mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga?

Huyo Mungu mwenye upendo yupo kweli?
MUNGU NI PENDO HAIJALISHI WEWE UNAMWONAJE !!
 
Kama wewe huamin hakuna ni uhuru wako kuamini hivyo sababu hujashikia fimbo umwamini

Lakin sis wengine tunaamini mbingu ipo tutaendelea kuamini
Ungebaki kanisani/misikitini wala hata usingeona tuna argue.

Naheshimu haki za watu kuamini watakacho.
Imani haina kanuni, unaweza kuamini hata jiwe tu.

Umeleta mjadala hapa JF kunasibisha imani yako mimi nakuomba uithibitishe madai yako.

Umeleta imani yako kwenye ulingo huru, mimi nkikuuliza kuhusu imani yako hapo nakuwa sijaingilia uhuru wako.

Unaelewa hilo?

Kwanini mnatueleza masuala ambayo hamuwezi kuyatetea humu kwenye mijadala iliyo wazi kwa watu wa mitazamo yote?
 
MUNGU NI PENDO HAIJALISHI WEWE UNAMWONAJE !!
Ni sawa kwa mtazamo wako.

Ila kwenye Dunia yenye Uovu, Mabaya, Magonjwa na Majanga ya asili kama radi, mafuriko, vimbunga na matetemeko ya ardhi huyo Mungu mwenye Upendo Hayupo.

Na hawezekani kuwepo.
 
Oyaa Msabato kaamka na akili za isiku huku 😂🤣🏃‍♂️
 
Mimi sifahamu fika chanzo cha huo ulimwengu.

Na naamini hakuna ajuaye zaidi ya nadharia tu,

Wewe unaweza kuwa unajua chanzo cha hayo uliyoyasema ili unieleze nami nisiwe mjinga tena!?
Ni kisema chanzo cha ulimwengu na vilivyomo ni Mungu ndy aliye viumba wew kwanini unabisha ilihali hujui chanzo chake?
 
Hayo ni matokeo ya kuumba ulimwengu ambao hawezi kuu control????
 
Mleta mada kuna kitu haelewi kwa nini Mungu anataka waovu mwisho wa siku awachome moto

Kaweka amri .zake zile lazima tutii.Sio kuwa tumtii yeye tu la zinaleta utengamano ndani ya dunia ili tusiumize wengine.Makosa mengi tunayotaka eti.Mungu atusamehe yanaumiza wengine na Mungu hataki mtu muumiza.wengine ndio maana mwisho wa siku ni motoni.

Mfano anasema usizini unazini na kumpa ukimwi mtu mwingine wewe ni wa kuchomwa moto kabisa muuaji mkubwa unaumiza wengine



Anasema usiibe unaibia wengine kwa kupitia njia mbalimbali ziwe ujambazi nk.na kuwaachia machungu makubwa wengine kwa wizi wako mwisho wa maisha Mungu.kaweka moto jitu.kama wewe ni motoni tu

Lingine unaambiwa usiseme uongo unadanganya watu na kuwatapeli na kuwaumiza pakubwa mwisho wa siku motoni

Unaambiwa usiue wewe unaua watu kwa njia mbali za.uchawi,nk unataka Mungu akakuweke wapi ukifa.Hana sehemu bora ya kuweka mtu kama huyo ni motoni tu

Moto umewekwa mahususi kwa wote wasiotaka kuishi kwa kutii amri za Mungu za kufanya Binadamu waishi kwa utengamano

Usipotubu dhambi na kuziacha na kuokoka moto jehanamu unakusubiri
 
Hivi wewe naomba nikuulize, iv unajua kwanini upo hai/umeletwa duniani ili iweje! ukinijibu hilo naungana nawewe kwenye imani yako
Yupo hai au tupo hai kwasababu mazingira unayoishi yanaruhusu uwe hai....

Mtoe samaki majini muweke nchi kavu kwamuda fulani alafu rudi majini waulize ulio waacha kwanini wapo hai
 
Ni kisema chanzo cha ulimwengu na vilivyomo ni Mungu ndy aliye viumba wew kwanini unabisha ilihali hujui chanzo chake?
Una uthibitisho kwamba Mungu ndie chanzo cha ulimwengu na vilivyomo?

Toa uthibitisho wa kwamba ndiye chanzo cha ulimwengu sio kuishia kusema tu.

Kwa nini unalazimisha ulimwengu uwe na chanzo na Mungu asiwe na chanzo?

Chanzo cha Mungu ni kipi?
 
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kutenda mabaya?

Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na Uovu?
 

Hao wanyonge wanaodhulumiwa nao wanadhulumu waliochini Yao.

Labda useme, vipi wenye Haki wanaodhulumiwa hapo utakuwa na hoja. Lakini dhulma Kwa mnyonge anayedhulumu wa Chini yake naona ni Ulimwengu wao.
 

Walioweka Amri NI miungu.
Mungu Muumba WA mbingu na nchi yeye alichotaka ndicho kinachofanyika.

Huwezi mfundisha Mbwa Kubweka.
Wala huwezi mfundisha mbuzi Kula majani.

Kwanza Mungu Muumba WA mbingu na nchi hajawahi kuonekana wala Sauti yake haijawahi kusikika popote pale. Huyo anayesema amri Fulani ni za Mungu Mkuu ni muongo. Sema amri za miungu kulingana na asili na tamaduni za Watu.
 
Na asipokuelewa hapa ndo basi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…