Mungu ulikuwa wapi wakati wa biashara ya utumwa?

Mungu ulikuwa wapi wakati wa biashara ya utumwa?

Kwa hiyo mafundisho yake yliruhusu mtumwa au kukomboa utumwa?
 
Mimi nadhani Mungu aliamua kuacha mambo yajiendee ili tuweze kujionea maisha yatakavyokuwa apart from Him.. na tumeona kuwa sisi wanadamu hatuwezi kujitawala/kujiongoza bila msaada wa Mungu........"O LORD, I know the way of man is not in himself;it is not in man who walks to direct his steps" (jeremiah 10:23)......
 
Kwani we ulikuwa wapi?

Mwaaaaaaaaaaa! Pilipili hapa (in eliud's voice)
 
Mimi nadhani Mungu aliamua kuacha mambo yajiendee ili tuweze kujionea maisha yatakavyokuwa apart from Him.. na tumeona kuwa sisi wanadamu hatuwezi kujitawala/kujiongoza bila msaada wa Mungu........"O LORD, I know the way of man is not in himself;it is not in man who walks to direct his steps" (jeremiah 10:23)......
mkuu kama ni msomaji mzuri wa maandiko ya vitabu hivi vinavyoitwa vya dini utagundua hakuna wakati binadamu aliishi Kwa amani tangu kuumbwa kwake ... Hakuna ni machafuko tu na machafuko mengine Mungu eti aliruhusu yatokee sasa kama ndo hivyo Kwa Nini anajinadi ana upendo
 
Habari wana JF

Ni muda mrefu nimekuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu uwepo wa Mungu lakini kuhusu masimulizi yanayo elezea matendo yake mazuri na huruma kuu Kwa viumbe wake.
Mungu kupitia wajumbe wake hapa duniani na maandiko yanadai Mungu ni mwema na mwenye huruma sana lakini ukitafakari Kwa kina unapata ukakasi kuhusu madai yao kuhusu Mungu huyo.

Katika historia ya maisha ya mwanadamu hapa duniani hakuna nyakati ngumu alizopitia kama nyakati za biashara ya utumwa, biashara ya utumwa iliwagusa na kuwamiza zile jamii ambazo ni dhaifu zisizo weza kujitetea hivyo tegemeo lao kubwa lilikuwa ni Mungu mkuu.Bahati mbaya Mungu hakuja kuwatetea na kuwapigania.

Kama Mungu yupo kila mahali, ni mjuzi wa kila jambo na muweza wa mambo yote Kwanini alijificha na hakuja kuwapigania wanadamu wake...Tuna ambiwa Mungu aliandaa mipango ya kuwatoa wana wa Israel utumwani misri na akawatumia viongozi ili kufanilisha misheni hiyo 🥺 kwanini hakufanya hivyo Kwa jamii zingine wakati wanachukuliwa watumwa haswa Afrika?

Mungu ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini wakati huo inaumiza sana 😭
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo hata leo.

Angekuwepo, usingeweza hata kuwa na swali kama yupo.
 
Hata sasa Mungu bado anawakomboa watu dhidi ya utumwa wa dhambi au wewe huoni Mkuu?. Huoni watu wanavyostaafu ukahaba,ujambazi,utapeli,ushoga n.k?. Yesu hakuja duniani kuzurura!

Na wangapi wanageuka makahaba, majambazi na matapeli kila siku?
 
Mimi nadhani Mungu aliamua kuacha mambo yajiendee ili tuweze kujionea maisha yatakavyokuwa apart from Him.. na tumeona kuwa sisi wanadamu hatuwezi kujitawala/kujiongoza bila msaada wa Mungu........"O LORD, I know the way of man is not in himself;it is not in man who walks to direct his steps" (jeremiah 10:23)......

Miaka 400? Kweli imani ni ugonjwa wa kufisha aisee
 
Habari wana JF

Ni muda mrefu nimekuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu uwepo wa Mungu lakini kuhusu masimulizi yanayo elezea matendo yake mazuri na huruma kuu Kwa viumbe wake.
Mungu kupitia wajumbe wake hapa duniani na maandiko yanadai Mungu ni mwema na mwenye huruma sana lakini ukitafakari Kwa kina unapata ukakasi kuhusu madai yao kuhusu Mungu huyo.

Katika historia ya maisha ya mwanadamu hapa duniani hakuna nyakati ngumu alizopitia kama nyakati za biashara ya utumwa, biashara ya utumwa iliwagusa na kuwamiza zile jamii ambazo ni dhaifu zisizo weza kujitetea hivyo tegemeo lao kubwa lilikuwa ni Mungu mkuu.Bahati mbaya Mungu hakuja kuwatetea na kuwapigania.

Kama Mungu yupo kila mahali, ni mjuzi wa kila jambo na muweza wa mambo yote Kwanini alijificha na hakuja kuwapigania wanadamu wake...Tuna ambiwa Mungu aliandaa mipango ya kuwatoa wana wa Israel utumwani misri na akawatumia viongozi ili kufanilisha misheni hiyo 🥺 kwanini hakufanya hivyo Kwa jamii zingine wakati wanachukuliwa watumwa haswa Afrika?

Mungu ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini wakati huo inaumiza sana 😭
dunia na vilivyomo ni mali ya ibilisi.
ulimwengu huu na serikali na mali na kila kitu vipo chini ya ibilisi.
yesu aliambiwa kama angekubal kumsujudia angepatiwa vyote.

kwaio usimlaumu Mungu chochote,
huu ulimwengu utapotea na kuharibiwa ili uje ule mpya ambao mwenye kuubuni na kuujenga n mungu mwenyewe.
 
Meaning Mungu alikosa njia nyingine nzuri na sahihi hadi kutumia njia ya kutweza utu wa watu... Ila tuna ambiwa yeye ni mbora kwenye kupanga why alishindwa katika hili
Malizia "watu weusi" kama anaona ni binadamu
 
Ukiondoa waarabu wa north Africa. Waafrika waliobaki hawana mashikamano yoyote na dini zote zilizopo wala miungu yao. Kama wengi wakiendelea kujiuliza "inakuaje mtu aliyekugeuza mtumwa akupe kitabu cha dini kwa nia njema?" Basi soon zitatokea dini zetu wenyewe kama Indians na most Asian cultures.
 
Soma biblia kumbukumbu la torati mstari 28 majibu yako yanapatikana hapo
 
Tukisema Mungu aliwapendelea zaidi Wazungu, swali likuja why ?
Basi huyo mungu ni mshenzi mmoja anayetakiwa kupopolewa kwa mawe huko aliko. Hilo swali tayari ni upuuzi tosha, kwani unatambua wazi watu hufanya vitu kwa kujipendelea na huyo mungu wamemtengeneza wao kwa ajili yao. Wewe wamekuletea ujichanganye kama hivi ili wakutawale kiurahisi. Nini cha ajabu hapo?
 
Haya mambo ukiyafikiria sana utapoteza muda wako. Ukisoma kitabu cha Joshua utaona mauaji ya kimbari (genocides) yaliyofanyika kwa baraka za Mungu wa waisrael. Sio poa kabisa
 
Utumwa ilikuwa ni Njia ya Mungu ili aweze kufika Afrika. Tofauti na hapo tungekuwa tunaabudu Magogo na Milima
Anhaa, so unasema huyo Mungu wako amekuona hauna maana na amekudharau vya kutosha kiasi cha kushindwa kukutumia mjumbe hata mmoja kama alivyofanya kwao badala yake akatumia utumwa, mauaji na udhurumishi wa washenzi waliokuja na hiyo dini ili usiabudu magogo? Na bado unaona huyo Mungu wako ni mwema na yupo? Hiyo ndiyo hoja yako fikirishi? Smh.

Na kuna ubaya gani kuabudu magogo? Kuna tofauti gani na kuabudu sanamu la mzungu aliyepigwa misumari ubaoni? Unaogopa kuwa tofauti? Asians wanaoabudu masanamu yao vilevile, wewe umewazidi nini?
 
Back
Top Bottom