Wanabodi...
Poleni na majukumu ya week nzima, as we are welcoming another beautiful weekend.
Naomba tuongelee hili swala kidogo, tumeaminishwa kuhusu uwepo wa Mungu na miujiza yake ya kuponya viwete, kutenganisha bahari na hata kurudisha uhai kwa wafu.
Je Mungu huyo yupo?
Maana nimefika point sasa najiuliza sana, ya kuwa what if dini ni utapeli wa kihisia na imani kwa kitu ambacho hakipo?
What if miujiza tunavyo ambiwa kuwa ukiomba utapata ni kama dhana ya kutuweka tuendelee kuwa watumwa wa shida unazo zipitia?
Maana mimi nilisoma shule za kikatoliki na tukikuwa tunasali sana rosali kila siku, japo ilikuwa na msaada katika masomo na kutupa imani iliyo thabiti, ila bado watoto walikuwa na tabia mbaya sana,
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na Visungura, zile pombe za pakti. Vijana walikuwa wanavusha na kunywa, watu walikuwa wana ruka ukuta, na ikifika rosali wanasali na kutubu...
Ila pia hata kwenye maisha, watu wanahudhuria makanisani, ila bado wanazini na wake za watu,
Watu wanakesha makanisani ila bado wanafanya dhambi na kwenda tena kuomba Mungu awasamehe, je ndugu zangu dhambi ni kitu kibaya?
Mapadri wenyewe tu pia wanalala na kuzaa na wanawake kisiri
Sijawahi kuona mbwa anahudumiwa kwenda kuimba nyama jikoni, atapigwa na atajifunza kumbe kuchukua nyama ni kosa! sijawahi kuona dhambi ikiwa applied kwa kiumbe kingine ila binadamu tu.
Unakaa unajiuliza ni kwanini binadamu tunawekewa hukumu katika vitu na desire za kimwili ambazo muda mwingine ni haja za kinyama kabisa?
Je dini ni illusion? Na kama ni kweli kwanini binadamu amekuwa mgumu kukubali kuwa hakuna mtu aliye juu mawingu I anayemwangalia kila jambo analolifanya na kuna siku atamuhukumu kwenda kuchomwa moto wa milele?
Ndugu zangu, weekend hii tutaenda makanisani...
Je unakwenda kumwabudu Mungu, aliyeshuhsa mana katika ghalika la waizraeli? Ndiye Mungu aliye sambaratisha bahari ya shamu? Au ni tunakwenda kuabudu Mungu aliye bumbwa kwenye taswira ya binadamu wa kale?
Sijasema Dini ni mbaya, wala sijaikataa Dini ila nataka kujua na kuuliza ni kwanini binadamu hufwata kitu kisicho na maana kwa ajiri ya kupata comfort ya muda mfupi?
Lakini pia wanaoikataa Dini mbona hamna mahala mnaposema kuwa hichi mlicho kikuta kimeanzia, na chimbuko la mwanadamu ni hili? Kwa nini Msiwe delusional tu, ilihali mnapendana na kutaka a mema kwa manufaa ya jamii iliyo bora?
Mimi naamini kila kitu ni energy na hata hawa wanaoa mini katika Dini si kwamba hawako sahihi, energy is incomprehensible hasa kwa limits zilizo kwenye mlango ya fahamu, so expression ya hiyo energy lazima iwe abstract, ndo maana kuna vitu kama miujiza, which are manifestaion of energy forms.
Swali ni je, Mungu huyo tunayekwenda kanisani kumwabudu ni yupi? Na mbona unaendelea kwenda ilihali hatumjui? (kwa sisi ambao hatujamwona)