Mungu wa miujiza mbona sijawahi kumwona? Au kuona miujiza yake?

SIku ukiweza kuachana na kuwaza maswala ya dini na mambo yake ,bac nikuhakikishie mkuu utaangaika hata nayo tena .maana dini n miradi ya watu kama ww vile uamue kuanzisha tu mradi wako na uangalie soko lako litakuwa ktk nchin gan upige hela za wateja na ndicho katoliki na islami walichowini ktk bara hili la GIZA .
 
Ni
inahitaji kufahamu big bang theory kwanza?
Nime quote swali lako hapo chini, niliuliza hivo ili nijue mtazamo wako inakua rahisi kidogo kuelezea
 
Reactions: Lax
.


Ni ngumu kuthibitisha uwepo wa mungu bila kumuhusisha na chochote.
Basi Mungu huyo hayupo.

Kutumia vitu vingine visivyo na uhusiano wowote na huyo Mungu, kuvihusisha na huyo Mungu, ili kuonyesha uwepo wake ni kufanya logical fallacy inaitwa Non-sequitur.

Unaunganisha vitu viwili tofauti visivyokuwa na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.

Ni sawa uniambie nijitetee kizimbani bila ushahidi
Sasa pia, utasemaje Mungu yupo bila ushahidi na uthibitisho?
 
Imani ni Mtihani wa "Ghaibu" (Mambo Yasiyoonekana/unseen )

Lengo la maisha ya dunia ni mtihani. Kama Mwenyezi Mungu angeonekana waziwazi kwa macho ya kila mtu, kusingekuwa na maana ya "Imani" (kuamini kisichoonekana) na kusingekuwa na mtihani tena, kwani kila mtu angelazimika kuamini.
Qur'ani inaanza kwa kusifu wale wanaoamini mambo yasiyoonekana kwa macho lakini yanathibitika kwa akili na mioyo:

"Hichi ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uwongofu kwa wacha-mungu. Ambao wanaiamini ghaibu (yasiyoonekana)..." — (Surat Al-Baqarah, 2:2-3)

Nihitimishe kwa kusema kuwa :

Huwezi kumwona Mungu kwa macho, lakini unaweza kumwona kupitia kazi Zake. Kama vile usivyoweza kuona upepo au akili, lakini unaona athari zake—vivyo hivyo ulimwengu thabiti, mapigo ya moyo wako, na mifumo ya nyota ni ushahidi na miujiza tosha ya uwepo wa Muumba.
 
Lengo la mtihani ni nini mkuu
 
Mungu yuko nje ya mfumo wa Muda
Kwanza thibitisha uwepo wa Mungu kabla ya kusema yupo nje ya mfumo wa muda.

Mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.

Unarukia kusema tu, Mara ooh! Yupo nje ya mfumo wa muda.

Wakati bado hujathibitisha kwamba yupo.
Big Bang ndiyo iliyotengeneza Muda na space

Yule aliyesababisha Big Bang llazima alikuwepo kabla ya muda kuanza.

Na huyo ndo Mungu- alikuepo na ataendelea kuepo
If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.

Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi.

Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.

Huyo Mungu hawezi kuwepo tu, from nowhere.
 
Unathibitishaje kwamba mifumo ya ulimwengu ni kazi ya Mungu?

Au unafosi tu?
 
Neno Imani linamaana ya kuamini mambo yaliyofichikana kwa yakini kutoka moyoni pasi na chembe ya shaka ndani yake.
Suala la kusema kuwa bora niamini tu kuwa Mungu yupo ili hata nisipomkuta niwe safe huu ni UNAFIKI. Ina maana bado moyo wako unashaka.

Pia mwanadamu mwenye akili hawezi kuhangaika kutafuta miujiza ya Mungu ili hali Mungu kaweka kila aina ya ishara za uwepo wake ndani ya miili yetu na mazingira yanayotuzunguka.

Kinachotakikana ni kukaa na kutulia kisha utafakari jinsi ulimwengu unavyofanya kazi kuanzia asubuhi mpaka usiku. Kisha jiulize Je hays yamefanyika tu bure out of nowhere?
 
If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.
Imani yangu mizizi yake imejikita kwenye Big bang,. Neno "kuumbwa" au "kusababishwa" linahitaji uwepo wa muda (ili kisababishi kitokee kabla ya tokeo). Kwa sababu Mungu yuko nje ya mshale wa muda, hana mwanzo wala mwisho, hivyo haitaji kuumbwa. Yeye ndiye "Chanzo Kisichofungwa na Chanzo Kingine" (The Uncaused Cause).
 
Lengo la mtihani ni nini mkuu
Mungu kaweka huu mtihani ili aone nani miongoni mwetu atamuamini na kisha kutenda vitendo vyema.


Quran 67:1-2

" AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha"
 
Soma Waebrania 11 1 Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
 
hapo swala ni kujiuliza binadamu tumetokana na nini hapo ndo utagundua kuwa mungu yupo au hayupo
 
Ni wakati gani ulimwengu haukuwepo kisha ukawepo kwa kuumbwa na huyo Mungu?
 
Kuna namna yeyote ya uwezekano wa upendeleo katika mchakato huo?
 
hapo swala ni kujiuliza binadamu tumetokana na nini hapo ndo utagundua kuwa mungu yupo au hayupo
Mungu hayupo.

Mama yako alikuzaa. Wala hukuumbwa na huyo Mungu.

Binadamu hawaumbwi. Na wala hatukuumbwa.

Binadamu, tunazaliana wenyewe kwa wenyewe.

Na wala hatuhitaji muumbaji.

Kama kila kitu kilichopo kitahitaji muumbaji, Basi hata huyo muumbaji na yeye atahitaji muumbaji wake mwingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho exist chenyewe tu pasipo muumbaji.

Na hivyo kutakuwa na msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji wengi, pasipo kukoma. Endless to infinite.

An infinite regress of causes is an endless chain of events where every cause has its own prior cause going back forever.

There is no first event, no start, and no uncaused beginning.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…