Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Ndipo ilipo tofauti kati yetu,

Umesema mwisho wako ni kaburini.

Sisi tumwaminio kristo hatuna mwisho, sisi ni WA MILELE, kaburi Haina nguvu juu yetu maana tumeshinda MAUTI na kuzimu.
Kuna kipindi jamaa mmoja alinitishaga na kunipandikizia Roho ya mauti. Nilikuwa naogopa sana kuhusu Mauti. Bwana akaniambia, unaogopa nini wakati wana wa Mungu hawafi utalala tu kusubiri siku ya kuamsha kwako.

Hili lilinijenga sana na toka kipindi kile, siogopi tena Mauti.
 

Kwa sasa hana kiburi kwani hukumu yake ilishaandikwa. Hana kiburi chochote na ni mboga sana na ndio maana alikimbilia baharini akiamini Moto aliohukumiwa nao hautawaka kwenye maji. Anajua siku zake zimekaribia na anadanganya watu wasiojitambua tu ila hana lolote wala hana nguvu kwa muamini.
 
Mlokole anaweza kubadilika katika maombi akawa kama Malaika na kwenda kumsaidia mtu au kumfungua aliyefungwa au kuibiwa nyota.

Wana wa ufalme, waliookoka, Tumepewa mamlaka na uwezo mkubwa mno, tatizo ni kutokutumia mamlaka yetu vizuri.
Mlokole anaposali na akianza kulia tu na kumsifu mungu wake mnaita kunena kwa lugha,basi anakua ni roho sio binadamu tena.Lakini yeye anajiona yupo kawaida kumbe pale yupo kiroho.Mungu wa walokole anajua hesabu ya walokole wote duniani ila wanajimu wanashindwa kuhesabu hesabu kamili ya walokole wote,sababu mda wote wale walokole wanafunikwa na pinde za rangi tofauti tofauti na wakati mwingine wanafunikwa na mabawa ya wale watu warefu
 
USHAURI:Fuata aliyoyaagiza tu ,ukiyatimiza kisha ukaenda Jehanam hapo utakuwa na uhalali wa kusema ulilosema
 
Samahani mkuu unaweza kuadithia kidogo ilikuaje??
 
Ni sahihi kabisa mtumishi japo Hilo la nyota ni fundisho la uongo. Binafsi nikishaona mtumishi anaongelea kuhusu nyota huwa simsikilizi wala mfuatilia kwani namuona ni tapeli.
Kuna wanajimu wanajiita walokole na wachungaji ila kwenye ulimwengu wa roho ni waganga na wachawi.
 
Huu ni ushuhuda wangu mwenyewe. Mwaka 2017 nilihama toka nilipokuwa mwanzo na kuhamia nilipo sasa. Nilipofika, nilikuwa nasali kwa nguvu na kuhubiri mtaani. Watu wengi wa mji huu, walikuwa wananikwepa nilikutana nao barabarani. Wengine walikuwa hawanisogelei karibu na hata watu wazima tena machifu kuniamkia "Shikamoo".

Hapa namaanisha nini? Ukiwa na alama na moto wa kimungu, waganga, wachawi, wanajimu na washihiri watakukimbia na kumuogopa kama simba.
 
Tupe madini mkuu tufunguke akili tumepotezwa muda mrefu na hizi dini
 
Unakua unatembea na nguzo za moto pembe nne zote za mwili wako.Unakua pamoja na wale watu warefu wa kuakusi mwanga unaopofusha macho
 
Ni sahihi kabisa mtumishi japo Hilo la nyota ni fundisho la uongo. Binafsi nikishaona mtumishi anaongelea kuhusu nyota huwa simsikilizi wala mfuatilia kwani namuona ni tapeli.
Katika maandiko nyota zimeandikwa.

Mungu ametukataza kupiga BAO au kutafuta habari za yajayo na nyota kupitia uganga.

Anataka tumuulize na kumtegemea Yeye pekee kupitia Roho MTAKATIFU.

Niliposema nyota, nilimaanisha NAFSI. NAFSI ya mtu inaweza kufungwa kuzimu, pangoni, chooni, barabarani au chini ya kitanda nk nk,

Wakati NAFSI ya mtu imefungwa Mahali pengine, Pepo hukaa ndani ya mtu, wakati mtu halisi hayupo.

So kwenye nyota weka NAFSI mtumishi.

Amen.
 
Hizo ni sifa za Mungu katika dini ya Uislamu.
Kila dini Ina sifa za Mungu wake, usiforce standards unazotumia wewe zifanane na za wengine. Dini kama ya Kihindu, Mungu wao anaonekana sasa utamuambia nini Mhindi?
Ni sahihi, Mungu wetu tumeuona na watu wake wamemuona toka enzi na enzi. Toka Adam, Isaya, Daniel, Mikaya, Ezekieli hadi Yohana pale kisiwani patimo wameona "yule mzee wa siku nyingi" yeye aliye "mfano wa mwanadamu" ambaye kichwa chake ni Nywele safi mfano wa sufu, yeye aketiye juu ya majeruhi, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi kilicho na magurudumu ya moto na mbele yake kuna mto mkubwa wa moto na maelfu kwa maelfu wanaotumikia.

Nina ushuhuda kuhusu ufunuo huu. Mungu wetu yu jirani nasi, yu rafiki na Baba mwema kwetu. Yeye anatupenda na anatutaka nasi tumpende ili awe karibu nasi.

Nakumbuka akaniambia " Umepata Neema na Bahati katika kizazi hiki kuniona na kusikia sauti yangu"
 
Hapa tukaenda tofauti, hakuna sehemu yoyote mtumishi imefundisha kuhusu nyota. Toka utoto wangu hadi sasa uzee wangu, toka naanza kusoma Biblia nikiwa darasa la nne hadi sasa, sijawahi ona kuhusu fundisho la ukombozi wa nyota. Yesu hajafundisha wala mitume hawajafundisha kuhusu nyota mkuu. Pia NAFSI ni tofauti na hsifanani wala fananishwa na nyota.

Sawa, tuendelee.
 

Amen
 
Thanks but you have not replied my questions;

  • do they use the same Bible?
  • and if they believe that Jesus stays in their heart etc than what are the current beliefs of those attending the Churches of the Catholics and Lutherans?

- Why do the preachers utilize 'oil' and charge for 'treatments'??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…