Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Ndipo ilipo tofauti kati yetu,

Umesema mwisho wako ni kaburini.

Sisi tumwaminio kristo hatuna mwisho, sisi ni WA MILELE, kaburi Haina nguvu juu yetu maana tumeshinda MAUTI na kuzimu.
Kuna kipindi jamaa mmoja alinitishaga na kunipandikizia Roho ya mauti. Nilikuwa naogopa sana kuhusu Mauti. Bwana akaniambia, unaogopa nini wakati wana wa Mungu hawafi utalala tu kusubiri siku ya kuamsha kwako.

Hili lilinijenga sana na toka kipindi kile, siogopi tena Mauti.
 
Na huyu mkuu wa jamii za baharini kwanini anakiburi mpaka sasa,wakati Jehova na mwanaye Yesu kristo wameshamuandikia adhabu na hukumu kali na angalia anajua na kutambua pia yakwamba Jehova ambaye ni mkuu wa anga za juu sana ananguvu na anatisha sana kuliko yeye? Au ana kiburi cha ujinga, na upumbavu au ameamua kujitoa muhanga huyu mkuu wa jamii za baharini?

Kwa sasa hana kiburi kwani hukumu yake ilishaandikwa. Hana kiburi chochote na ni mboga sana na ndio maana alikimbilia baharini akiamini Moto aliohukumiwa nao hautawaka kwenye maji. Anajua siku zake zimekaribia na anadanganya watu wasiojitambua tu ila hana lolote wala hana nguvu kwa muamini.
 
Mlokole anaweza kubadilika katika maombi akawa kama Malaika na kwenda kumsaidia mtu au kumfungua aliyefungwa au kuibiwa nyota.

Wana wa ufalme, waliookoka, Tumepewa mamlaka na uwezo mkubwa mno, tatizo ni kutokutumia mamlaka yetu vizuri.
Mlokole anaposali na akianza kulia tu na kumsifu mungu wake mnaita kunena kwa lugha,basi anakua ni roho sio binadamu tena.Lakini yeye anajiona yupo kawaida kumbe pale yupo kiroho.Mungu wa walokole anajua hesabu ya walokole wote duniani ila wanajimu wanashindwa kuhesabu hesabu kamili ya walokole wote,sababu mda wote wale walokole wanafunikwa na pinde za rangi tofauti tofauti na wakati mwingine wanafunikwa na mabawa ya wale watu warefu
 
MI KINACHONISIKITISHA

Ni kama KILA kitu kilipangwa kabla hata misingi ya ulimwengu haijakuwepo!!

Yaani hata hao wa jehanam na hao wa peponi walipangiwa kuwa fate yao itakua hivyo!!

Unafikiri huyo shetani alipoumbwa na kuwa shetani ilikua by surprise!!?

Yaani chanzo kikuu cha vyote hivi ni muumba mwenyewe hakuna Bahati mbaya wakuu!!

Uwepo wa shetani,moto,pepo vyote ni mpango KAZI hata hao watakaoingia ni mpangokazi rasmi hakuna Bahati mbaya KWA lolote itategemea yeye muumba alikuandikia nini coz hakuna anaewez and kujifanya mtakatifu wala muovu isipokua KWA Mapenzi yake yeye aliemuumba yeye na pande ZOTE mbili yaani shetani na upande wa pili!!!

Ni hayo tu!!
USHAURI:Fuata aliyoyaagiza tu ,ukiyatimiza kisha ukaenda Jehanam hapo utakuwa na uhalali wa kusema ulilosema
 
Kuna kipindi jamaa mmoja alinitishaga na kunipandikizia Roho ya mauti. Nilikuwa naogopa sana kuhusu Mauti. Bwana akaniambia, unaogopa nini wakati wana wa Mungu hawafi utalala tu kusubiri siku ya kuamsha kwako.

Hili lilinijenga sana na toka kipindi kile, siogopi tena Mauti.
Samahani mkuu unaweza kuadithia kidogo ilikuaje??
 
Ni sahihi kabisa mtumishi japo Hilo la nyota ni fundisho la uongo. Binafsi nikishaona mtumishi anaongelea kuhusu nyota huwa simsikilizi wala mfuatilia kwani namuona ni tapeli.
Kuna wanajimu wanajiita walokole na wachungaji ila kwenye ulimwengu wa roho ni waganga na wachawi.
 
Nina maswali mengi, ila nianze na Hili. ...

Ulisema hao watu warefu wakikugusa Ile alama haifutiki. Na ukasema katika ulimwengu wa roho inaonekana.Ina maana Ile alama wachawi wanaiona muda wote? Na wachawi wakiiona wanafanyeje? Wanaiheshimu Ile alama au mtu mwenye Ile alama? Au wanamfanyia ubaya? Au Ile alama inawaogopesha wachawi?
Huu ni ushuhuda wangu mwenyewe. Mwaka 2017 nilihama toka nilipokuwa mwanzo na kuhamia nilipo sasa. Nilipofika, nilikuwa nasali kwa nguvu na kuhubiri mtaani. Watu wengi wa mji huu, walikuwa wananikwepa nilikutana nao barabarani. Wengine walikuwa hawanisogelei karibu na hata watu wazima tena machifu kuniamkia "Shikamoo".

Hapa namaanisha nini? Ukiwa na alama na moto wa kimungu, waganga, wachawi, wanajimu na washihiri watakukimbia na kumuogopa kama simba.
 
NINAENDELEA.......!!!!
WANAJIMU NA WAGANGA :Wanajimu na waganga hawana usharika na walokole katika lolote lile.Wao ni washirika wa wale watu warefu wa baharini.Unajimu haufundishwi kwenye mikusanyiko ya kilokole sababu una makufuru na hatua zake nyingi zina ushirikiano na uganga.Wanajimu wanachukua nyota za wangu na kuzitumia kwa manufaa yao.Wanajimu wanafanya tafukuri ambayo ni laana kiroho.Wanajimu hawana utii kwa mkuu wa mamlaka aliye mkuu wa wote,bali wao wanatii uganga wako na miungu ya kwenye sayari za ndani ya mfumo ww jua wa ulimwengu.Wanajimu wanashirikiana na wale viumbe wa baharini kumuhujumu mwanadamu aliepo duniani.Wanajimu wanatafuta elimu ya anga kwa njia za uchawi wa kale wa kiarabu na kiajemi.Wanajimu hawana maombi ya kubariki bali wana maombi ya kulaani,kwani kwao laana ni sehemu ya matambiko yao.Hivyo wanajimu ndani ya ulimwengu wa kiroho sio watu wema.
WALE VIUMBE WAREFU :Kama nilivyosema pale mwanzo kua,kuna aina mbili za wale viumbe warefu
MOJA :Watu warefu wa angani wanaoakisi mwanga
MBILI :Watu warefu wa baharini wasioakisi mwanga.
WATU WAREFU WA ANGANI WANAOAKISI MWANGA :Wale watu warefu wazuri kwa muonekano,wanaoshika panga na kulinda walokole ni watu wa ajabu sababu ya tabasamu zao na upendo wao.Akikusogelea kwa karibu utatamani ulie kwa furaha maana unapata amani ya moyo iliyopitiliza.Wana upendo mkuu sababu ukiona jinsi wanavyowahudumia walokole lazima upendezwe nao.Walokole ni kama vitoto vidogo mbele ya hawa walinzi wao ""Watu warefu""..Upenda na ulinzi ndio sifa yao kuu.Wao ni moto ndani ya moto wa shaba,wana nguvu kama umeme wa radi.Kimuonekano wengine wana mabawa na wengine hawana mabawa ila wote warefu kwa vimo.
WATU WAREFU WA BAHARINI WASIOAKISI MWANGA :Hawa ni washirika wa waganga na wanajimu na wachawi.Kimuonekano ni watu wa kubadilika badilika.Hawana muonekano mzuri wa kudumu bali wanachukua sura halisi za binadamu,hasa binadamu wa bara hindi na uajemi.Hawana usharika na walokole sababu walokole wanaharibu kazi zao wanazofanya na wanajimu na wachawi.Hawana upendo wala amani ya moyo wakikusogelea,zaidi zaidi utasisimka na kuogopa.Ni washirika wa mkuu wa ulimwengu mwenye vita vya kudumu na walokole.Tusiwazungumzie sana hapa maana lengo sio kuwazungumzia wao bali Mungu wa walokole.
Kwa binadamu wa kawaida unakua na amani ukikutana na hawa watu warefu wa angani ambao ni walinzi wa walokole,maana wanalinda watoto,wanalinda wagonjwa,wanalinda walokole na wasiokua walokole na wanazuia majanga ya kutengenezwa na wale watu warefu wa baharini na washirika wao ambao ni wachawi na wanajimu na waganga na washirikina wa kibinadamu.Popote pale duniani kwenye ulimwengu wa kiroho utawaona wanaruka huko na huko.
Afu mungu wa walokole ambae ni mkuu wa mfumo wa anga kuu nje ya mfumo wa sayari za ulimwengu kaficha siri ya mfumo wa ulimwengu nje ya mfumo wa anga na sayari zote,,maana angani ni kama mfumo wa anga na sayari unaelea ila huwezi jua umejishikiza wapi.
Hesabu za kinajimu zina kikomo ila hesabu za unajimu wa nje ya mfumo wa ulimwengu hazina kikomo na zinaongozwa na mwana wa mmliki.Na ndio maaana huyo mwana wa mmliki na wale watu warefu weupe wanaishi milele toka dahari ya kwanza mpaka dahari isiyo na ukomo kwa kingereza wanaita""Eternity's""".
Walokole wanaposali ndio mda mzuri wa kua nao sababu mungu wao anashuka kwa njia kuu tatu(3)
MOJA :Kama njiwa mweupe wa dhahabu
MBILI :Kama moto wa mataji ya viduara na kukaa vichwani mwa walokole
TATU :Kama wingu za moto unafunika eneo zima.
Sasa kama walokole wakiwa wanasali na wewe upo karibu basi baraka zao kiroho zinakufikia mpaka wewe.Mungu wa walokole hana ubaguzi katika kutoa baraka kwa bunadamu,ni kama anatusubiri tumjue atubariki.Lakini pamoja na upole wake,huyu mungu wa walokole ana mzaha pale unapotaka kudhuru walokole wake na haoni hasara kukuua kwa pumzi yake ya moto.Anawapenda walokole wake kuliko kitu kingine chochote.
NITAENDELEA..... ....!!!!
Tupe madini mkuu tufunguke akili tumepotezwa muda mrefu na hizi dini
 
Huu ni ushuhuda wangu mwenyewe. Mwaka 2017 nilihama toka nilipokuwa mwanzo na kuhamia nilipo sasa. Nilipofika, nilikuwa nasali kwa nguvu na kuhubiri mtaani. Watu wengi wa mji huu, walikuwa wananikwepa nilikutana nao barabarani. Wengine walikuwa hawanisogelei karibu na hata watu wazima tena machifu kuniamkia "Shikamoo".

Hapa namaanisha nini? Ukiwa na alama na moto wa kimungu, waganga, wachawi, wanajimu na washihiri watakukimbia na kumuogopa kama simba.
Unakua unatembea na nguzo za moto pembe nne zote za mwili wako.Unakua pamoja na wale watu warefu wa kuakusi mwanga unaopofusha macho
 
Ni sahihi kabisa mtumishi japo Hilo la nyota ni fundisho la uongo. Binafsi nikishaona mtumishi anaongelea kuhusu nyota huwa simsikilizi wala mfuatilia kwani namuona ni tapeli.
Katika maandiko nyota zimeandikwa.

Mungu ametukataza kupiga BAO au kutafuta habari za yajayo na nyota kupitia uganga.

Anataka tumuulize na kumtegemea Yeye pekee kupitia Roho MTAKATIFU.

Niliposema nyota, nilimaanisha NAFSI. NAFSI ya mtu inaweza kufungwa kuzimu, pangoni, chooni, barabarani au chini ya kitanda nk nk,

Wakati NAFSI ya mtu imefungwa Mahali pengine, Pepo hukaa ndani ya mtu, wakati mtu halisi hayupo.

So kwenye nyota weka NAFSI mtumishi.

Amen.
 
Hizo ni sifa za Mungu katika dini ya Uislamu.
Kila dini Ina sifa za Mungu wake, usiforce standards unazotumia wewe zifanane na za wengine. Dini kama ya Kihindu, Mungu wao anaonekana sasa utamuambia nini Mhindi?
Ni sahihi, Mungu wetu tumeuona na watu wake wamemuona toka enzi na enzi. Toka Adam, Isaya, Daniel, Mikaya, Ezekieli hadi Yohana pale kisiwani patimo wameona "yule mzee wa siku nyingi" yeye aliye "mfano wa mwanadamu" ambaye kichwa chake ni Nywele safi mfano wa sufu, yeye aketiye juu ya majeruhi, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi kilicho na magurudumu ya moto na mbele yake kuna mto mkubwa wa moto na maelfu kwa maelfu wanaotumikia.

Nina ushuhuda kuhusu ufunuo huu. Mungu wetu yu jirani nasi, yu rafiki na Baba mwema kwetu. Yeye anatupenda na anatutaka nasi tumpende ili awe karibu nasi.

Nakumbuka akaniambia " Umepata Neema na Bahati katika kizazi hiki kuniona na kusikia sauti yangu"
 
Katika maandiko nyota zimeandikwa.

Mungu ametukataza kupiga BAO au kutafuta habari za yajayo na nyota kupitia uganga.

Anataka tumuulize na kumtegemea Yeye pekee kupitia Roho MTAKATIFU.

Niliposema nyota, nilimaanisha NAFSI. NAFSI ya mtu inaweza kufungwa kuzimu, pangoni, chooni, barabarani au chini ya kitanda nk nk,

Wakati NAFSI ya mtu imefungwa Mahali pengine, Pepo hukaa ndani ya mtu, wakati mtu halisi hayupo.

So kwenye nyota weka NAFSI mtumishi.

Amen.
Hapa tukaenda tofauti, hakuna sehemu yoyote mtumishi imefundisha kuhusu nyota. Toka utoto wangu hadi sasa uzee wangu, toka naanza kusoma Biblia nikiwa darasa la nne hadi sasa, sijawahi ona kuhusu fundisho la ukombozi wa nyota. Yesu hajafundisha wala mitume hawajafundisha kuhusu nyota mkuu. Pia NAFSI ni tofauti na hsifanani wala fananishwa na nyota.

Sawa, tuendelee.
 
Mlokole anaposali na akianza kulia tu na kumsifu mungu wake mnaita kunena kwa lugha,basi anakua ni roho sio binadamu tena.Lakini yeye anajiona yupo kawaida kumbe pale yupo kiroho.Mungu wa walokole anajua hesabu ya walokole wote duniani ila wanajimu wanashindwa kuhesabu hesabu kamili ya walokole wote,sababu mda wote wale walokole wanafunikwa na pinde za rangi tofauti tofauti na wakati mwingine wanafunikwa na mabawa ya wale watu warefu

Amen
 
Kwanini walokole wana nguvu?

Jibu: Walokole wamemkaribisha YESU akae ndani yao, wanamuamini kwa Kila wafanyalo, hii inafanya sasa Mlokole awe ananguvu maana anayemtu anamsaidia ambaye ni Roho Mtakatifu

Kwanini sio wanaosali makanisa kama Lutheran na Catholics?

Jibu: Wanaosali makanisa hayo ulivyotaja pia wapo waliookoka nao wanazo nguvu, ila wengi wao hawana nguvu hizo, ni kwakuwa wao wanaishi kwa Sheria za kanisa na mazoea...
Thanks but you have not replied my questions;

  • do they use the same Bible?
  • and if they believe that Jesus stays in their heart etc than what are the current beliefs of those attending the Churches of the Catholics and Lutherans?

- Why do the preachers utilize 'oil' and charge for 'treatments'??
 
Back
Top Bottom