Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Hao walokole hawana utambulisho wa makanisa.Wana utambulisho wa kiimani tokea kanisa lolote.Na sio kila mkristo ni mlokole.I hope you understand swahili.
Katika ulimwengu wa Roho kuna watu wa namna tatu.
1. Kuna wanaotembea uchi ( Watemda dhambi na waasi)
2. Kuna wenye mavazi meupe (Wakristo wasio na maombi na wasio na ushuhda mzuri).
3. Kuna wenye mavazi meupe na wamezungukwa na nuru kali ya moto. Hawa wana mioto na mwanga mkali kwenye mioyo yao na wenye paji za uso wao.(Walokole) hawa hawatambuliki kwa makanisa yao, bali hatambuliwi kwa utakatifu na maisha yao ya maombi na ushuhuda.
 
Katika ulimwengu wa roho wanasema hakuna.Sababu huyo mungu wa walokole anamiliki ulimwengu wa nje ya mzio wa kawaida wa sayari na minyongeo yake.Na hizo jamii nyingine za ulimwengu wa nje hazipendi kumzungumzia zinamwita mmiliki wa jua nyota na mwezi.
Pia wanamuita Mwana wa mmiliki au MWENYE HAKI.
 
Nawakumbyka wale wawili nilio kaa nao na kuishi nao zaidi ya miezi 6. Akaniambia, mmoja ni kwa ajili ya ulinzi wako na mwingine ni kwa ajili ya riziki zako. Huu uzi umenirudishia na kuniongezea imani yangu. Malaika wapo na ni kweli.
Wale watu warefu wanaoakisi mwanga wa jua????? Wanaishi ndani ya pumzi za moto.
 
Pia wanamuita Mwana wa mmiliki au MWENYE HAKI.
Au mzee wa siku nyingi[emoji123]

Danieli 7:9
[9]Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
I beheld till the thrones were cast down, and the Ancient of days did sit, whose garment was white as snow, and the hair of his head like the pure wool: his throne was like the fiery flame, and his wheels as burning fire.
 
And what about the other Christians who attend recognized Churches such as Roman Catholic and Lutherans?

To add;
  • Does the Mlokole read the very same Bible as Roman Catholic and Lutherans? if yes, than what makes them 'superior' in being able to see 'Angles, Blue Circles' etc etc
  • Why do the other preachers such as Mwamposa etc use:
  • 'oil' as a supposed healing method?
  • Create 'clinics' with different charges and why so, if they feel 'superior' or 'special'?
Kwanini walokole wana nguvu?

Jibu: Walokole wamemkaribisha YESU akae ndani yao, wanamuamini kwa Kila wafanyalo, hii inafanya sasa Mlokole awe ananguvu maana anayemtu anamsaidia ambaye ni Roho Mtakatifu

Kwanini sio wanaosali makanisa kama Lutheran na Catholics?

Jibu: Wanaosali makanisa hayo ulivyotaja pia wapo waliookoka nao wanazo nguvu, ila wengi wao hawana nguvu hizo, ni kwakuwa wao wanaishi kwa Sheria za kanisa na mazoea...
 
Anasema alikaa na viumbe wanaoitwa"""Malaika"""""miezi sita!!!
Zaidi ya Miezi sita nilikaa nao, nikiwaona na kushuhudia uwepo wao pindi niombapo au niombeapo wengine au nikihubiria wengine habari njema za Yesu Kristo. Ni kweli wale watu warefu, wanatembea kwa kasi, hawagusi ardhini wanapotembea, wana nguvu, wanavaa mavazi/kanzu nyeupe, wana sura nyeupe na inayong'aa kama jua wapo na ni halisi. Simu moja wakanichukua hadi Mbinguni. Waliniambia, tumetumwa tukuchukue.
 
Nitaleta ushuhuda wangu kuhusu Mungu wa walokole, Muonekano wake kwa sasa na muonekano wake kwa jinsi ya mwili alipokuwa duniani.
Huu uzi wako umeimarisha na kuinua imani yangu kwa Mungu wa walokole. Nakumbuka jinsi alivyonitokea.
Mkuu mimi natamani hata kesho nipate access ya kukaa na mungu wa walokole au wale watu warefu wenye haki usoni mwao.Ninapata faraja kuona kumbe kuna watu mnamfahamu huyu mkuu wa wakuu,mmliki wa mfumo wote wa ulimwengu na nje ya ulimwengu.Kila siku namchunguza sababu jinsi unavyomchunguza ndio unavutiwa nae.
 
Amina, Mungu wa walokole akutane na haja ya moyo wako mkuu.
 
Zaidi ya Miezi sita nilikaa nao, nikiwaona na kushuhudia uwepo wao pindi niombapo au niombeapo wengine au nikihubiria wengine habari njema za Yesu Kristo. Ni kweli wale watu warefu, wanatembea kwa kasi, hawagusi ardhini wanapotembea, wana nguvu, wanavaa mavazi/kanzu nyeupe, wana sura nyeupe na inayong'aa kama jua wapo na ni halisi. Simu moja wakanichukua hadi Mbinguni. Waliniambia, tumetumwa tukuchukue.
Mkuu napokuandikia ujumbe huu,ujue wewe ulibarikiwa kupata bahati ya kushirikiana na wale watu wa haki ambao ni washirika wa walokole wanaomwakilisha mwana wa mmliki ambae wanajimu wanamwita""NYOTA YA MASHARIKI NA MSHINDI WA MLIKI ZA ANGA.!!!
 
Kwanini walokole wana nguvu?

Jibu: Walokole wamemkaribisha YESU akae ndani yao, wanamuamini kwa Kila wafanyalo, hii inafanya sasa Mlokole awe ananguvu maana anayemtu anamsaidia ambaye ni Roho Mtakatifu

Kwanini sio wanaosali makanisa kama Lutheran na Catholics?

Jibu: Wanaosali makanisa hayo ulivyotaja pia wapo waliookoka nao wanazo nguvu, ila wengi wao hawana nguvu hizo, ni kwakuwa wao wanaishi kwa Sheria za kanisa na mazoea...
Umesoma andiko lote?amesema walokole wamo kwenye makanisa yote na hata nje ya makanisa ikiwemo mashambani,kazini,barabarani n.k,tena kwenye makanisa mengine yanoyojiita ya kilokole/pentecostal walokole hawamo kabisa kwa hiyo akasema ulokole ni mahusiano ya mtu na Mungu sio mahali anaposali.
 
Kuna vitu vingine inabidi ufikilie kwa akili ya ubinaadamu siyo lazima uende shule ukasoma, nafasi ya Mungu kwa binadamu ni kila kitu, yeye alikuwepo, yupo, atakuwepo daima.

Pole sana ndugu yangu, lakini ujuaji wetu huu wote mwisho wake ni kaburini, halafu Mungu mwenyewe kaweka pazia, kiasi kwamba hatuna nafasi ya kuludi tena kuja kusahihisha makosa yetu
Ndipo ilipo tofauti kati yetu,

Umesema mwisho wako ni kaburini.

Sisi tumwaminio kristo hatuna mwisho, sisi ni WA MILELE, kaburi Haina nguvu juu yetu maana tumeshinda MAUTI na kuzimu.
 
Back
Top Bottom