Muonekano wa kichwa cha Treni ya SGR

Muonekano wa kichwa cha Treni ya SGR

Kichwa hiki cha Mkandarasi kinachotumia nishati ya umeme kimewasili bandarini jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuanza majaribio ya miundombinu ya umeme katika reli ya kisasa - SGR kipande cha Dar es Salaam - Morogoro.View attachment 2126501View attachment 2126502View attachment 2126503View attachment 2126504


Ebu elezea vizuri, hii ni nini? Kitakuwa ndio kichwa cha Treni cha TRC au ni kwa ajili tu ya majaribio na kitaondolewa? Hii sio kabisa, mbona old sana hii
 
Mkandarasi analeta vichwa vingapi vya majaribio kuna kile cha kwanza cha njano kilianguka na picha zilisambaa tena ndio hukitumia kubeba viongozi wakitembelea mradi sasa haya majaribio mpaka lini tupo nje ya muda hawana uhakika na ujenzi wao
 
Huu mtumba una sura mbaya kama kichwa cha panzi ndio mama kaamua kuuleta, aache utani na watanzania? Ama kuna asilimia yake hapo maana vichwa hivi si vya kisasa kabisa..
Hiki ni kichwa cha mkandarasi yeye kaleta kwa ajili ya majaribio tu
 
Huu mtumba una sura mbaya kama kichwa cha panzi ndio mama kaamua kuuleta, aache utani na watanzania? Ama kuna asilimia yake hapo maana vichwa hivi si vya kisasa kabisa..
"Kichwa hiki ni cha mkandarasi" acha upotoshaji mkuu
 
kenya.JPG


800px-Kenya_Railways_DF8B_locomotive_on_the_new_SGR_line,_06-06-2017.jpg

Hizi za Jirani vipi?
Zina uafadhali?
 
Pathetic.
Hivi watu wengine wakienda nchi za nje wanaangaliaga nini?
Hicho si Kama vile vya Kenya MSA ..NBI masaa 8 halafu wsnaita SGR.
Jamaa hivi unajua maana ya SGR? Naona umekurupuka tu kama ngiri.
Soma na elewa maana ya Standard Gauge Railway ndio utoe comment.
 
Huu mtumba una sura mbaya kama kichwa cha panzi ndio mama kaamua kuuleta, aache utani na watanzania? Ama kuna asilimia yake hapo maana vichwa hivi si vya kisasa kabisa..
Ungemwekea vichwa vya kisasa mkuu, ili ajue watanzania wa sasa sio mambumbumbu.
 
Kwann kimechorwa logo za trc
emoji848.png
Mbona kimekuwa branded na tanzania
Sidhani kama suala la branding linaweza kuwa issue...

1. Pale Pugu Road kulikuwa na jengo liliandikwa Quality Plaza wakati mmkili hakuwa Yusuf Manji

2. Pale jirani na KAMATA kuna jengo limeandikwa Mkuki na Nyota wakati mmiliki sio Mzee Walter

3. Leo hii unaweza kuwa na kampuni kwa mfano ukaita DeepPond Airways na ukawa unatumia ndege za kodi na bado logo kwenye hizo ndege zitakuwa DeepPond Airways ingawaje wewe sio mmiliki wa hizo ndege

Jambo la msingi ni hiyo taarifa ime-describe vipi hicho kichwa cha treni...

...Cha Mkandarasi... Majaribio!!

Tusisahau, ile reli ni ya umeme kwahiyo LAZIMA pafanyike electric traction testing. Mwenye wajibu wa kufanya hiyo testing ni Contractor anayefanya tract electrification.

Kutokana na hilo, I strongly believe hicho kichwa na leased (or owned) by the contractor kwa ajili ya kuja kufanya hiyo testing. Hiyo branding, isiwape taabu... ni maandishi tu hayo! Na kwavile kichwa kimesafirishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine, ni vema kuki-label ili in case of anything, ifahamike kinaenda wapi hasa!!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Huu mtumba una sura mbaya kama kichwa cha panzi ndio mama kaamua kuuleta, aache utani na watanzania? Ama kuna asilimia yake hapo maana vichwa hivi si vya kisasa kabisa..
Mbona mnapenda kulaumu sana, umeambiwa mali ya mkandarasi kwa.ajili ya kujaribu miundo mbinu, wewe unatokwa povu. Mbona nyumbani kwako una tv ya kichogo sie tumekaa kimya hatukwambii.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Afrika ilishakuwa dampo la vyuma chakavu haiwezekani serikali inayojinasibu ni safi iingie mkataba wa hovyo kiasi hiki kwa kutuletea vyuma chakavu kama hilo dubwashwa hapo juu..

Ukute limepigwa service ndio wakalisafirisha kuja huku kwetu, inasikitisha kwa kweli..
Una pesa za kununua mpya wewe
 
Kama n kichwa Cha mkandaras bas akimaliza kutest aondoke nacho

Na kwann atest na kichwa Cha kizaman wakat vinavyokuja n vya kisasa



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Unaweza kuwa Una point ya msingi hapa. Kwa vile kichwa cha majaribio cha mkandarasi kina air resistance kubwa maana kipo bapa. Hivyo haiwezi kuwa na speed kubwa. Na vile vya TRC vitakavyo kuja vina sura 'mchongoko' hivyo vina air resistance ndogo, hivyo speed yake ni kubwa. Kama majaribio umefanya vichwa vyenye dynamics tofauti na vile vitakavyo tumika kwenye kazi halisi. Hapo watajuaje yatakayo vichwa vya TRC vitavyo kuja?..... Wajuzi wa haya mambo tufahamishe. Tafadhali.
 
Back
Top Bottom