GE2025 Musiba: Kama kuna mtu yeyote nilimkosea, naomba anisamehe. Ule ulikuwa ni ujana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Amefanya jambo jema. Kuomba msamaha ni tunu. Asamehewe asisamehewe yeye keshamaliza.
 
Ametutukana sana huyu muhuni kwa hiyo anaomba msamaha wa nini aendelee na yale maigizo yake alimchafua sana Membe sijui kesi yao imeishia wapi..
 
kesi tena mkuu? membe si alisharip na saivi ndoivo jamaa kashachutama kuomba msamaha au
 
Nampongeza kafanya uungwana haswaaa
 
Wakuu,

Inaonekana kama Musiba baada ya kukatwa na CCM akili zimeanza kumrudi.

Leo akiwa anaongea na waandishi wa habari ameomba radhi watu wote ambao aliwakosea kipindi hicho na akaongeza kuwa kipindi kile alikuwa kijana tu.

Nadhani msamaha huu unawahusu sana wakina Fatma Karume na wengineo ambao walichafuliwa sana na huyu baba kipindi cha mwendazake

Mwanaharakati huru Cyprian Musiba amechutama na kuwaomba radhi wote aliowakosea na kuwafanyia mabaya siku za nyuma akidai kuwa yote aliyoyafanya ulikuwa ni ujana huku akiwasisitiza waafrika kutokuwa na visasi na kuacha kuweka vitu moyoni.

"Watu wananisema eti wewe ulikuwa unawaombea wenzako mabaya. Inawezekana nilikuwa kijana sana. Sasa hivi nimekuwa mtu mzima - akili zinakua, unabadilika, unakuwa na busara. Unajua kadri unavyozidi kukua, ndivyo unavyopata hekima, busara na utu. Wakati mwingine ujana sio mchezo.

"Kwahiyo waafrika tuna tatizo la visasi na sijui tutaacha lini, visasi sio vizuri, visasi pia vinasababisha nchi haiendi mbele inarudi nyuma tu, sasa msipende kuweka kitu moyoni, ni kitu kibaya sana kwasababu nchi hii ni yetu sote, mtu akikukosea kasirika hapo hapo mmalizane tu msameheane maisha yaendelee," amesema Cyprian Musiba.

HAHAHAA SEMA HIVI NIMEKOSA SANA NIMEKOSA SANA WATANZANIA MNISAMEHE TUKUFIKIRIE ELSE NA WEWE HUKUTAKIWA HATA KUENDELEA KUWEPO
 
Wakuu,

Inaonekana kama Musiba baada ya kukatwa na CCM akili zimeanza kumrudi.

Leo akiwa anaongea na waandishi wa habari ameomba radhi watu wote ambao aliwakosea kipindi hicho na akaongeza kuwa kipindi kile alikuwa kijana tu.

Nadhani msamaha huu unawahusu sana wakina Fatma Karume na wengineo ambao walichafuliwa sana na huyu baba kipindi cha mwendazake

Mwanaharakati huru Cyprian Musiba amechutama na kuwaomba radhi wote aliowakosea na kuwafanyia mabaya siku za nyuma akidai kuwa yote aliyoyafanya ulikuwa ni ujana huku akiwasisitiza waafrika kutokuwa na visasi na kuacha kuweka vitu moyoni.

"Watu wananisema eti wewe ulikuwa unawaombea wenzako mabaya. Inawezekana nilikuwa kijana sana. Sasa hivi nimekuwa mtu mzima - akili zinakua, unabadilika, unakuwa na busara. Unajua kadri unavyozidi kukua, ndivyo unavyopata hekima, busara na utu. Wakati mwingine ujana sio mchezo.

"Kwahiyo waafrika tuna tatizo la visasi na sijui tutaacha lini, visasi sio vizuri, visasi pia vinasababisha nchi haiendi mbele inarudi nyuma tu, sasa msipende kuweka kitu moyoni, ni kitu kibaya sana kwasababu nchi hii ni yetu sote, mtu akikukosea kasirika hapo hapo mmalizane tu msameheane maisha yaendelee," amesema Cyprian Musiba.

Mwendazake akirudi na huo ujana unarudi tena!
 
Anataka mabaya yake aliyowafanyia wenzake yote, yafutwe na neno NISAMEHE 😂, atulie tu zamu yake ifike , unafanya ubaya kwa kutegemea kuomba msamaha.
 
Ngoja vigogo wachukue form muanze kuimba "tuliipenda wenyewe".
 
Hatufaki msamaha wake aendelee na ujana wake tu
 
Huyu Musiba kila siku anaomba msamaha
Ukiona hivyo ujue kuna mawili:
1. Kalazimishwa na Israel mtoa roho bila yeye kujijua au
2. Kayaona yaliyotokea baada ya kifo cha ndugai.

Katika historia za wengi waliotangulia, toba ikisha fanyika tu, huwa hawadumu zaidi ya miaka 2 na utasikia ule wimbo wa palapanda inalia…

Asamehewe tu ili atulie na muumba wake…
 
Huyu sio wakusamehe alitakiwa apigwe viboko hadharani.

Zama za magu kaumiza watu sana na vigazeti vyake uchwara . Alifikilia atatesa milele magu kafa yatima wanateseka huku na mtaomba sana msamaha.

Nasema hivi mtaondoka mmoja mmoja ndugai amesepa bado wewe na konda boy
Acha roho mbaya, wewe usiposamehewa mabaya yako utabaki salama?
 
Back
Top Bottom