GE2025 Musiba: Kama kuna mtu yeyote nilimkosea, naomba anisamehe. Ule ulikuwa ni ujana

GE2025 Musiba: Kama kuna mtu yeyote nilimkosea, naomba anisamehe. Ule ulikuwa ni ujana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wakuu,

Inaonekana kama Musiba baada ya kukatwa na CCM akili zimeanza kumrudi.

Leo akiwa anaongea na waandishi wa habari ameomba radhi watu wote ambao aliwakosea kipindi hicho na akaongeza kuwa kipindi kile alikuwa kijana tu.

Nadhani msamaha huu unawahusu sana wakina Fatma Karume na wengineo ambao walichafuliwa sana na huyu baba kipindi cha mwendazake

 
Nilishwaambia hata mkifanya dhambi fanyeni kwa akili,Musiba kajitakia maisha magumu kwa upuuzi wake!!.
 
Aisee! pole Bw. Musiba kwa yaliyokukuta hadi umeamua uombe msamaha
 
Wakuu,

Inaonekana kama Musiba baada ya kukatwa na CCM akili zimeanza kumrudi.

Leo akiwa anaongea na waandishi wa habari ameomba radhi watu wote ambao aliwakosea kipindi hicho na akaongeza kuwa kipindi kile alikuwa kijana tu.

Nadhani msamaha huu unawahusu sana wakina Fatma Karume na wengineo ambao walichafuliwa sana na huyu baba kipindi cha mwendazake

Sponsa amevuta, akili zinarudi sasa
 
Mimi nimemsamehe.

Nitajitahidi kusahau pia 😊
Pole mkuu
Ila kama tukienda kwa style hii unawaumiza watu makusudi kwa kutegemea msamaha
Hatutafika mbali.Musiba kawaumiza sana watu ,sema sasa ameona alikua anatumika vibaya na amepigwa chini (halipwi tena)na waliokua wanamtumia

Msamaha wa hivyo akitokea mtu akamlipa tena atarudi kazini
 
Akawaombe msamaha kwa kugalagala Zitto Kabwe na Sufiani Juma kwa kuwatangaza kuwa wanaishi kama Mme na mke, na walikuwa wanamgombania na kiongozi mwenzake.
 
Yule MUSIBA aliyetamba kipindi cha utawala wa mwendazake Magufuli.

Ametoka mafichoni tangu kifo cha Magufuli ameamua kujishusha mbele ya watanzania na kuomba msamaha.

Watanzania kazi kwenu kumsamehe ndugu MUSIBA.
 
Huyu sio wakusamehe alitakiwa apigwe viboko hadharani.

Zama za magu kaumiza watu sana na vigazeti vyake uchwara . Alifikilia atatesa milele magu kafa yatima wanateseka huku na mtaomba sana msamaha.

Nasema hivi mtaondoka mmoja mmoja ndugai amesepa bado wewe na konda boy
 
Back
Top Bottom