Musoma: CCM yaizawadia Shule kengele ya Kisasa


Inafikirisha sana mkuu...! Acha tu.
 
CCM inaumwa
 
Hivi vitu vingine sio hata vya kutangaza kwa kweli.
Kwahiyo Mheshimwa mbunge kaenda kuokota rim kalipeleka shule kama zawadi ya kengele.

Hatari sana kiongozi sidhani kama mtoto wake anampelekea zawadi za aina hiyo mkuu.
 
Duh yani anashindwa kutoa fungu ifungwe electric bell/alarm system hapo shuleni badala yake anapeleka rim ya lorry
Ya Tsh 22,000/= kwenye chuma chakavu maana hiyo bei hilo rim wanakupimia kwa Kg.

Ila kupitia picha kama hizi tunaweza kujua namna Tanzania kulivyokuwa bado na jamii duni kiasi kupewa rim scraper kwa ajili ya kengele ya shule kunaweza kuonekana kama sherehe.
 
Nilikwenda Ujerumani hivi karibuni, nikatembelea kanisa fulani. Mwenyeji wangu alinitembeza humo kanisani, kitu alichojivunia sana ni kengele iliyo tundikwa kwenye mnara wa hiyo kanisa - ina uzito wa Tani moja na inapigwa na watu watatu wanao vuta kamba ndani ya chumba mahasusi kwa kazi hiyo kila jumapili asubuhi au wakati wa siku muhimu kwa kanisa hilo.
Hivyo, hiyo rimu ya Gari inafaa sana kwa ajili ya kengele ya shule - ina mlio mkali unao fika mbali. Hivyo itatoa na faida kubwa kwa wakazi wa karibu na shule, kusaidia kushiriki katika kuwawajibisha walimu na wanafunzi (mlio wa kengele ya rimu). Pongezi kwa walio liona hilo na kutoa msaada huo. Na wewe kama unayo rimu chakavu hapo nyumbani, usiipeleke kuiuuza kwa vyuma chakavu - donate it to any school. Haimalizi LUKU!
 
Ulienda Ujerumani na ulichojifunza ni kuwa rimu ya gari ni kengele nzuri!
Poor you.
 
CCM inaumwa
[emoji1][emoji1][emoji1]
Sipendi siasa ila hawa jamaa wagonjwa
Kuna mwingine bungeni anasema upandaji wa miti umesababisha Ngedere na Tumbili wajae na kula mazao yao halafu eti hawana uzazi wa mpango

Hebu imagine anazungumzia Ngedere na Tumbili wawe na uzazi wa mpango
Halafu anasubiriwa na watoto kwa shangwe huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…