Ila we jamaa umekaza fuvu kwa mambo usiyoyajua ilhali huna ulijualo. Eti wanaoamini uwepo wa ushirikina ni mazwazwa, zwazwa ni wewe unayepinga uwepo wa mambo ambayo yapo.
Kwa taarifa yako viongozi wote wa dini wanaamini hayo mambo yapo maana vitabu vyote vitakatifu vimetaja uchawi na vinaukemea. Papa Francis, Maaskofu,Mapadre,Wachungaji,Maimamu,Masheikh,n.k wengi ni wasomi wa viwango vikubwa kukuzidi yet wanajua uchawi upo.Kuamini uwepo wa uchawi/ushirikina haimaanishi kwamba unaunga mkono mambo hayo.
Mhe.Andrew Chenge amasoma Havard University ambako hujawahi kutia mguu na pengine ukafa bila kukanyaga pale, ila muulize kuhusu hayo mambo atakwambia. Mhe.Mizengo Pinda alishawahi kuhojiwa kuhusu kama kweli hayo mambo yapo kule kwao Sumbawanga kama wengi wanavyodai, akakiri yapo kwa sana tu. Sasa we mwenzetu
Bufa sijui ulizaliwa na kukulia Amsterdam? Ila sisi tuliozaliwa na kukulia hapa Africa tunajua hayo mambo yapo kwa wingi tu.