Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Mvua ya kawaida hii wakuu, mbona huwa mnapenda kukuza mambo...!!!

Kuna maeneo hapa Tanzania huwa zinapiga mvua za upepo hadi unasikia paa zinapiga kelele kama vile bati zinataka kuchomoka...
Si unajua tena watu wa huo mkoa ni mayai mayai sana
 
Naskia upepo umesababisha kifo cha mtoto kwa kuangukiwa na mti
 
Mvua kubwa Jana Makonda alitamba kutoa matingatinga 20
Mungu kajibu kwapigo la kungoa madaraka Kwa Gwajima
Tuone hayo matingatinga sasa
 
Jirani yangu nyumba yake msingi unaning'inia saa yoyote inashuka na kahamia mwaka jana hata mwakq hajamaliza mkewe leo tulikuwa tunampepea hajiwezi
 
Mvua ni kubwa sana wanaokaa sehem za mabondeni sijui wakoje mwenyezmungu awanusuru nimepita toangoma nyuma ya kituo cha mafuta oilcom sasa hv mitaa ya kule kama bwawa maji yamejaa sana sijui. Wakaz wake wakoje
Afadhali umesema kesho nilikuwa na Safari ya huko siendi
 
Taarifa nyingi hapa ni za uongo, ina maana kila mtu anaandika taarifa ya eneo alipo na simu haiwezi kupiga picha ahahahaaa..!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…