Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Yani ndio nimeamka muda huu nikidhani ni alfajiri kumbe ni saa mbili kasoro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee mimi pia ni mhanga wa hili jambo zamani kidogo niliwahi shuhudia rafiki yetu akifariki kwa radi... tangu hapo mimi na radi hatuendani kabisa
 
Mikoani Radi zinapiga za nguvu sana kupita huko mjini.
Naiogopa sana Radi maana kukuondoa ni dk.0 tu
Huko zinawasaidia EarthWire nadhani.
Huku vijijini ni chache sana
Wakati nipo High school Bukoba Kagera kuna mwanafunzi wa shule ya msingi inaitwa Kabugalo alikuwa darasa la nne alikufa kwa kupigwa na radi.

Alitoka darasani na mwamvuli kwenda kumpelekea mwalimu aliyepo kwenye gari ili waje naye darasani asinyeshewe na mvua.

Mvua ilikuwa inapiga vibaya mno na radi za kule Bukoba zinapiga vibaya mno na kumulika mithili ya vimulimuli...

Aiseeeee!! Yule Mwanafunzi anatoka tu nje, iliwaka radi akapigwa na radi akaanguka chini.

Baada ya mvua kuisha kwenda kumcheki amekaushwa na kuwa mweusi tii. Hakuruhusiwa mtu yeyote kumgusa hadi ambulance ilivyokuja kumchukua kumpeleka mochwari.

Niliishi kwa wasiwasi sana hadi nilipomaliza masomo maana mvua za Bukoba ni 24/7 na radi zake zinapiga hadi unaona ule mstari mweupe unatua chini..
 
Sijawahi kuogopa radi za Dar mpaka nilipofika mkoa fedenge ilipiga nikajikuta uvunguni aroo nilijua bati limetoka lote. Ile ilikua sio radi bwana vigagula wanatoa na dedication humohumo wanaongezea mlio
Radi za Rukwa, Tabora, Kigoma, mtwara,Kagera na Ruvuma ni balaa..

Mimi wakati nipo Bukoba nilikuwa naogopa sana, Yani radi ikipiga ule mstari mweupe wa radi unaokuwa zig-zag [emoji298] unauona mbele yako na mwanga ule wa kimulimuli mweupe unaingia hadi ndani utadhani taa imewashwa ...

Baada ya hapo inapiga ngurumo moja unahisi ngoma ya sikio inataka kupasuka..[emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…