Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Wananzengo,
usiku saa 9 nimejikuta navamiwa na wanangu chumbani, wanaogopa radi kabambe zinazopiga sambaba na mvua hii kubwa yenye upepo wa kuhamisha milima.

Soon kunakucha.

Tujuzane endapo kuna maafa maeneo yenu. Lengo ni kupashana taarifa. Tupia picha .

Nawalinda wanangu hapa wasipigwe na ngurumo ya radi.😀😀😀..... yaani kha! Wanaogopa sana lile libombastic sound baada ya radi kumulika.

Tanesco aibu sana kwa haya mnayotufanyia.

============

Madhara mengi ni kutokana na mipango miji mibovu, na sioni suluhu kwasababu wahusika walio shindwa wwnajiandaa kwa uchaguzi mkuu hawataki wahudhi wote walio jenga ktk njia za maji na mabonde.
 
Madhara mengi ni kutokana na mipango miji mibovu, na sioni suluhu kwasababu wahusika walio shindwa wwnajiandaa kwa uchaguzi mkuu hawataki wahudhi wote walio jenga ktk njia za maji na mabonde.
Pale ferry barabara inayokatiza soko la samaki. Mvua hata ya dk 10 inajaza maji pale na maji hayadogei ilihali bahari ni nukta sufuri tu hapo
 
Wanaosema Mungu hayupo angalieni hatari ya hiyo Radi, nani anaweza kuizuia usimtoe Roho?

Siku za usoni ikinyesha mvua kama hiyo ya Leo na Radi, mala mbili ya hiyo kwa siku tatu mfululizo huko mjini kwenu, nadhani kila mmoja wenu ataanza kumlilia Mungu wake aiweke nchi katika hali ya tulivu wa kawaida.
Kusema Mungu hayupo ni kushiba majivuno tu.
Sasa kuwepo Kwa mvua inayoharibu nyumba za binadamu na kuua watu ndio uwepo wa mungu huo?

Kwanini uwepo wa mungu usijidhihirisshe Kwa kuizuia mvua isiue watoto wake
 
Tanesco wanakuambia mabwawa hayana maji [emoji1]
Lakini Bashe anasema mashamba ya miwa yamejaa maji ndio maana hakuna sukari ya kutosha[emoji205]
Acheni ujuaji kwani ninyi hamjui kwamba hii nchi mvua zinachagua pa kunyesha, huwa zinanyesha kwenye mashamba na makazi ya watu tu, zikifika kwenye vyanzo vya maji huwa zinakata kona zinabadili muelekeo
 
Mvua nzuri sana kwa wakulima ila isizidi kipimo
 
Eneo lote chini ya Bagamoyo Road halikutakiwa kuwa makazi ya watu. Ni kinamasi cha kuishi mamba, samaki na kambare.
 
Hata kama alizima na rimort radi ikishuka hiyo mitaa hata zile LNB zina kufa hapo hapo huwenda nyumba mbili tatu za hako la mtaa haziko salama kama vitu vilikua kwenye umeme kuzima sio inshu wachana na radi [emoji120][emoji120][emoji871][emoji846]
Kweli,sie tulizimaga lkn mtaa mzima ulifikiwa, sie Tv,visimbuzi/2,radio,pasi,viliujgua ni vizuri kuchomoa cable tu,
 
Ambao hawajashuhudia yaliyotokea usiku wa leo ni haki yao kusema wanachojisikia.

Kuna miti imeanguka barabarani ambapo ukiangalia umetokea wapi hupati jibu! Eneo la karibu hakuna mti, hatari!
Kuna mingine inakuwa imesafirishwa na maji na kudumpiwa mahali
 
Wanaume wa dar bwana![emoji28][emoji28][emoji28]
Hahahahaha wanaongopa mvua,

Mwaka juzi Nilikuwa kwa anko g/mboto,mvua ilikuwa inanyesha ya kawaida usiku mie nililala zangu,,,,,,aunt akaja kuniamsha eti nisilale mvua inanyeshaa na radi,hahahahaha,

Huku kwetu radi zina piga mchana na jua linawaka na si ajabu,
 
Mvua ya kawaida hii wakuu, mbona huwa mnapenda kukuza mambo...!!!

Kuna maeneo hapa Tanzania huwa zinapiga mvua za upepo hadi unasikia paa zinapiga kelele kama vile bati zinataka kuchomoka...
Wa dar utaweza basi,,,Kama huku kwetu inanyesha Kama dozi Tena ya maana.
 
Back
Top Bottom