mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Pamoja na ukweli kwamba siamini katika adhimisho la ibada na mfu ama wafu, lakini natambua ya kwamba JPM alikuwa "benevolent" dikteta mwenye uthubutu wa kulinda rasilimali za nchi.Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea pumziko la milele mbinguni Hayati John Pombe Joseph Magufuli.
Misa hii takatifu itafanyika Jumapili ya Machi 20 katika viwanja vya madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Kawekamo kuanzia saa nne kamili asubuhi.
Aidha, Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande anatukumbusha kumuenzi Hayati Magufuli kwa kuwa Wazalendo wa kweli, kudumisha amani, undugu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Hayati Magufuli apumzike kwa amani mbinguni.
View attachment 2147385
His missing gap is real clear now. Some of his actions were very awful indeed, but when it comes to his devotedly patriotism, it real sounds something real needed to be acknowledged.