Mwaka wa 9, Sijawahi kumuona mtu mwingine akitumia JamiiForums

Mwaka wa 9, Sijawahi kumuona mtu mwingine akitumia JamiiForums

Watu wote wanaonifahamu wanajua kabisa huwa nikiingia mtandaoni basi ni Jamiiforums na twitter basi
 
Ni mwaka wa ku 9 tangu Nilipoanza kuutumia huu mtandao lakini sijawahi kukutana na mdau wa mtandao huu.

Leo nimejaribu kuwauliza colleagues Kama wanaufahamu, wote walikiri kuufahamu lakini wakasema hawautumii.

Nikajiuliza iwapo ni kweli au wanaficha privacy zao. Je, uliwahi kumuona mtu live akitumia JamiiForums?
Ukija pale kitengo makumbusho watu wengi tunautumia huu mtandao bila kificho! Sijui huko kwenu
 
Nimeshakutana na wengi kiukweli huu mtandao una vigogo wengi acha tuendelee kutumia fake id
 
Kuna mzee flani ni wa makamo niliwahi mfuma anatumia jf kila nikikutana nae yupo jf ni msomi ila mlevi, sijawahi bahatisha kujuwa id yake na wala sikuwah mgusia kama naujua huu mtandao , maana nikimuuliza direct awezi nitajia id yake

Pia niliwah kutana na mtu ktk gari yupo online jf
 
Watu huwa tu wananishangaa niko busy na simu..wakichungulia wanaona Jamii Forum..wengi wanajua JF ni watoaji habari tu..

Mkuu ukijulikana upo JF wanajua wewe ndo msanuaji wa mambo yao.

Huu mtandao unajulikana kwa kuweka mambo yaliyojificha wazi.

Hivyo ofisini ukijulikana tu [emoji2][emoji2] majanga. Ndiyo maana hata watumiaji hawataki wajulikane.
 
Nilikuwa kwenye bus ya JMC ya dar singida, kufika Dodoma ilipanda pisi moja kali sana ikawa inaperuzi jf nikachungulia nikaona ID yake dooh sikuamini aisee!!
Hadi sasa tupo friends but hajui kama nimemjua yupo hapa jf ila naamini kwa comment hii akiiona atanifahamu .

Ila mjue tu JF kuna pis kali aisee si mchezo?

😂 usijali mama ndo mimi D wako!!!
Inaonyesha pisi Kali sio mropokaji humu🤣🤣🤣🤣ungekuta na wale machizi wa humu nadhani ungeandika negative,,ila umeandika positively....
 
Inaonyesha pisi Kali sio mropokaji humu🤣🤣🤣🤣ungekuta na wale machizi wa humu nadhani ungeandika negative,,ila umeandika positively....
Ndo siwezi tu kumtaja kamwe lakini huwezi amini ni ID maarufu sana hapa.

Elewa ninavosema humu kuna pis kali mnatakiwa kunielewa jamani ni vitu haswa kama utabahatika kuviona.

Huyu sio mropokaji ni mtu smart sana.
 
Ni mwaka wa ku 9 tangu Nilipoanza kuutumia huu mtandao lakini sijawahi kukutana na mdau wa mtandao huu.

Leo nimejaribu kuwauliza colleagues Kama wanaufahamu, wote walikiri kuufahamu lakini wakasema hawautumii.

Nikajiuliza iwapo ni kweli au wanaficha privacy zao. Je, uliwahi kumuona mtu live akitumia JamiiForums?
JF ni sawa na zimwi likujualo ambalo wewe haulijui!

Ni ngumu sana kukutana na member, hata tu ile kumuona mtu anacomment chochote kakamatia key board, ni vigumu mno.

Waweza kuishi maisha yako yote hadi kung'ata shuka bila ya kuona hilo tukio.

MwanaJf ukitaka kumuona live, lazima uwe na biashara unauza, tena biashara iliyoenda shule, ama connection za madili ya kazi ama utafutaji mwingine, ndiyo utaiona sura ya mwana Jf ikijidhihirisha kwako.

Mimi Jf ilishaniunganisha na members kibao na kuonana live kwa sababu za kibiashara.
 
Daah mimi Jf imenifanya nimekutana na watu wengi sana na tunatambuana kwa majina ya JF hata ukimpa jina la nyumbani anaendelea kukuita Isanga Family unajua kabisa hii zamani JF...Big up sana kwa Melo
 
😆 😆 😆 😆 😆
Kuna rfk yangu huwa busy sana na JF yani hata mkiwa pamoja utasikia nasoma mambo ya JF..kwenye group anatupia labda link za uzi fulan ambao na mm nimeusoma..ila ukimuuliza yy ni member anakataa anasema anasoma tuu ila kwa jinsi kichwa chake kilivyo najua yupo humu huwa najaribu kuunganisha dots na watu humu bado sijampata..ila kama anataka kufanana na member fulani humu..mwandiko/hulka ya uchangamfu....japo na mimi sijawahi mwambia nipo JF
 
Back
Top Bottom