Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Hii stori ni ya kufikirika na haina hata chembe ya uhalisia. Nahisi ina lengo tu la kuwajaza watu upepo ili watokwe na mapovu!

Naomba niwe tu wa mwisho kuiamini. Maana ina maswali mengi kuliko majibu.
Magufuli alipoongeza makato bodi ya mkopo kutoka 8%-15% nilijikuta na take home ya laki 1.82 hapo nikiwa na mke na mtoto mmoja. Kila nikitembea nilikuwa nailaani CCM
 
Data base ya watumishi wa umma ni moja.
Unapotoroka kazi, kupata kazi labda ughushi kila kitu, jambo ambalo ni gumu.

Ukiona mtumishi anatoroka, elewa katamani ujasiria mali ama kazi za mashirika binafsi.
Huyu akitaka kurudi hata leo kazini anarudi tu bila shida,tena rahisi sana
 
Nimesikitishwa kupata habari kuhusu mwalimu anayefundisha shule ya sekondari Dunda iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani kukimbia kazi ya ualimu baada ya kulipwa 34000 kwa mwezi.

Hii inatokana na adhabu ya kushushwa cheo na kulipwa nusu mshahara na Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kosa la utoro kazini.

Mwalimu huyo wa kike aliishi maisha magumu sana hapo hapo shuleni ,alikosa mpaka hela ya kula ilimlazimu auze miwa na maembe aliyoyaokota hapo shuleni ili apate pesa ya kula.

Uzalendo ukamshinda baada ya mazingira magumu ya kazi aliamua kuondoka kazini bila ya taarifa kwa muajiri.

Habari nilizozipata mwalimu huyo yupo Mlandizi akifanya kazi ya kuhudumia wateja bar.

TSC mnapotoa adhabu ya kupunguza mishahara kwa walimu mzingatie iwapo kama mtuhumiwa ana mikopo benki, isitoshe adhabu ya kupunguza mshahara ni ya kikatili maana mshahara wenyewe hautoshi hapo hapo mnaupunguza.

Habari nilizozipata huyu mwalimu alikuwa na madeni benki na taasisi za fedha hapo Bagamoyo.

Kutokana na mazingira magumu ya kazi mwalimu huyo kaamua kutelekeza kazi yake.
Qnet m9 BITCOIN na ponzi schemes zingine zimehusika hadi huyo mwalimu kufika hapo. Ponzi schemes zimekula vichwa vya waalimu ambao hawana majukumu na wenye vichwa vya panzi. Nimejionea mengi. Waathirika wakubwa wa ponzi schemes ni waalimu
 
Sheria ya kukatwa mshahara haina mantiki na kama wakiona mtu aendani nao wa mwache tu
 
System imuondoe afu imlipe nusu mshahara? Ni sisitimu ipi hiyo mkuu? K
Ninachosema ni hivi?

Sasa hivi na zamani ni tofauti.

Zamani mtu aliweza kuacha kazi na kutafuta kazi nyingine bila tatizo bila kujulikana.

Lakini kwa mfumo wa sasa, kuanzia kuajiriwa hadi kuacha ama kufutwa kwa utoro alama wanabaki nayo.

Hivyo popote utakapotaka kuajiriwa kazi za serikali waki retrive wanakuona pamoja na sababu zilizokuondoa kazini.

Lakini mashirika ya binafsi wala haina shida.
 
Sio kwa kumpondea mwalimu,lakini katika taaluma ngumu kufukuzwa au kupewa adhabu serikalini ni taaluma ya ualimu,nadhani kuja wakafikia hatua hiyo,huyo mwalimu ni mtoro sugu tena aliyekubuhu, Kuna Wakati nilifanya kazi na mwalimu x wa kike,kule Lindi ,yeye alikuwa akinywa pombe na kulewa alikuwa ana anguka chini anapoteza fahamu ,watu wanaanza kumbaka kwa zamu,kwa huruma ya mkurugenzi,walimuhamisha toka vijijini na kumleta mjini ili awe chini ya usimamizi lakini hakubadilika,alienywa Mara kadhaa lakini hakusikia,mwisho wa siku alifukuzwa kazi.

Yaani ukiona mwalimu anapewa adhabu za namna hii ujue kweli huyu mwalimu ni tatizo katika utumishi.
 
Hii stori ni ya kufikirika na haina hata chembe ya uhalisia. Nahisi ina lengo tu la kuwajaza watu upepo ili watokwe na mapovu!

Naomba niwe tu wa mwisho kuiamini. Maana ina maswali mengi kuliko majibu.

inawezekana kabisa kama mwalimu akikopa anapata 10m alaf anataka hapo anunue kiwanja na ajenge ,, kapata kiwanja kwa 5-6m tuseme kwa kuwa yuko bagamoyo kwenye 10m anabakiwa na 4m anajenga nyumba inaishia level ya lenta inabidi aende faidika ili amalizie nyumba ,,,,
Nmb makato labda laki 3 kwa mwezi faidika yao laki na ishirini ,,,,,take home haiwezi kuvuka laki ,,,huo utoro unachangiwa na kukosa nauli labda ,,,,,,ila kiukweli walimu wanamaisha magumu sana [emoji26]
 
Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Wala kazi ya ualimu haina laana yoyote, tatizo ni huyo mwl aliekopa hovyo kwenye taasisi za kifedha, na bado akawa mtoro kazini Sasa ulitaka walee uzembe?
 
kazi ya kwanza baada ya kuacha kazi ni ubamedi aloooh ok ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe
 
Let’s say alikuwa na netpay ya 468,000 na jumla ya makato yalikuwa 200,000.
Ukiigawa nusu na bank wakakata chao unabaki na 34,000 ikutunze kwa siku 30 zijazo. Mmmmae naacha kazi.

Mwajiriwa na madeni ni pete na kidole, pengine ukute huo utoro kazini chanzo ni kujiongeza kutafuta kipato cha ziada baada ya maisha kuwa magumu pale unapokopa na kuwekeza kwenye ujenzi na pesa ikakata kwenye renta.
 
Walimu waboreshewe maslahi kama wabunge.

Nilisikia report ya katibu mkuu wa tume ya Utumishi wa Walimu kwamba asilimia 50 ya Walimu wamefukuzwa kazi kwa utoro baada ya kuishi ktk mazingira magumu.

Mbona hatusikii idadi hiyo kuacha kazi Benki Kuu, TRA, Uhamiaji, Bandari, Jeshi?
Sijawahi sikia watoro kama walimu!!! Sijui kwa nini walimu tu!?
 
Afukuzwe tu..hao sio wajinga kumpunguzia mshahara..
huyo hana maadili ya ualimu..
 
Ninachosema ni hivi?

Sasa hivi na zamani ni tofauti.

Zamani mtu aliweza kuacha kazi na kutafuta kazi nyingine bila tatizo bila kujulikana.

Lakini kwa mfumo wa sasa, kuanzia kuajiriwa hadi kuacha ama kufutwa kwa utoro alama wanabaki nayo.

Hivyo popote utakapotaka kuajiriwa kazi za serikali waki retrive wanakuona pamoja na sababu zilizokuondoa kazini.

Lakini mashirika ya binafsi wala haina shida.
Jibu kwanza swali langu mkuu ni system gani inaweza kukulipa nusu mshahara afu useme imekuondoa?
 
Ninachosema ni hivi?

Sasa hivi na zamani ni tofauti.

Zamani mtu aliweza kuacha kazi na kutafuta kazi nyingine bila tatizo bila kujulikana.

Lakini kwa mfumo wa sasa, kuanzia kuajiriwa hadi kuacha ama kufutwa kwa utoro alama wanabaki nayo.

Hivyo popote utakapotaka kuajiriwa kazi za serikali waki retrive wanakuona pamoja na sababu zilizokuondoa kazini.

Lakini mashirika ya binafsi wala haina shida.
Huyo hachaacha kazi na wala hajafukuzwa kazi na ndyo mana anapata mshahara,tatizo hapo ni utoro
 
Back
Top Bottom