MwanaFA azomewa na wananchi baada ya kuanza kusifia Awamu ya 6 kwenye Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva

Ile midada imelewa tayali ndio kaambiwa ivyo na Babu Tale!
ikabidi hawapotezee tuโœ๏ธ

Ikijengwa iyo Arena iyo iyo midada itajaaa umo ๐Ÿค ๐Ÿค 
na wao ni wapumbavu zaidi,unakaaje na walevi usiku.
 
Ninachopendea Walevi na wanywaji wakiwa kwenye burudani na starehe hawataki siasa wala mahubiri ya dini ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜€
Nakuhakikishia wangesikia anasema Tundu Lissu ameachiwa au Polepole amepatikana wangeshangilia...

Watanzania wamechoka...

Na walichokichoka wanakijua vizuri sana.
 
Mwana F.A ana hela gani ya kujenga Arena mpaka atambie watu!??!Achaneni na Siasa za kizamani nyie CCM..

Hao wanaozomea wanajua ujenzi wa Arena ni matokeo ya kodi zao..

Siyo Rais wala Waziri,wanajenga kwa hela yao ya mfukoni.
 
Hahaha
 
Mpuuzeni tu Mwana F.A,kwake Siasa ni -Zali La Mentali-kimaisha,hukuwahi kuwa na fikra wala msukumo binafsi wa kuwa Mwanasiasa.

Kati ya Wanasiasa wa Tanzania wanaotokea ghetto anayepwaya ni Mwana,F.A.

Ni zao la Siasa za kishamba za Marehemu Magufuli,kwamba CCM nayo uwe na Wabunge Wasanii eti waiongezee mvuto.
Ndiyo akapigiwa chapuo na Madam UMMY MWALIMU,aliyekuwa rafiki sana wa JPM.

Sugu,Baba Levo,Profesa J,Jokate..wao hata kazi zao za sanaa zilikuwa zina aksi utetezi wa haki na Siasa kwao bado inabaki kuwa ni moja ya platform ya kuendeleza harakati za kutetea wanajamii..na hata hawategemei msukumo wa Serikali pekee.

-Mifano michache:
1-Baba Levo anailalamikia Serikali juu ya Wanafunzi wa Elimu ya juu kukoswa Mikopo huku anaingia mfukoni mwake kuwapatia hela wakaendelee na Masomo kwa kadri uwezo wake unavyomuruhusu na si kuwakopesha.

2-Jokate-ametumia vilivyo exposure yake ya Usanii kwa kutafuta wafadhili wa nje wakajenga shule akiwa D.C.Kisarawe.
3-Sugu-akiwa mbunge aliwahi kusambaza tablets kwenye baadhi ya Shule akiwa Mbunge,kwa kuwatumia rafiki zake wa Marekani waliotokana na Usanii wake.

HAYA:-
Mwana,F.A:-

Amekuwa ni msambazaji wa pesa za Mama Samia kwenye Misiba ya Wasanii na kwa Wasanii wanao umwa!!

Na akifika utambulisho ni huu

-:..Mama amenituma pokea/anakupa pole...!!!

Hana Dira wala jipya,nje ya kusifu Serikali na Viongozi.
 
Mwana F.A ana hela gani ya kujenga Arena mpaka atambie watu!??!Achaneni na Siasa za kizamani nyie CCM..

Hao wanaozomea wanajua ujenzi wa Arena ni matokeo ya kodi zao..

Siyo Rais wala Waziri,wanajenga kwa hela yao ya mfukoni.
Ewe nyumbu uliyechanganyikiwa Hadi hujisikii unapoongea, hajasema atajenga yeye Wala hakulitaja jina la Samia maskini ya Mungu; aliitaja serikali tu. Au serikali Haina pesa ewe nyumbu?!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ