kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Ndio hayo uliyoyasoma baaasi!Unataka kusema nini hapo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio hayo uliyoyasoma baaasi!Unataka kusema nini hapo?
ndiyo maana walikuwa wanatumia nguvu nyingi watu wasajili laini ili waweze kuwathibiti vizuri
Kwani hayo maajabu yameanza leo? Naamini iko siku tutaongea lugha moja.Mambo ya ajabu sana! Aibu aibu ...
Namna ya ukamataji. Watu sita na bunduki! Wakati huyo ni mtu ambaye hata angetumiwa ujumbe angefika kituoni. Hatuna polisi bali zama hizi ni hao wasiojulikana.Kwa nini kila anayekamatwa munaripoti ni watu wasiojulikana? Kuweni na subira maana naona muda kidogo tunaambiwa yuko polisi. Kwani polisi hawatakiwi kumkamata mtu? Imekuwa ni kukimbizana kuripoti sijui tunamuwahi nani!
Aseee,wewe ndo mange nini,kwa hii essay ukiwa hauna hata mahusiano nae ntashangaa kweli na uzee wangu huuNimeshangaa sana kuona wakisema kuwa Mange Kimambi sijui amehongwa Pesa ndefu mara sijui ametishiwa kuwa akiendelea na harakati zake basi watavujisha Siri za tukio zima alilofanyiwa Marehemu Baba yake. Hivi kweli kuna Mamlaka ya Kipumbavu hapa duniani ambayo tayari imechafuliwa kwa 99.9% na Mtu ( hapa namaanisha Mange Kimambi ) tena Mkuu wake wa nchi ndiyo akiongoza Kuchafuliwa huku na kule na hadi Siri zake zingine za mambo yake Binafsi Kuanikwa na karibia zimejulikana na Watanzania wengi japo siyo wote halafu eti leo tena hao hao ( Mamlaka ) wapoteze Pesa zao kumpa Mange Kimambi ili atulie. Hivi kama ni kumpa Pesa Logically tu walitakiwa wampe kabla hajaharibu au baada ya kuwa ameshaharibu hivi? Hivi Mtu ambaye ameshakupiga hadi Kukujeruhi kabisa nusura ya hata kutaka Kukuua unaweza tena hapo hapo ukawaomba Ndugu zako ili wajipange na wampe Pesa ili asiendelee Kukushambulia?
Na hii Hoja eti Mange Kimambi sijui ametishiwa kuwa akiendelea na harakati zake basi Video za Kitendo alichofanyiwa Baba yake itawekwa wazi ( Hadharani ) ni ya Kipumbavu sijapata Kuona au Kusikia. Hivi kwa jinsi Mange Kimambi alivyo ( Mtu asiyejali, aliyedata na asiyeogopa huku akiwa ameshajitoa kwa kila Kitu ) leo hii hata akiona Picha ya Baba yake ( namaanisha Video ) imewekwa mnadhani ataguswa nayo kwa lolote au labda ndiyo ataumia au itamuuma?
Acheni Kuficha Ukweli kwa Kuhamisha Goli kuwa Mange Kimambi amehongwa au ametishwa kuhusu Video ya Baba yake bali ukweli ni ule ule ambao tena aliuweka mapema tu kuwa hatojihusisha tena na harakati za Kuwatetea na Kuwapigania Watu ( akimaanisha Watanzania ) ambao ni Waoga na Wanafiki huku akionekana Kuchukizwa na Kitendo cha Watanzania ( hasa wa Kupitia kile Chama cha Upinzani alicho na Mahaba nacho ) kwamba Walimsaliti na alimtupia mno Lawama zake nyingi Mwenyekiti wa hicho Chama na baadhi ya Makada ( Makamanda ) wake Waandamizi.
Binti wa Watu mmemsaliti kwa Unafiki na Uwoga wenu katika ile Kampeni yake Kabambe ya UKUTA leo hii mnaanza Kumlaumu kuwa sijui amehongwa na ametishiwa. Na bahati nzuri ni kwamba Watu ambao leo hii wanamzushia hivi ( hasa hapa JF ) ni wale wale ambao miongoni mwao ile Siku ya UKUTA walijibanza Majumbani mwao huku wakiwa wanaserebuka tu Vitandani na Wake / Waume zao ila hapa nyuma ya Keyboard ndiyo wanajifanya Wababe, Watetezi na Wanaharakati. Unafiki mtupu! Na kama mnasema kuwa amehongwa na ametishiwa mbona bado anaendelea tu Kutoa taarifa Nyeti kadhaa za Kuhusu Mamlaka za nchi hii japo kwa sasa hatoi nyingi?
Jibu sahihi na ambalo yawezekana kwa Uvivu wenu wa Kufikiri ( baadhi yenu ) ni kwamba siyo kwamba huyu Binti amehongwa au ametishiwa bali ni ukweli usiopingika kuwa wale Watu wake waliokuwa wakimpa Classified Information za hasa Executive ama wameshajulikana na wamedhibitiwa vilivyo kwa Maadili ya Kazi zao ( na najua ninaposema Wamedhibitiwa wale Wabobezi wa Masuala ya Kimafia mmeshanielewa vyema tu hapa ) kutokana na Operation Kabambe iliyoendeshwa kwa Msaada wa Wataalam wa IT na Mitandao ambapo wengi wao waliweza Kudakwa na Kujulikana upesi huko hivyo Mange Kimambi hapati tena Taarifa zile Nyeti Kiurahisi kama ilivyokuwa hapo awali na hata hizi anazozipata sasa ni nyepesi na pengine ndiyo maana wengi wenu Siku hizi mnaona kama vile amehongwa au ametishiwa.
Na mnaohoji leo Mange Kimambi kuachana na Harakati zake zile mlizozizoea na kuonekana sasa akijiusisha na Uvaaji wa Vichupi mnashangaza mno. Hivi hamjui kuwa ni zile zile Pesa zenu alizokuwa akiwaombeni na nyingine kwa Kujipendekeza Kwenu Kwake Kumtumia ndiyo hizo hizo Mwenzenu amejiongeza na sasa kaamua Kujikita nazo katika Kujiajiri katika Sekta hiyo nzima aliyopo sasa ya Fashion and Design? Wakati nyie ( Wapumbavu baadhi ) mkimcheka kuwa anaonekana kuonyesha Vichupi vyake Mitandaoni ( hasa katika Kurasa zake za Mitandaoni ) tambueni ya kuwa Mwenzenu hapo hapo pia ndiyo anatengeneza Pesa ambazo wengi wenu hapa Mtandaoni hata mkija Kustaafu Kwenu huko Makazini mlipo bado Viinua Mgongo vyenu havitoweza Kufikia Pesa ambayo Mange Kimambi anatengeza huko sasa. Tena kwa Unafiki wenu hadi Mkamsaliti ile Siku ya UKUTA ni kama vile Watanzania wengi ( Wanafiki ) mmempotezea mno muda wake na huenda asingekuwa anajihusisha na Harakati zake za Kuwapiganieni Kiuwanaharakati na akajikita tu Kupigania Maisha yake na ya Wanae huko Marekani aishipo basi huenda leo hii angekuwa ni Mmoja wa Watanzania Matajiri sana waishio Ughaibuni ( Diaspora )
Haya endeleeni na Uwongo na Uzushi wenu Kumhusu Mange Kimambi ila nilitaka tu nilitolee hili Ufafanuzi kwani linakera mno.
Vodacom wamevunja sheria za mawasiliano za kitaifa na kimataifa.Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera anadaiwa kuvamiwa na 'watu wasiojulikana' nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam baada ya watu kadhaa wakiwa na magari kuvamia na kuzingira nyumba na kuzuia watu kuingia.
Namba ya gari lililomchukua imetajwa ni T746DFS.
View attachment 1166543
Erick Kabendera, a Tanzanian journalist, has been abducted from his home in Mbweni, Dar es Salaam. He told one of his colleagues of a high presence of security vehicle and unknown people around his house shortly before he disappeared to never be reached by phone this evening.
UPDATES:
Baada ya watu hao kuzingira nyumba huku wakionekana kuwa na nia ovu, yeye na familia walifunga milango. Wananchi akiwemo M/kiti wa mtaa walipofika na kuhoji wao ni nani walisema wao ni Polisi (hawakuwa na sare wala gari la polisi). Sasa inadaiwa wamekwenda naye kituo cha Polisi Oysterbay.
UPDATES: 2100HRS
Jeshi la Polisi inadaiwa linaendelea kumhoji Kabendera kuhusu mambo ambayo hayajawekwa wazi na wala hawajasema anahojiwa kituo gani. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kinondoni.
Kabendera alichukuliwa na watu 6 waliokuwa na silaha na inadaiwa simu yake ilikuwa blocked tangu Jumamosi huku Mtandao wa Vodacom wakimwambia wamefanya hivyo kwa maagizo ya TCRA. Wakimtaka ajisalimishe Voda Shop
View attachment 1166671
Wananchi waliokusanyika nyumbani kwa Erick walijitahidi kuwazuia watu hao na kuwataka wajitambulishe. Pamoja na jitihada za wananchi kutaka kupiga picha, simu zao zimechukuliwa kwa kudaiwa kuwa hawaruhusiwi kupiga picha.
praise team inanufaika na mumo, wana ccm wengi pia wananufaika, hata nduguze huyu jamaa waliopo ccm bado tu wanaimba iyena iyena, hii nchi Mungu mwenywe aje kutukomboa..lakini huku bado kina Pengo, mufti, Malasusa, nk wanaendelea kuwapigia makofi hawa watu!
wewe ni mgeni insta na siasa hujui.Naona huyu Ngurumo anataka kuchukua nafasi ya yule bint aliwatikisa jamaa zetu kupitia instagram hadi akasababisha makamanda kuandamana ila ameufyata baada ya kupigwa mkwara ya kwamba akiendelea na fujo bhas jamaa zetu wangeachia picha za tukio lililomfanya baba yake ajiue pia kwa ustaarabu wa jamaa zetu wakampa US dollars kadhaa kama kiinua mgongo cha kumstaafisha Instagram....sasa hivi page hata kutembelea inabidi uwe peke yako maana ni vichupi tuu ndivyo anavyo post na mala chache huwaponda akina Paulo ambao ana personal conflicts nao.....
Uovu ni uovu na kamwe sijawahi kuutetea! Jema nalisema na ovu nalikemea na hii ni tofauti na nyie wafia vyama ambao mnataka yasemwe mabaya tu ndio uonekane kamanda!Kwani hayo maajabu yameanza leo? Naamini iko siku tutaongea lugha moja.
Mbona aliendaga kuchukua form ya ubunge kama sio mwanasiasawewe ni mgeni insta na siasa hujui.
yule ni model, mrembo na si mwanasiasa,
alipiga siasa baada ya jiwe kumzingua kwenye mambo yake binafsi.
alosema mwenyewe baada ya watu kugomea maandamano anaaacha siasa, kaacha eti kahongwa, akirudi utasema hela imeisha, pumbav sana wewe
Kumbe kakamatwa mbona mlitudanganya kuwa ametekwa?? Yaani siku hizi JF limekuwa jukwaa za uongo uongo!!Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera anadaiwa kuvamiwa na 'watu wasiojulikana' nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam baada ya watu kadhaa wakiwa na magari kuvamia na kuzingira nyumba na kuzuia watu kuingia.
Namba ya gari lililomchukua imetajwa ni T746DFS.
View attachment 1166543
Erick Kabendera, a Tanzanian journalist, has been abducted from his home in Mbweni, Dar es Salaam. He told one of his colleagues of a high presence of security vehicle and unknown people around his house shortly before he disappeared to never be reached by phone this evening.
UPDATES:
Baada ya watu hao kuzingira nyumba huku wakionekana kuwa na nia ovu, yeye na familia walifunga milango. Wananchi akiwemo M/kiti wa mtaa walipofika na kuhoji wao ni nani walisema wao ni Polisi (hawakuwa na sare wala gari la polisi). Sasa inadaiwa wamekwenda naye kituo cha Polisi Oysterbay.
UPDATES: 2100HRS
Jeshi la Polisi inadaiwa linaendelea kumhoji Kabendera kuhusu mambo ambayo hayajawekwa wazi na wala hawajasema anahojiwa kituo gani. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kinondoni.
Kabendera alichukuliwa na watu 6 waliokuwa na silaha na inadaiwa simu yake ilikuwa blocked tangu Jumamosi huku Mtandao wa Vodacom wakimwambia wamefanya hivyo kwa maagizo ya TCRA. Wakimtaka ajisalimishe Voda Shop
View attachment 1166671
Wananchi waliokusanyika nyumbani kwa Erick walijitahidi kuwazuia watu hao na kuwataka wajitambulishe. Pamoja na jitihada za wananchi kutaka kupiga picha, simu zao zimechukuliwa kwa kudaiwa kuwa hawaruhusiwi kupiga picha.
05:20am - July 30, 2019
Chanzo kinabainisha Erick alikamatwa na Maafisa wa Polisi waliotokea Kituo cha Polisi Mbweni lakini njiani inadaiwa magari yalibadilishwa na bado hakuna taarifa rasmi za kituo gani anahojiwa.
😂😂😂Mbona aliendaga kuchukua form ya ubunge kama sio mwanasiasa
ni maagizo toka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.
Kabendera ni mwandishi wa habari za uchunguzi kwenye magazeti mbalimbali pamoja na gazeti la Africa Confidential linalochapishwa nchini Uingereza.
Waandishi wa habari ni watu hatari sana wakitumia kalamu zao vibaya. Hata hii habari ya Kabendera, kuna media wametangaza eti ametekwa, amekamatwa,amechukuliwa na wengine eti amepotea. Waandishi wengi wanaandika huku wenyewe tayari wameshachagua upande. Sio kwa weledi bali kwa mihemko.Wacha tuwaulize hao wasiyo julikana watujibu