Tanzania hatuongelei kuhusu mental health. Huyu jamaa ametaabika sana, Mpaka amefikia hatua ya kutoa uhai wake.
Sad story ni hamna mtu anaejua alikua anapitia nini haswa.
Nakubaliana nawe kwa 50% sababu siwezijua huenda kauwawa na wasiojulikana kwa upande wa pili.
Hiyo hali iliwahi kunikuta nilipopatwa na ajali nikiishi home zaidi ya miaka mi3 bila kazi nikiwa na njemba 2 ilihali nikitegemewa na Ndugu wengine zaidi ya 5.
Tarehe 01 nilikuwaga namalizia kutoa mshahara benki na baada ya hapo ni kushinda tu home nikijiuguza hadi tarehe 25/26 ya mwezi mwingine.
Usiku mmoja saa 7 kifua kilinibana sana wakat huo wale Kaka zangu walienda kwenye harusi walichelewa kurudi home, sina vocha wala hata mia mfukoni, niliamsha Majirani kwa sauti ndogo maana maumivu yalizidi sana na hawakunisikia kabisa.
Nilienda umbali wa km 2 nikamwomba Jamaa mmoja nauli tu alinipa 2,000/= na kufika Hospitalini Kairuki saa 04:00 PM, bahati nzuri nilikuwa na bima ya afya.
Vipimo vilionesha nina "Metro Valve prolapsing" yani kuna baadhi ya misuli ya kwenye moyo ina linkage tokana na msongo wa mawazo hivyo damu, hewa na maji vinaunganishwa kwa nguvu kubwa sana ya moyo kuliko inavyotakiwa kikawaida.
Dr alinishauri dawa bora ni kuchukulia hali niliyokuwa napitia ni kawaida sana na nisikae pekeyangu, pia ni heri nikatafuta vitu vinavyonifanyaga niwe na furaha zaidi la sivyo nitazua balaa zaidi.
Nilifanikiwa kurudi ktk hali ya kawaida kiafya baada ya wiki 2, na ndipo nikajua wakati mwingine excessive stress ni tiketi ya kifo 1 kwa 1 maana nilikuwa siwezi kuhema, kuinama wala kusimama kwa jinsi nilivyokuwa na maumivu zaidi kifuani.