Mwanamke anachokifuata kwenye mahusiano ni pesa (uchumi) na si mapenzi

Mwanamke anachokifuata kwenye mahusiano ni pesa (uchumi) na si mapenzi

Nimeshashuhudia watu kadhaa wenye hela zao wanavyosumbuliwa na mapenzi.... Love is all about affection

Mwanamke huwezi ukamdiscribe kirahisi hivyo ... wenye kujua mind set ya mwanamke hatujawahi kutetereka na tumepata wanawake wenye mapenzi ya kweli katika hali zetu hizi hizi za kipato cha kati

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
Mna miaka 20 na ngapi kwenye ndoa?
 
Amekutendea nini; na mna miaka mingapi kwenye ndoa yenu?
Miaka 13 tunaishi pamoja .Sikuwa na hela yeye akawa anapata vihela ila yupo tu.Nikapata vihela akakosa kazi yupo tu.Wote tuna vihela namtunzia na vihela vyake yupo tu.Ndugu zake na rafiki wananionaga miyeyusho ila yeye yupo tu.Hakuna mtu anaweza kuishi na mimi,kesho tu ataondoka ila yeye yupo tu.
 
Kafanye Research tena....; Kuna watu wali-abscond hata ufalme (na kuacha Pesa) na kukimbia na mpenzi wao kwenda kuishi maisha ya kimasikini wote wawili...

Binadamu huwa anathamini kitu ambacho hana (kwahio ukiwa na pesa (kwa wengi) kwako pesa sio kigezo tena )
 
Mwanamke anachokifuata kwenye mahusiano ni pesa (uchumi) na si mapenzi.

kama uamini, poteza kipato uje utoe ushuhuda hapa jukwaani.

Kama huna kipato au ramani zako hazisomeki, atakuvumilia kwa muda tu, baadaye anakutelekeza.

Kwa kifupi, hakuna mwanaume anayependwa bila kuwa na kipato.
Na mwanamke mwnye kipato je?? Hana haja ya mapenzi si ndiyo??
 
Miaka 13 tunaishi pamoja .Sikuwa na hela yeye akawa anapata vihela ila yupo tu.Nikapata vihela akakosa kazi yupo tu.Wote tuna vihela namtunzia na vihela vyake yupo tu.Ndugu zake na rafiki wananionaga miyeyusho ila yeye yupo tu.Hakuna mtu anaweza kuishi na mimi,kesho tu ataondoka ila yeye yupo tu.
Ilo ni jambo la heri, ingawa dunia pia ina mitihani; ebu fumba macho na ujiulize, pale umeishiwa pesa na ukawa huna mwelekeo, na ikatokea umelazwa hospitali kwa zaidi ya miezi minne, yaani wewe uwe ni wakusiaidiwa kila kitu kama mtoto mdogo; je atakuwepo?​
 
Hayo namuachia Mungu tu mkuu.
 
Back
Top Bottom