Mwanamke anachokifuata kwenye mahusiano ni pesa (uchumi) na si mapenzi

Mna miaka 20 na ngapi kwenye ndoa?
 
Amekutendea nini; na mna miaka mingapi kwenye ndoa yenu?
Miaka 13 tunaishi pamoja .Sikuwa na hela yeye akawa anapata vihela ila yupo tu.Nikapata vihela akakosa kazi yupo tu.Wote tuna vihela namtunzia na vihela vyake yupo tu.Ndugu zake na rafiki wananionaga miyeyusho ila yeye yupo tu.Hakuna mtu anaweza kuishi na mimi,kesho tu ataondoka ila yeye yupo tu.
 
Kafanye Research tena....; Kuna watu wali-abscond hata ufalme (na kuacha Pesa) na kukimbia na mpenzi wao kwenda kuishi maisha ya kimasikini wote wawili...

Binadamu huwa anathamini kitu ambacho hana (kwahio ukiwa na pesa (kwa wengi) kwako pesa sio kigezo tena )
 
Na mwanamke mwnye kipato je?? Hana haja ya mapenzi si ndiyo??
 
Ilo ni jambo la heri, ingawa dunia pia ina mitihani; ebu fumba macho na ujiulize, pale umeishiwa pesa na ukawa huna mwelekeo, na ikatokea umelazwa hospitali kwa zaidi ya miezi minne, yaani wewe uwe ni wakusiaidiwa kila kitu kama mtoto mdogo; je atakuwepo?​
 
Hayo namuachia Mungu tu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…