Mwanamke hata umtoe Out, mnunulie zawadi za bei, Umfanyie shopping lakini kama anakudai Buku yake Bado hamtaelewana

Mwanamke hata umtoe Out, mnunulie zawadi za bei, Umfanyie shopping lakini kama anakudai Buku yake Bado hamtaelewana

Wakuu,

Hawa viumbe mungu kawaumba tofauti,
Hata umfanyie shopping na kumfurahisha kwa gharama yyte ile lakini kama hukumlipa hela anayokudai hata kama ilikua ni elf 1. Hamuelewani

We mpe mnunulie simu, mnunulie gari lakini kama anakudai Bado hujasema.
Chamsingi anza kulipa deni lake ndo mengine yaendelee
Unawezaje kumnunulia gari lakini unashindwa kumlipa 1000? Hiyo kwa kweli ni dharau.

Amandla...
 
Sawa, ila mkumbuke kutoomba kwa mnaemdai dai, kama hamtaki kuhesabu anavyowagaramia baada ya kumkopesha.
Tusiwaombe kivipi 🙄🙄Mungu mwenyewe alijua Adam hataweza kutumia pekeake, akamletea Eva aje ale. Hela zenu tunakula ila hela zetu hela zetu.
 
Wakuu,

Hawa viumbe mungu kawaumba tofauti,
Hata umfanyie shopping na kumfurahisha kwa gharama yyte ile lakini kama hukumlipa hela anayokudai hata kama ilikua ni elf 1. Hamuelewani

We mpe mnunulie simu, mnunulie gari lakini kama anakudai Bado hujasema.
Chamsingi anza kulipa deni lake ndo mengine yaendelee
Kuna mmoja toka 2006 anasema anadai 120,000/- kila nikimsabahi anasema nakudai nikasema Mimi sikumbuki,mwingine Yuko Dubai Leo hii namtafita whatapp anasema nakudai nilikulipia malipo ya masomo bei gani anasema 100,000/- nikamwambia sikumbuki,these creature
 
Wanawake wa ajabu sana, jamaa alimfungulia mpenzi wake genge kubwa na likachangamka sana. Cha ajabu mnunuzi wa mboga ndiye anaemfaidi huyo mwanamke kuliko huyo mpenzi wake.
 
Dawa ya deni kulipa acha janjajanja kutoana dinner, kununuliana zawadi sio makubaliano yetu..!!
 
Wakuu,

Hawa viumbe mungu kawaumba tofauti,
Hata umfanyie shopping na kumfurahisha kwa gharama yyte ile lakini kama hukumlipa hela anayokudai hata kama ilikua ni elf 1. Hamuelewani

We mpe mnunulie simu, mnunulie gari lakini kama anakudai Bado hujasema.
Chamsingi anza kulipa deni lake ndo mengine yaendelee

Mzee baba unaanzaje kudaiwa na "demu"?
 
I say, uko sahihi 150% Kuna dada niliomba aniazime hela yake nikiwa nimekwama, laki moja. Ikanisaidia sana. Sasa kuna siku nae akaja kunililia shida, kabla sijamrudishia ile laki. Nikampa laki tatu, ambayo haikuwa mkopo, nikijua narudisha hisani. Kuna siku akanifuata ananiuliza lini nitamrudishia laki yake niliyomkopa?😳

Nilimwomba samahani nikamrudishia. Siku alipokuja kuomba tena msaada ndio nikampasukia, kwamba hana akili sawasawa, nikamkumbusha juu ya laki yake na laki zangu tatu. Nikasema iwe mwisho kuniomba msaada, na sintaomba tena msaada kwake.
Wakati unampa laki tatu ungemwambia laki moja ya deni, hizo mbili umempa msaada.
 
Umenikumbusha nikadai deni langu la 180,000 japo juzi nilipewa 1m lakini ilikuwa ya issue nyingine haihusiani na deni langu.
Wababa sisi tunapenda mtimize ahadi zenu hata kama utanipa hiyo hela kisha tuitumie kununua mabati ama chakula ila utaje ni lile deni langu.😀😀
 
Dawa ya deni kulipa acha janjajanja kutoana dinner, kununuliana zawadi sio makubaliano yetu..!!
Hapana, ni namna pia ya kuangalia kama mna akili kichwani, kumbuka naweza kukutoa nje kwa gharama mara tano ya deni lako, fedha ambayo ningelipa deni lako na chenji ibaki, na sio kwamba unanilazimisha nikutoe. Kwa hiyo unatakiwa kuufikirisha ubongo wako
 
Back
Top Bottom