Mwanamke, Ukipata fursa usiiache kisa mwanaume uliyenaye

Mwanamke, Ukipata fursa usiiache kisa mwanaume uliyenaye

Hapo sasa kwa wanandoa wenye kufanya kazi sehemu tofauti ni mtihani.

uhalisia kabisa mwanamke hatawki kufanya kazi nje ya mji anaofanya mumewe.
 
Pole sana shangazi Nyendo
Wanaume tulio wengi ni wema
sana,hasa kama mwanamke
ni mtii...hata kazi atafanya tu.
Pole kwa maumivu uliyonayo.
Mungu akusaidie😂😂😂
 
Wanawake tutafute hela jamani, yaani tuzisake hadi zishangae.

NB: Naunga mkono hoja🤝
 
Mwanamke yapaswa utambue furaha yako haipo katika kutafuta Hela .Maana hizo Hela hata utafute vipi uwe unalipwa kiasi kikubwa vipi Kuna uwazi utauhisi kama haupo kwenye familia yako na mume ambaye unaweza kumtegemea.

Wanawake wengi mnataka kwenda against nature hiyo Hela mnayoitafuta wakina Wema Sepetu na Lady Jay Dee wanazo Sana lakini hawana furaha.

Hakuna furaha ambayo mwanamke anaweza akapata ambayo ni zaidi ya kuwalea watoto wake mpaka wanakua pamoja na mume wake hayo mambo mengine ni kupoteza muda tu.
 
Huyu yupo kipindi cha mwisho kuingia menaopause kama siyo mwisho wa mwaka huu basi mwakani hatoboi so anakuja kuwatia ujinga wale wanaochipukia.

Unfortunately,mfano wa kipofu kumuongoza kipofu mwenzake unaa-aply sana kwa hii jinsia.
Asante, jifunze kujibu hoja acha lugha zisizofaa
 
Emu subiri
Unasema mwanaume akifanikiwa anakuona wew sio levels yake? Sio kweli
Hizo ni pigo zenu wanawake
Mwanaume akikupotezea basi kuna sababu ya MAANA! Ambayo kimsingi umeianzisha mwenyewe
Wanawake ni watu pekee wanaweza kufanya mambo bila ya sababu.
 
Nimeshangaa ukahaba unahalalishwa mdogo mdogo...
Kama mwanamke kila mwanaume anamuona fursa sasa ana tofautiana nini na kahaba??
Unakutana na mmoja yeye weekend anasema hapiki anataka kula restaurants tu.
 
Infact, mwanamke kuwa na mafanikio ni jambo jema sana lakini imekuwa tatizo kubwa sana kwenye taasisi ya ndoa..
 
Huu utaratibu wa wasimbe kuwashauri wanawake kuhusu ndoa haujakaa poa kabisa[emoji19]
Jifunze kujibu hoja, kwa sababu hujui unayemjibu nani? Kwanza usimbe sio ugonjwa.

Mwanamke kutumia fursa anayopata sio kosa kwa sababu hajui kesho yake wala hana bima ya mahusiano.

Kwank walioachana ni wangapi?

Acheni kuwashawishi wawe tegemezi ili muwafanye mtakavyo.
 
Emu subiri
Unasema mwanaume akifanikiwa anakuona wew sio levels yake? Sio kweli
Hizo ni pigo zenu wanawake
Mwanaume akikupotezea basi kuna sababu ya MAANA! Ambayo kimsingi umeianzisha mwenyewe
Wanawake ni watu pekee wanaweza kufanya mambo bila ya sababu.
Acha hizo, kwani ni wanaume wangapi wanaofanikiwa na kutelekeza familia zao?

Tatizo jinsia ya kiume hujipa utakatifu hata kama haiko nao.

Hupenda kuona jinsia ke ndio tatizo lakini kimsingi kila upande una shida na inapaswa kila mmoja ajue kuwa ana jema na baya bila kujali jinsia aliopo na kumwachia mwenzake

Familia zipo nyingi ambazo baba kafanikiwa na kabadilika kama ilivyo kwa mama kubadilika baada ya mafanikio.

Na hatuwezi kiyakataa mafanikio kwa kuogopa mabadiliko ila yatupasa kuchukua tahadhali ya kuwa na uwezo wa kujiongoza binafsi pale tufanikiwapo.

Angalia mtaani uone machozi ya mama na watoto ndani ya familia ambazo baba kafanikiwa, so sio kwamba wanawake pekee ndio hubadilika ni both sides.

Ni uchoyo na ubifsi kutaka mmoja abaki nyuma eti kisa upo kumuhudumia, vipi ukipata na majanga kama kudondoka kiuchumia, maradhi nk nani atamuhudumia? Maana hatujui ya kwasho na nani atatangulia kufa au atapatwa na shida ipi.

Lakini mama akibaki au akiwa na uwezo wa kiuchumi ni rahisi watoto na yeye kujiongoza au hata kukusaidia wewe pia.
 
Asante, jifunze kujibu hoja acha lugha zisizofaa
Huna hoja ndiyo maana nimeandika hayo uliyoyasoma hapo juu.

Unadhani mama zetu waliotuzaa wangekuwa na mindset kama unayohamasisha wenzako hapa leo tungekuwa smart kama tulivyo?tafuta humu uzi umeanzishwa leo kuhusu watoto wa William Malecela waliolelewa na mama yao independent woman walivyomtukana matusi ya nguoni.
 
Huna hoja ndiyo maana nimeandika hayo uliyoyasoma hapo juu.

Unadhani mama zetu waliotuzaa wangekuwa na mindset kama unayohamasisha wenzako hapa leo tungekuwa smart kama tulivyo?tafuta humu uzi umeanzishwa leo kuhusu watoto wa William Malecela waliolelewa na mama yao independent woman walivyomtukana matusi ya nguoni.
Dunia ya mama zetu si dunia ya leo, dunia ya mama zetu ndoa ilikuwa ya jamii, mke aliweza kuachwa na mume na akaamua kwenda kukaa ukweni ili alee watoto na kupata chakula.

Leo mwanamke akiachwa anaweza kubaki kwa wazazi au ndugu wa mume?

Au baba akifariki ndugu walio wengi wa leo wana moyo wa kulea watoto wa ndugu yao kama wa kwao?

Malezi ya watoto si ya mama pekee, bali ni baba na mama, haijalishi mnaishi wote wala mmeachana, na sijasema watu waachike bali nimesema wasiache fursa bali waziendee fursa kama ni mahusiano yataendelea ndani ya fursa au akirudi yataendelea.

Mwanamke mwenye matumaini ya kesho anakuwa na akili iliyotulia hata kulea hao watoto kwa kuwa hapati mzigo wa kuwaza watoto watakula nini,

Hao watoto walioharibika lazima kuna shimo la uharibufu lilifunguliwa aidha na wazazi wote au mmoja kuna sehemu hawakutimiza wajibu wao au watoto wamekataa njia waliooneshwa kupita na wazazi wao.
 
Back
Top Bottom