Mwananchi anyimwa fursa ya kuuliza swali kwa kuanza swali la kusema waliosaini sio Watanganyika

Hivi kuna rais/mawaziri walio laumiwa kusaini mkataba kwa sehemu walio tokea?.

Au Mnyamwezi kulaumu Mchaga kwa kusaini mkataba mbovu.
Wanyamwezi na wachaga wote ni Watanganyika, ni tofauti na kesi ya bandari yetu ambayo raia wa nchi nyingine wamesaini mikataba kwa niaba ya raia wa nchi nyingine! Mbaya zaidi mkataba huo unaonekana kuwa wa kinyonyaji na kinachoshtua zaidi upande wanaotoka waliosaini (Zenji) hauhusiki kwenye utekelezaji wa mkataba huo!
 
Ishu ninachosema sio mjadala kuhusu hizo sema ni kwamba zinasaidia na ufanisi unaonekana basi ni kheri.

Point yangu je kama Dp world akileta ufanisi na nchi inanufaika kuna tatizo jamani?

TICTS alikosa ufanisi basi akaondolewa hilo sio tatizo kufuatilia performance ya mkataba kama atashindwa kuleta ufanisi anatimuliwa hata kwa mutual agreement.
 
Sasa ulitaka mtu MWEHU kama huyo asiyejua kuwa hatuna nchi inayoitwa TANGANYIKA aendelee kupewa nafasi ili achangie nini!?.Tanganyika ilishazikwa mwaka 1964 huko.

Mamburura mko wengi sana hapa Tz.
Hivi kuna Tanzania bila Tanganyika??
 
Sasa machafuko halafu ndio mtawale au? Tanzania hakuna machafuko na haitatokea. Hivi uchaguzi halali ni mpaka wapinzania washinde tu? Hao viongozi wengine ni kina nani, maana tuwekane sawa ni kina nani hao wa ridhaa? Uchaguzi sio katika uchaguzi mkuu tu hata serikali za mitaa ndio CCM wamekamata. Shida ya wapinzani wakisoma huko tweeter wanaamini basi nchi wanabeba lakini mitaani watu wana mashaka sana na wapinzani uwezo wao. Wapinzani wengi ni wale walioshindwa CCM wanatafuta njia nyepesi ya kupita. Tanzania hakuna wapinzani ni watu wanatafuta kick za kupita nazo basi.
 
Huyu Msigwa kanishangaza Sana yaani anamlazimisha mwananchi kusema uongo?

Kumbukeni Msigwa ni Mwandishi wa habari, just an ordinary reporter aliyetunukiwa kusogezwa karibu na mfalme.

Sio expert wala nini, anajiongeza tu! Then we should not expect wonders from ordinary brain kama hii yake!

Tumsamehe bure tu wala hajui kama issue ya bandari ina magnitude gani! Anahisi ni kama bwawa la kijiji kule mtambaswala!
 
Kipindi bimkubwa anaenda dubai expo wakajua anaenda ........
Acha niishie hapo
 
Chukueni hatua nyie subirini maji yamwagike ndipo muanze kuyazoa wakati huo haiwezekani.
 

Kwamba huko kwenye chaguzi za serikali za mitaa CCM huwa ndio wanashinda kihalali, lakini kwenye mkuu ndio wanapora? Au unadhani zile chaguzi huwa zinafanyika sisi tukiwa nje ya nchi? Kama wapinzani wanaamini wanachokiona huko tweeter, si ndio ilikuwa mahali pa ccm kufanya chaguzi za halali ili ukweli uwe wazi? Sasa unasema inakubalika, sijui ina sera nzuri, wananchi hawana imani na upinzani, lakini kwenye uchaguzi ndio unaoongoza kwa rafu!
 
Sasa ulitaka mtu MWEHU kama huyo asiyejua kuwa hatuna nchi inayoitwa TANGANYIKA aendelee kupewa nafasi ili achangie nini!?.Tanganyika ilishazikwa mwaka 1964 huko.

Mamburura mko wengi sana hapa Tz.
Nakubaliana na wewe, Tanganyika haipo. Je, Zanzibar ipo?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Sasa ww Kwa akili Yako huo ni uungwana tuache ushabiki wa kijinga huyo mnayesema c mtanganyika ndio anajenga vituo vya afya,shule,barabara,uhuru wa vyombo vya habari tuache ujinga wa kubaguana
Anajenga kwa pesa yake?
 

Cha muhimu na ambacho ata wewe unakubali kimoyo moyo ni muda wa mkataba uwepo ukomo yaani kama DP world wanafanya vizuri wanaongezewa muda ata kama itaenda hadi kiama sawa tu. Ila wakizingua basi mkataba ukiisha ndo basi serikali inaachana nao. Hiyo mutual agreement inaweza kua ni mwiba kwa nchi mfano wakisema ili tuachane nao inabidi tuwalipe trillion kadhaa nani atakua kapata hasara. Na ujue wananchi ndo wenye kubebeswa hiyo hasara kipindi hicho watia sign na wabuge waliopitisha wao kama watakua bado hai hakuna atakae wachukulia hatua yoyote. Mkuu tukubaliane muda wa mkataba ni muhimu sana kwenye hii inshu ya DP world
 
Unaongea rafu bila ushahidi wowote inakuwa ngumu kukubaliana na wewe, hizi rafu ni dhana tu kwa yoyote anliyeshindwa hata huko USA tunakoamini wako juu sana kwenye chaguzi lakini kuna na issues rafu sijui nchi fulani imedukua haya mambo hayawezi kuisha. Mimi sisemi chaguzi ziko perfect 100% lakini pia sina shaka kuwa CCM wameshinda huku vijijini CCM ushawishi wao ni mkubwa sana hili halina shaka. Kura tunagawana humu mijini tu
 
Acha unafiki, mzanzibari aitwe mzanzibari ila mtanganyika asiitwe mtanganyika. Huu muungano ni ujinga.
Yaani ndani ya ndoa mke sawa kuitwa mke, lakini mume asiìtwe mume maana ni ubaguzi!
 
Acha ujinga hapa Kuna nchi mbili tanganyika na Zanzibar na ndio maana huyo mwanasheria koko kasema Zanzibar kama nchi inasheria zake kwenye bandari zake Sasa iweje waliotoka huko Zanzibar hamtaki watajwe kwamba ni wazanzibar?
Yes it goes both ways.. Kama hawataki nao wabadili
 
Mama anaupiga mwingi
 
Hivi kuna rais/mawaziri walio laumiwa kusaini mkataba kwa sehemu walio tokea?.

Au Mnyamwezi kulaumu Mchaga kwa kusaini mkataba mbovu.
Waliosaini mkataba wanatokea Zanzibar ambayo ina mamlaka kamili,ina Serikali yake,ina Bunge lake na Mahakama zake.Pia ina Bendera yake ya Taifa na ina Wimbo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…