Unaongea rafu bila ushahidi wowote inakuwa ngumu kukubaliana na wewe, hizi rafu ni dhana tu kwa yoyote anliyeshindwa hata huko USA tunakoamini wako juu sana kwenye chaguzi lakini kuna na issues rafu sijui nchi fulani imedukua haya mambo hayawezi kuisha. Mimi sisemi chaguzi ziko perfect 100% lakini pia sina shaka kuwa CCM wameshinda huku vijijini CCM ushawishi wao ni mkubwa sana hili halina shaka. Kura tunagawana humu mijini tu
Kama ni ushahidi wala sio wa kutafuta upo wazi, na mara zote taarifa huwa zinatolewa polisi. Lakini kwakuwa vyombo vya dola ni sehemu ya CCM, taarifa hizo huwa zinapotezewa, ama ww mtoa taarifa unageuziwa kibao. Haya ni mambo ambayo huwa yanafanywa hadharani na vyombo vyetu vya dola, na ushahidi upo.
Utasema kwenda mahakamani, wanaowapa amri polisi za kuumiza wapinzani, ndio haohao wanaoziagiza mahakama namna ya kutoa hukumu. Ushahidi ni huu uchaguzi wa 2020, Makada wengi wa CDM walifungwa bila ushahidi wa kutosha, yaani kubambikiwa kesi, na sasa baada ya maridhiano uchwara, mahakama zimeagizwa kuwaachia, na wanapoachiwa mahakama hukiri kabisa kuwa walifungwa bila ushahidi kutimia. Na hata juzi kada mkongwe wa CCM Rostam Azizi, alisema sio rahisi wawekezaji wa kimataifa kutumia mahakama zetu za ndani kwa migogoro, kwani inawezekana hakimu/jaji akapigiwa simu na kiongozi kisha kutoa hukumu kinyume na ushahidi. Na kwa kukuonyesha nini kinaendelea kwenye mahakama zetu, kuna kesi ya wabunge waliofukuzwa huko CDM, kesi ile ina miaka miwili sasa lakini hakuna hukumu, wakati hapo Kenya kulikuwa na kesi ya matokeo ya urais, hukumu ilishatoka muda mrefu.
Sababu hizo hapo juu pamoja na udhaifu mwingine wa kimifumo, ndio unaofanya ccm hadi leo iwe madarakani, na wala sio kwa ushawishi wake wa kisiasa. Uchaguzi wa mwisho wa CCM kukaa madarakani kihalali ilikuwa ni uchaguzi wa 2005, baada ya hapo ccm ipo na itaendelea kuwepo madarakani kwa mbeleko ya vyombo vya dola, na udhaifu mwingine wa mifumo unaochangiwa na katiba hii outdated. Huu ni ukweli ambao sikulazimishi kuukubali lakini ndio uhalisia.