Mwananchi anyimwa fursa ya kuuliza swali kwa kuanza swali la kusema waliosaini sio Watanganyika

Mwananchi anyimwa fursa ya kuuliza swali kwa kuanza swali la kusema waliosaini sio Watanganyika

Katika mjadala unaendelea Clubhouse mwananchi mmoja ameshindwa kuuliza Siswali baada ya kusema kuwa waliosaini mkataba sio watanganyika ni Wazanzibar.

Moderator wa mjadala, Gerson Msigwa alimtaka mwanachi huyo afute kauli yake ili aulize swali lakini mwananchi huyo alisema huo ndio ukweli hivyo akashindwa kuuliza swali lake kuhusu DPW katika Mjadala wa bandari unaoendelea.
Simple na sisi bara turuhusiwe kusaini mikataba ya Zanzibar
 
Unaongea rafu bila ushahidi wowote inakuwa ngumu kukubaliana na wewe, hizi rafu ni dhana tu kwa yoyote anliyeshindwa hata huko USA tunakoamini wako juu sana kwenye chaguzi lakini kuna na issues rafu sijui nchi fulani imedukua haya mambo hayawezi kuisha. Mimi sisemi chaguzi ziko perfect 100% lakini pia sina shaka kuwa CCM wameshinda huku vijijini CCM ushawishi wao ni mkubwa sana hili halina shaka. Kura tunagawana humu mijini tu

Tufanye rejea ya uchaguzi wa 2015, maana 2020 hakukuwa na uchaguzi. Japo hata hiyo 2015 nayo ilikuwa ni ubadilishaji wa matokeo wazi wazi hasa huko Zanzibar baada ya CCM kushindwa dhahiri.

Matokeo ya urais yalikuwa 8m+ wapinzani wakipata 6m+, data hizi ni rasmi toka tume ya uchaguzi ambayo haiaminiki bado. Unataka kumaanisha hizo kura wapinzani walipata kwa kugawana huku mijini, lakini ccm ilipata za mijini na huko vijijini? Je wabunge na madiwani wapinzani walipata maeneo ya mjini tu? Kama wapinzani wanaweza kupata kura hizo mijini tu, huoni ccm haiwezi kupata 2/3 ya kufanya maamuzi watakavyo bungeni? Na sababu hasa ya wizi wa kura ni kwa kupoteza ushawishi, na kulazimisha kupata idadi ya kufanya maamuzi.

Narudia tena, ccm haina uwezo wa kushinda kwa kuvuka 50% kwenye uchaguzi wowote halali, na sio kushinda tu, pia haitakaa iweze kushinda tena zaidi ya kura hizo. Na sababu hasa ni kizazi kubadilika. Na ifahamike ccm sio chama cha kizazi hiki.

Kitakachofanyika iwapo ccm itaendelea kulazimisha kukaa madarakani bila ridhaa ya wananchi, moja wananchi wanaopiga kura watazidi kupungua, huku ccm ikiendelea kubweteka kwa kufanya makosa kama haya ya bandari, pili wizi mkubwa kama ulivyo kwenye ripoti za CAG, na hatimaye itatolewa madarakani kwa machafuko baada ya wananchi kusema enough is enough. Ukitaka kujua ninachomaanisha, cdm wamejitoa kwenye hizi chaguzi ndogo za marudio, subiri uone idadi ndogo sana na hamasa ya wapiga kura. Na uchaguzi wa marudio ya ubunge wa Mbarali iwapo wapinzani watasusia kushiriki hasa CDM.
 
Akili za ma ccm zinashangaza sana. Yaani Muungano ni wa nchi mbili! Tanganyika na Zanzibar! Halafu baada ya huo muungano, nchi moja ife! Halafu nchi nyingine ibakie!!

Ok. Time will tell. Watanganyika tumeshawashtukia. Na tunakoelekea, tutagawana tu fito. Maana hakuna Mtanganyika aliye na akili timamu kichwani, anaweza kuvumilia huu upuuzi unao endelea nchini.
Pole!
JamiiForums-1883457645.jpg


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
ukishaoma kijana mdogo anajihusisha na mambo ya CCM tambua huyo ni opportunistic na ni mpenda dezo dezo.

Huwezi ukakuta kijana hardworker anayeamini kwenye kufanya kazi kwa maarifa makubwa na bidii ili apate kipato akawa anajishughulisha na mambo ya CCM.

CCM ni mali ya mabwanyeye kwa sasa ambao ndio wanamiliki kila kona ya uchumi kupitia ufadhili kwa CCM iendelee kuwa chama dola.
Imeisha hiyo!
JamiiForums-1625200532.jpg


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Unaongea rafu bila ushahidi wowote inakuwa ngumu kukubaliana na wewe, hizi rafu ni dhana tu kwa yoyote anliyeshindwa hata huko USA tunakoamini wako juu sana kwenye chaguzi lakini kuna na issues rafu sijui nchi fulani imedukua haya mambo hayawezi kuisha. Mimi sisemi chaguzi ziko perfect 100% lakini pia sina shaka kuwa CCM wameshinda huku vijijini CCM ushawishi wao ni mkubwa sana hili halina shaka. Kura tunagawana humu mijini tu
Kama ni ushahidi wala sio wa kutafuta upo wazi, na mara zote taarifa huwa zinatolewa polisi. Lakini kwakuwa vyombo vya dola ni sehemu ya CCM, taarifa hizo huwa zinapotezewa, ama ww mtoa taarifa unageuziwa kibao. Haya ni mambo ambayo huwa yanafanywa hadharani na vyombo vyetu vya dola, na ushahidi upo.

Utasema kwenda mahakamani, wanaowapa amri polisi za kuumiza wapinzani, ndio haohao wanaoziagiza mahakama namna ya kutoa hukumu. Ushahidi ni huu uchaguzi wa 2020, Makada wengi wa CDM walifungwa bila ushahidi wa kutosha, yaani kubambikiwa kesi, na sasa baada ya maridhiano uchwara, mahakama zimeagizwa kuwaachia, na wanapoachiwa mahakama hukiri kabisa kuwa walifungwa bila ushahidi kutimia. Na hata juzi kada mkongwe wa CCM Rostam Azizi, alisema sio rahisi wawekezaji wa kimataifa kutumia mahakama zetu za ndani kwa migogoro, kwani inawezekana hakimu/jaji akapigiwa simu na kiongozi kisha kutoa hukumu kinyume na ushahidi. Na kwa kukuonyesha nini kinaendelea kwenye mahakama zetu, kuna kesi ya wabunge waliofukuzwa huko CDM, kesi ile ina miaka miwili sasa lakini hakuna hukumu, wakati hapo Kenya kulikuwa na kesi ya matokeo ya urais, hukumu ilishatoka muda mrefu.

Sababu hizo hapo juu pamoja na udhaifu mwingine wa kimifumo, ndio unaofanya ccm hadi leo iwe madarakani, na wala sio kwa ushawishi wake wa kisiasa. Uchaguzi wa mwisho wa CCM kukaa madarakani kihalali ilikuwa ni uchaguzi wa 2005, baada ya hapo ccm ipo na itaendelea kuwepo madarakani kwa mbeleko ya vyombo vya dola, na udhaifu mwingine wa mifumo unaochangiwa na katiba hii outdated. Huu ni ukweli ambao sikulazimishi kuukubali lakini ndio uhalisia.
 
..lakini Ticts hakusaini makubaliano / mkataba wowote ulihitaji ridhaa ya bunge.

..pia Ticts alipatikana kwa mchakato wa ushindani na sio kuteuliwa kama ilivyofanyika kwa Dp.

..mkataba wa Ticts ulikuwa na ukomo. Na hawakutufunga kwa vipengele kwamba tukitaka kufanya uwekezaji bandarini, au kukiwa na fursa zozote, lazima tuwape taarifa.

..Nashauri Raisi Ssh aingilie kati suala hili na kufanya MAREKEBISHO kulingana na ushauri uliotolewa na wasomi mbalimbali kama Prof.Shivji, Dr.Nshala, ...
Upo sahihi ila tunaangalia operation ya Ticts ndo hiyo itakuwa ya Dp world .


Ina maana Ticts alisharenew mkataba mara kadhaa kwa wala na pia malalamiko yake ya utendaji mbovu yalikuwa yanapokelewa na kuwasilishwa kwa mamlaka.

Mchakato ni process ndefu na pia katika kurekebisha hilo linawezekana kwa aslimia kubwa kwa sababu wadau washaingia katika kuchunguza mkataba ,bado wapo kweny makubaliano wanaweza kulumbana na kuweka sawa hata mwakani ili mradi uwe sawa .

Kama haiwezekani sio lazima DP world yeyote yule kikubwa ufanisi.

Hapa umeeleza mambo ya msingi lakini anakuja mtu anakuambia eti "wanauza bandari" 😅😅

Ticts kama sio utendaji mbovu angeendelea ni hakika huyu hata aingia akileta magumashi miaka 5 hatoboi.
 
Ndugai aliposema nchi itakuja kupigwa bei, mlimfurusha uspika na Wengine mlienda mbali zaidi na kumpa majina yote mabaya.

Hili lGA ya bandari ni moja kati ya IGAs /MOU nyingi zilizosainiwa pale Dubai na serikali yenu tukufu.

MOU ya 17 ikiwa implimented, itawarudisha utumwani.

Nyie endeleeni tu kupayuka anaupiga mwingi
Ndugai hakufurushwa, kajiuzulu kwa hiari yake kwa mujibu wa barua yake ya kujiuzulu.
 
Wanataka kuvunja muungano na wameona hii ndiyo njia pekee ya Tanganyika kuanzisha mchakato wa kuuvunja mchakato. Wako sahihi. Tuuvunje.
 
Hivi Kuna Mnyamwezi alishawahi kusaini mkataba wa uwekezsji wa serikali ya mapimduzi ya Zanzibar
1) Nyerere alimuondoa rais wa zanzibar kwa sababu ya Jumbe kutaka serikali tatu. Hivi rais wa Tanganyika kwanini amuondoe rais wa nchi ya zanzibar?.

2) Omar Ramadhan Mapuri(mzaliwa wa Tanganyika) alikuwa waziri wa elimu kule zanzibar kasaini mikataba mingi tu.

3) Kwa mujibu ya makubaliano ya muungano yalikuwa mambo 7, yakaongezwa 6 na kuwa 13. Baadae yakaongezwa 8 na kufikia 21 jee hayo 14 nani alie saini(marais gani wali kubaliana kusaini) Jee Bunge na Baraza la Wawakilishi nao walisaini mkataba wa Muungano na nyongeza zake?.
 
Waliosaini mkataba wanatokea Zanzibar ambayo ina mamlaka kamili,ina Serikali yake,ina Bunge lake na Mahakama zake.Pia ina Bendera yake ya Taifa na ina Wimbo wake.
Umesema ina mamlaka yake si ndio?.

Mamlaka gani?.
Unakumbuka mamlaka ya serikali ya Salmin Amour Juma(rais wa 5 wa zanzibar) alijiunga na OIC kwanini Nyerere alitaka wajitoe?
 
Back
Top Bottom