Mwananchi anyimwa fursa ya kuuliza swali kwa kuanza swali la kusema waliosaini sio Watanganyika

Simple na sisi bara turuhusiwe kusaini mikataba ya Zanzibar
 

Tufanye rejea ya uchaguzi wa 2015, maana 2020 hakukuwa na uchaguzi. Japo hata hiyo 2015 nayo ilikuwa ni ubadilishaji wa matokeo wazi wazi hasa huko Zanzibar baada ya CCM kushindwa dhahiri.

Matokeo ya urais yalikuwa 8m+ wapinzani wakipata 6m+, data hizi ni rasmi toka tume ya uchaguzi ambayo haiaminiki bado. Unataka kumaanisha hizo kura wapinzani walipata kwa kugawana huku mijini, lakini ccm ilipata za mijini na huko vijijini? Je wabunge na madiwani wapinzani walipata maeneo ya mjini tu? Kama wapinzani wanaweza kupata kura hizo mijini tu, huoni ccm haiwezi kupata 2/3 ya kufanya maamuzi watakavyo bungeni? Na sababu hasa ya wizi wa kura ni kwa kupoteza ushawishi, na kulazimisha kupata idadi ya kufanya maamuzi.

Narudia tena, ccm haina uwezo wa kushinda kwa kuvuka 50% kwenye uchaguzi wowote halali, na sio kushinda tu, pia haitakaa iweze kushinda tena zaidi ya kura hizo. Na sababu hasa ni kizazi kubadilika. Na ifahamike ccm sio chama cha kizazi hiki.

Kitakachofanyika iwapo ccm itaendelea kulazimisha kukaa madarakani bila ridhaa ya wananchi, moja wananchi wanaopiga kura watazidi kupungua, huku ccm ikiendelea kubweteka kwa kufanya makosa kama haya ya bandari, pili wizi mkubwa kama ulivyo kwenye ripoti za CAG, na hatimaye itatolewa madarakani kwa machafuko baada ya wananchi kusema enough is enough. Ukitaka kujua ninachomaanisha, cdm wamejitoa kwenye hizi chaguzi ndogo za marudio, subiri uone idadi ndogo sana na hamasa ya wapiga kura. Na uchaguzi wa marudio ya ubunge wa Mbarali iwapo wapinzani watasusia kushiriki hasa CDM.
 
Hiyo space ni ya Jenerali Gerson ama ni watu wa MAELEZO!?
 
Pole!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Imeisha hiyo!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kama ni ushahidi wala sio wa kutafuta upo wazi, na mara zote taarifa huwa zinatolewa polisi. Lakini kwakuwa vyombo vya dola ni sehemu ya CCM, taarifa hizo huwa zinapotezewa, ama ww mtoa taarifa unageuziwa kibao. Haya ni mambo ambayo huwa yanafanywa hadharani na vyombo vyetu vya dola, na ushahidi upo.

Utasema kwenda mahakamani, wanaowapa amri polisi za kuumiza wapinzani, ndio haohao wanaoziagiza mahakama namna ya kutoa hukumu. Ushahidi ni huu uchaguzi wa 2020, Makada wengi wa CDM walifungwa bila ushahidi wa kutosha, yaani kubambikiwa kesi, na sasa baada ya maridhiano uchwara, mahakama zimeagizwa kuwaachia, na wanapoachiwa mahakama hukiri kabisa kuwa walifungwa bila ushahidi kutimia. Na hata juzi kada mkongwe wa CCM Rostam Azizi, alisema sio rahisi wawekezaji wa kimataifa kutumia mahakama zetu za ndani kwa migogoro, kwani inawezekana hakimu/jaji akapigiwa simu na kiongozi kisha kutoa hukumu kinyume na ushahidi. Na kwa kukuonyesha nini kinaendelea kwenye mahakama zetu, kuna kesi ya wabunge waliofukuzwa huko CDM, kesi ile ina miaka miwili sasa lakini hakuna hukumu, wakati hapo Kenya kulikuwa na kesi ya matokeo ya urais, hukumu ilishatoka muda mrefu.

Sababu hizo hapo juu pamoja na udhaifu mwingine wa kimifumo, ndio unaofanya ccm hadi leo iwe madarakani, na wala sio kwa ushawishi wake wa kisiasa. Uchaguzi wa mwisho wa CCM kukaa madarakani kihalali ilikuwa ni uchaguzi wa 2005, baada ya hapo ccm ipo na itaendelea kuwepo madarakani kwa mbeleko ya vyombo vya dola, na udhaifu mwingine wa mifumo unaochangiwa na katiba hii outdated. Huu ni ukweli ambao sikulazimishi kuukubali lakini ndio uhalisia.
 
Upo sahihi ila tunaangalia operation ya Ticts ndo hiyo itakuwa ya Dp world .


Ina maana Ticts alisharenew mkataba mara kadhaa kwa wala na pia malalamiko yake ya utendaji mbovu yalikuwa yanapokelewa na kuwasilishwa kwa mamlaka.

Mchakato ni process ndefu na pia katika kurekebisha hilo linawezekana kwa aslimia kubwa kwa sababu wadau washaingia katika kuchunguza mkataba ,bado wapo kweny makubaliano wanaweza kulumbana na kuweka sawa hata mwakani ili mradi uwe sawa .

Kama haiwezekani sio lazima DP world yeyote yule kikubwa ufanisi.

Hapa umeeleza mambo ya msingi lakini anakuja mtu anakuambia eti "wanauza bandari" 😅😅

Ticts kama sio utendaji mbovu angeendelea ni hakika huyu hata aingia akileta magumashi miaka 5 hatoboi.
 
Ndugai hakufurushwa, kajiuzulu kwa hiari yake kwa mujibu wa barua yake ya kujiuzulu.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Wanataka kuvunja muungano na wameona hii ndiyo njia pekee ya Tanganyika kuanzisha mchakato wa kuuvunja mchakato. Wako sahihi. Tuuvunje.
 
Hivi Kuna Mnyamwezi alishawahi kusaini mkataba wa uwekezsji wa serikali ya mapimduzi ya Zanzibar
1) Nyerere alimuondoa rais wa zanzibar kwa sababu ya Jumbe kutaka serikali tatu. Hivi rais wa Tanganyika kwanini amuondoe rais wa nchi ya zanzibar?.

2) Omar Ramadhan Mapuri(mzaliwa wa Tanganyika) alikuwa waziri wa elimu kule zanzibar kasaini mikataba mingi tu.

3) Kwa mujibu ya makubaliano ya muungano yalikuwa mambo 7, yakaongezwa 6 na kuwa 13. Baadae yakaongezwa 8 na kufikia 21 jee hayo 14 nani alie saini(marais gani wali kubaliana kusaini) Jee Bunge na Baraza la Wawakilishi nao walisaini mkataba wa Muungano na nyongeza zake?.
 
Waliosaini mkataba wanatokea Zanzibar ambayo ina mamlaka kamili,ina Serikali yake,ina Bunge lake na Mahakama zake.Pia ina Bendera yake ya Taifa na ina Wimbo wake.
Umesema ina mamlaka yake si ndio?.

Mamlaka gani?.
Unakumbuka mamlaka ya serikali ya Salmin Amour Juma(rais wa 5 wa zanzibar) alijiunga na OIC kwanini Nyerere alitaka wajitoe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…