Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa

Ameongea kama baba levo tu.YY ndio angesema ukweli ulivyo kua ni miaka mingapi? Na kwenye mkataba Tanzania itanufaika hv n hv kwa miaka kadha.
 
Sasa kwa akili yako kukiwa na shida kwenye mkataba watakaoteseka ni chadema peke yao? Watu ambao ni ccm kweli na wasomi.walioshika nyadhifa za maana wameyaona mapungufu.
Haya alichokieleza AG kikaeleweka ni kipi? Waliopinga waliweka hoja na vifungu vyenye ukakasi yeye amepanguaje?
Alisema Dr. Nshala, kuwa kiongozi wa Serikali au mbunge hakukufanyi kuwa mwenye akili kuliko wote.
Shida ya wengi hawaangalii hoja wanangalia huyu mtoa hoja ni WA wapi!!
Msikilize Rostam anavyopambana na Dr. Slaa,anarukia eti huyu alikisaliti chama chake, sasa inahusiana nini na hoja zilizoibuliwa.
Hoja imekwenda bungeni mahali ambako huyo AG alipaswa ndio afafanue akaishia kumwachia Spika.
Tumeshuhudia mikataba yote yote yenye ukakasi ilipoibuiliwa bungeni tuliwaona maAG waliopita, walivyosimama na mpaka wengine kupoteza kazi zao.
Kashfa ya Richmond iliondoka na Johnson Mwanyika, ya Escrow tulimuona Jaji Werema akiachia ngazi. Lakini mjadala huu wa DP umemsikia AG akiibuka kuondoa taharuki iliyopo??Tena angalau hata Mh PM. Hata kama hana cha kufanya, lakini angalau kaonyesha staha kwa watu wenye maoni tofauti.
Hakuna anayepinga uwekezaji kwa vyovyote vile, hakuna aliyetaja rangi,Taifa au dini ya mtu, kinacholeta shida ni terms na condition za mkataba,wajuzi wa sheria wamezielezea, tulitegemea yeye AG, aje na utetezi dhidi ya vipengele vyote vya kwenye mkataba vilivyoibuliwa na siyo kutishia Kuna tuna discourage wawekezaji.
 
Huyo ni mwanasheria au roboti ya mama samia,mama samia kashika remote anachezesha kama anavyotaka unategemea aongee nini?..apeleke ujinga huko
Mbowe asingeuliza Sasa kwnn mwanasheria mkuu hajasema chchte mpk Sasa...na vilevile yy kama mtanzania pia ana haki ya kuchangia ukiachana na nafasi yake kama Mwanasheria mkuu wa serikali...kwhyo punguza makasiriko
 
Kwa nini kila kitu cha nchi hii sasa wanapewa Waarabu?
 
Hajajibu wapi ilipo sahihi yake kwenye mkataba huo, maana tumeitafuta weeeee, haipo !!!!!
 

Acha waje waamue vyoyote vile. Historia itawakumbuka.
 
Hajaitendea haki taaluma na cheo chake kaongea kama Msukuma au Babu Tale.
 
Mpuuzi moja anaye tumia kodi za wananchi kwa faida ya yeye na wanae
 
SAWA.
Lakini hajasema hakuna tatizo lolote ndani ya IGA?

Na haya huku je, hakuna shida yoyote?
 
Hujamwelelewa wapiii. Acheni ubaguzi wa wawekezajiii
 
SAWA.
Lakini hajasema hakuna tatizo lolote ndani ya IGA?

Na haya huku je, hakuna shida yoyote?
Ukimsikiliza vizuri kasema IGA ni relevant katika mazingira tuliyonayo zikiwemo sheria zetu
 
Yaani kaongea kama mlevi, hata hakuna hoja aliyojubu.., hivi huyu ni mwanasheria kweli? Yaani haeleweki kabisa!
 
An intergovernmental agreement (IGA) is an agreement made between the Commonwealth and state and territory governments. While IGAs are not legally binding, they express the commitment of governments to work together on certain objectives or goals.
 
Ukimsikiliza vizuri kasema IGA ni relevant katika mazingira tuliyonayo zikiwemo sheria zetu
Dah!
Umenirushia bomu la mkono hapa, mkuu 'comte'!

Wewe haya maneno unayaelewa vipi? Mimi sina hata moja ninalolielewa hapo!
 
Yaani kaongea kama mlevi, hata hakuna hoja aliyojubu.., hivi huyu ni mwanasheria kweli? Yaani haeleweki kabisa!
Mwanasheria kajibu hoja moja kubwa kwa kusema kuwa pale hakuna MKATABA
 
Dah!
Umenirushia bomu la mkono hapa, mkuu 'comte'!

Wewe haya maneno unayaelewa vipi? Mimi sina hata moja ninalolielewa hapo!
Mkuu sasa hivio wenye hela za kuwekeza ni waarabu; hakuna namna ya kuwakwepa hata waingereza wamewapa timu zao za mpira ingawa makocha wa timu hizo siyo waarabu ni wazungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…