Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa

An intergovernmental agreement (IGA) is an agreement made between the Commonwealth and state and territory governments. While IGAs are not legally binding, they express the commitment of governments to work together on certain objectives or goals.
Kunradhi kwa kusema hivi, lakini ndio ukweli wenyewe:
Ujinga (upumbavu) huanzia huko huko kwenye mambo kama haya..., "not legally binding"... sasa ya nini kupotezeana wakati?
Mambo yenyewe hadi inalazimu kuyapeleka Bungeni?

Ukoloni nao ulianza hivyo hivyo, na utumwa; kwa kulazwa akili tu watu!

Nenda kasome masharti yaliyomo kwenye hiyo IGA, halafu useme haina maana katika mikataba itakayofuata chini ya makubaliano hayo, halafu uje useme "not legally binding". Ninaelewa hii umeinyanyua tu mahala si maandishi yako, lakini kuamini hayo ni ujinga.
 
Sawa hakuna palipoandikwa miaka 100 wala mkataba wa milele, atuonyeshe basi wapi umeandikwa ni wa miaka mingapi?
Akipakosa
Atupe tafsili ya (MPAKA SHUGHULI ZA BANDARI ZITAKAPOKOMA)

Mkodishe mtu shamba lako kwenye makubaliano weka kifungu ataondoka pale SHUGHULI za kilimo zitakapokoma.
 
An intergovernmental agreement (IGA) is any agreement that involves or is made between two or more governments in cooperation to solve problems of mutual concern. Intergovernmental agreements can be made between or among a broad range of governmental or quasi-governmental entities. Governments use IGAs for cooperative planning, development review, resource sharing, joint planning commissions, building inspection services, and more.
Mkuu barua ya uchumba ikikubaliwa inakupeleka kwenye posa, hadi katika hatua hiyo hakuna mme wala mke halali hapo. Bunge lilipewa nafasi ya kusoma na kupitia barua ya uchumba- azimio lao linaruhusu sasa majadiliano kuanza na kuzaa mikataba mahususi kwa jambo mahususi. Rudisha akili zako kutoka kwa wapotoshaji
 
An intergovernmental agreement (IGA) is an agreement made between the Commonwealth and state and territory governments. While IGAs are not legally binding, they express the commitment of governments to work together on certain objectives or goals.
saini inayowekwa kwenye hizo agreement ni kwa ajili ya nini ukizingatia haziko legally binding kama mbavyotaka kuaminisha watu? Yaani tulipeleka bungeni kujadili mkataba ambao sio legally bindig? Saini zilizowekwa pale ni za nini?
 
Sawa hakuna palipoandikwa miaka 100 wala mkataba wa milele, atuonyeshe basi wapi umeandikwa ni wa miaka mingapi?
Akipakosa
Atupe tafsili ya (MPAKA SHUGHULI ZA BANDARI ZITAKAPOKOMA)

Mkodishe mtu shamba lako kwenye makubaliano weka kifungu ataondoka pale SHUGHULI za kilimo zitakapokoma.
Hapapo- na hii inamaanisha kuwa HAKUNA MKATABA
 
Mkuu sasa hivio wenye hela za kuwekeza ni waarabu; hakuna namna ya kuwakwepa hata waingereza wamewapa timu zao za mpira ingawa makocha wa timu hizo siyo waarabu ni wazungu
Hapana, sikubaliani kabisa na fikra za namna hii.

hata kama wana hela; na hata kama wangekuwa ni wao tu pekee ndio wanaowekeza, huwezi kuacha kutetea unayoyaona ya msingi kwako kwa vile tu unataka uwekezaji.

Hii dhana ndiyo itakayotuangusha kama taifa.
Sasa hivi hatujiamini kabisa kwamba tunaweza kufanya mambo mengi sana ykuhusu maendeleo yetu sisi wenyewe. Kila kitu ni lazima tutafute wenye hela!
Huku ndio kulemaa kwa akili kwenyewe.

Bandari hatuwezi kuiendesha, kwa vile hatuna pesa, au kwa vile hatuwezi kusimamia kazi zetu vizuri sisi wenyewe?

Usilinganishe Waingereza na hali yetu, ni vitu tofauti kabisa.
 
Hiyo hatua haijafikiwa ikifikiwa tahadhari zipo kwa mjibu wa sheria za Tanzania
 
An intergovernmental agreement (IGA) is any agreement that involves or is made between two or more governments in cooperation to solve problems of mutual concern. Intergovernmental agreements can be made between or among a broad range of governmental or quasi-governmental entities. Governments use IGAs for cooperative planning, development review, resource sharing, joint planning commissions, building inspection services, and more.
Mkuu barua ya uchumba ikikubaliwa inakupeleka kwenye posa, hadi katika hatua hiyo hakuna mme wala mke halali hapo. Bunge lilipewa nafasi ya kusoma na kupitia barua ya uchumba- azimio lao linaruhusu sasa majadiliano kuanza na kuzaa mikataba mahususi kwa jambo mahususi. Rudisha akili zako kutoka kwa wapotoshaji
Kwenye uchumba huwa mnasaini document yeyote? Yaani huwa mnaweka saini?
 
Unatupeleka kwenye udini- mkuu haupo uhusiano wa uarabu na uislam kama umeambiwa huko kanisani kwenu wamekudanganya
Hapa ni wewe ndiye unapeleka kwenye udini. Yeye hajaeleza chochote kinachohusiana kati ya uarabu na dini.
 
Uongo hutembea haraka na hasa ukiwa unaenezwa na wapumbavu kabla ukweli haujaja kumaliza kila kitu
Kwamba Yeye kama Mwanasheria Mkuu alichokisema ndio kamaliza utata uliopo? Hapana!

Amegusia Hoja tatu kama sikosei zilizozagaa

(1) Hoja ya Usuluhisho;
(2) Hoja ya Ukomo;
(3) Hoja ya Ubaguzi ambayo kiuhalisia Umeanzishwa na wafia dini! Na inayotumiwa na madalali.... Ati leo hii wanaipa uzito Ubaguzi wa hoja za mtandaoni wakati Wasukuma wamekuwa wanabaguliwa hapa na Serikali imekaa kimya!

Mtaji mkubwa ni upi? na kama ni kweli hawajabanwa na IGA ataje kiasi cha huo 'mtaji mkubwa' manake, binafsi mie nimejikita kwenye suala la Uwekezaji, na Wawekezaji(Waarabu) yaani uwekezaji wa Wazawa Uwekezaji wa Mwafrika! Isitoshe Umuhimu na Uharaka wa Kuingia- chochote kile kinachoitwa sasa hivi, makubaliano ya awali, Mkataba, Azimio, MOU IGA haijalishi, kwa kiingereza kama lugha inayotakiwa kutumika kwenye suala hil, I don't give a Faaak -Uharaka na unyemela wa nini?

Yaani hiyo PPP anayotumia kama msingi wa kuhalalisha ushirikiano wao, ni kwanini, kama alivyogusia asipewe Mwafrika? Kwanini iwe ni mzungu au Mhindi au Mwarabu? Maana anataka kutuaminisha Mwafrika hawezi wakati kinachowasumbua ni Pesa? Mwafrika hana pesa?

Hivi haoni hayo ni matusi?

Yaani kama kweli serikali ilidhamiria PPP na ina watanzania wenye uwezo iliwashinda nini kuwaelimisha, wakaungana wakawa ndio wasimamizi wa TPA?

Ngoja kwanza...nisije nikaharibu mengine
 
Hapana, sikubaliani kabisa na fikra za namna hii.

hata kama wana hela; na hata kama wangekuwa ni wao tu pekee ndio wanaowekeza, huwezi kuacha kutetea unayoyaona ya msingi kwako kwa vile tu unataka uwekezaji.

Hii dhana ndiyo itakayotuangusha kama taifa.
Sasa hivi hatujiamini kabisa kwamba tunaweza kufanya mambo mengi sana ykuhusu maendeleo yetu sisi wenyewe. Kila kitu ni lazima tutafute wenye hela!
Huku ndio kulemaa kwa akili kwenyewe.

Bandari hatuwezi kuiendesha, kwa vile hatuna pesa, au kwa vile hatuwezi kusimamia kazi zetu vizuri sisi wenyewe?

Usilinganishe Waingereza na hali yetu, ni vitu tofauti kabisa.
ACHANA NA NDOTO ZA NATIONALISM EAT YOUR PRIDE
 
Hapa ni wewe ndiye unapeleka kwenye udini. Yeye hajaeleza chochote kinachohusiana kati ya uarabu na dini.
Najua anakotaka kutupeleka- kwenye ubaguzi
 
Siyo kila saini inamaanisha kuwa ni mkataba
Saini maana yake nini? Yaani unaweka saini ili iweje?! Kwa ini msikubaliane tu halafu nasi, mnaweka saini ili iweje?!

495285B7-B6FC-4F64-8029-F83211BC8813.jpeg
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi atoa maneno mazito mjadala wa DP World

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.

"Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna," alisema Feleshi.

Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.

"Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?" Alihoji Jaji Feleshi.

Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.

"Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?" Aliongeza.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.

"Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi," alisisitiza.

Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.

"Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika," alisema.

Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.

"Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari)," alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.

Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Credit: Jambo TV
Huu ufafanuzi una tofauti gani na wa Mwijaku? Si Bora maswali mawili ya Mrisho Mpoto?
 
Back
Top Bottom