Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa

Walioelewa mtuambie mm sijaelewa lolote..Nilitegemea kama AG ungetambaa na ulalo wa Sheria ukichambua issues ambazo wananchi wana mashaka nazo mfano..Useme hii miaka sio milele wala sio mia ila iko hivi na vile..useme pia nchi itafaidika hivi na vile kuanzia mwaka huu mpaka huu...sasa ukianza kusema miradi inakwama kweli bandari ikiendeshwa na DP world ndio miradi haikwami??? Nchi hii dah ni ya kuhurumia sana
Thubutuuu hana hizo guts hapo anatetea uteuzi tu
 
Hiyo IGA ni makubaliano yaliyotiwa saini, sasa saini ya nini katika makubaliano yasiyo na nguvu kisheria? Unaweka saini kwa lengo gani?

View attachment 2669707
Unambishia Hadi mwanasheria mkuu!!?..mna matatizo
Sawa hakuna palipoandikwa miaka 100 wala mkataba wa milele, atuonyeshe basi wapi umeandikwa ni wa miaka mingapi?
Akipakosa
Atupe tafsili ya (MPAKA SHUGHULI ZA BANDARI ZITAKAPOKOMA)

Mkodishe mtu shamba lako kwenye makubaliano weka kifungu ataondoka pale SHUGHULI za kilimo zitakapokoma.
Si umeambiwa hakuna mkataba ulosainiwa!!..Sasa akuoneshe nini!?
 
si
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi atoa maneno mazito mjadala wa DP World

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.

"Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna," alisema Feleshi.

Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.

"Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?" Alihoji Jaji Feleshi.

Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.

"Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?" Aliongeza.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.

"Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi," alisisitiza.

Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.

"Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika," alisema.

Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.

"Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari)," alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.

Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa M
 
Wewe nawe ondoa kauli za kipumbavu, mkataba utawekwa sign, uchaguzi wa serikali za mitaa CCM, uchaguzi ujao CCM, nadhani mmesahau JPM alichowafanyia piga chini mpaka mwenyekiti wenu ohhh sijui tuandamane hakutoka hata mmoja barabarani. Mama Samia kaja kamuonea huruma kamtoa sasa pembe zinakuwa dawa ipo karibu tu.
Kwani Mbowe alibambikiwa kesi kipindi cha dhalimu, au ni kipindi cha mama wa kambo?
 
Mahakama ndiyo sehemu sahihi; wameshaenda tayari wataeewana huko
Mahakama hizi ambazo wawekezaji hawazitumii nazo ni mahakama au majengo ya mahakama yaliyo chini ya Makada wa ccm?
 
Hakika Wajinga ndio waliwao kwamba IGA ni mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kuboresha bandari, siyo wa utekelezaji, ambao hauna nguvu za kisheria isipokuwa pale mikataba ya utekelezaji (HGAs) itakapoandaliwa na kutekelezwa.

Kama sababu kuu ndiyo hiyo, ya Falme ya Dubai kushirikiana na Tanzania, kuendesha na kuboresha bandari, kwa kutumia DPW, kampuni yao, kwa nini inatakiwa kutafuta fedha ya uwekezaji (Ibara ya 4:4,5) na siyo kupewa na nchi yao? Kusudio hilo hakika ni nje ya huo ushirikiano kwani DPW, kampuni ya kibiashara, haihitaji kubebwa na nchi yao kuwekeza popote duniani. Na naamini kule ilikowekeza nchi hizo hazina mikataba ya ushirikiano (IGA) na Dubai.
 
Jibuni hoja, kwa makubaliano yasio na nguvu ya kisheria, mnaweka saini ili iweje?
Ndiyo maana tangu mwanzo nilitaka u-google, sababu kufanya mjadala na wewe huwa shida,mgumu kuelewa au huwa una misimamo yako,unakua na majini yako mfukoni
 
Kupata baraka kwenye haya makabrasha?

Tena watakuwa wamewadharau sana wabunge na wananchi.

Hii ndio Dr Tulia alipelekewa???

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Tunaheshimu Phd yako usiteteebhaya mskabrasha. Utaaibika.
Hawa ndio wanasababisha Phd za bongo kuonekana ni takataka tu.
 
Ndiyo maana tangu mwanzo nilitaka u-google, sababu kufanya mjadala na wewe huwa shida,mgumu kuelewa au huwa una misimamo yako,unakua na majini yako mfukoni
Niligoogle na kutoona tofauti, kikubwa nilikuta zote ni legally binding, tofauti na ulivyodanganya kwamba si legally binding..., sasa utumbie tofauti ni ipi?
 
Huyo ni mwanasheria wa ccm... kaongea utumbo mtupu...nchi hii ina wapumbavu wengi sana aisee alafu wanajiita wasomi
 
Wewe nawe ondoa kauli za kipumbavu, mkataba utawekwa sign, uchaguzi wa serikali za mitaa CCM, uchaguzi ujao CCM, nadhani mmesahau JPM alichowafanyia piga chini mpaka mwenyekiti wenu ohhh sijui tuandamane hakutoka hata mmoja barabarani. Mama Samia kaja kamuonea huruma kamtoa sasa pembe zinakuwa dawa ipo karibu tu.
Dada yake lucas mwashambwa una matatizo aisee
 
Back
Top Bottom