mahindi hayaoti mjini
JF-Expert Member
- Nov 29, 2022
- 2,120
- 2,709
Mmesikia nyie wagalatia na parokia, haya nendeni sasa mkaimbe
Case closed
Case closed
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
You don't know that!Kama mwanasheria mkuu, tena jaji, ana uwezo wa kujibu kwa kina na kwa weledi, zaidi ya alivyofanya. Naona kajibu kwa namna hii ili kuwaridhisha waliomlazimisha aseme neno.
.
Unajiuliza sana huko kwenye LNG sijui wamesaini kitu gani kama hawa ndio wanasheria wa serikali, maana huko kuna hesabu za advanced management accounting na sheria juu; utatia akili. Ndio maana mtu kama January anavyoona rahisi hayo mambo unajichekea tu pembeni.
Aje huku atuambie hii ni nin
Hao wanaziba masikio tu, na akili yao inawatuma kuwa mtawafanya nini.Sasa kwa akili yako kukiwa na shida kwenye mkataba watakaoteseka ni chadema peke yao? Watu ambao ni ccm kweli na wasomi.walioshika nyadhifa za maana wameyaona mapungufu.
Haya alichokieleza AG kikaeleweka ni kipi? Waliopinga waliweka hoja na vifungu vyenye ukakasi yeye amepanguaje?
Alisema Dr. Nshala, kuwa kiongozi wa Serikali au mbunge hakukufanyi kuwa mwenye akili kuliko wote.
Shida ya wengi hawaangalii hoja wanangalia huyu mtoa hoja ni WA wapi!!
Msikilize Rostam anavyopambana na Dr. Slaa,anarukia eti huyu alikisaliti chama chake, sasa inahusiana nini na hoja zilizoibuliwa.
Hoja imekwenda bungeni mahali ambako huyo AG alipaswa ndio afafanue akaishia kumwachia Spika.
Tumeshuhudia mikataba yote yote yenye ukakasi ilipoibuiliwa bungeni tuliwaona maAG waliopita, walivyosimama na mpaka wengine kupoteza kazi zao.
Kashfa ya Richmond iliondoka na Johnson Mwanyika, ya Escrow tulimuona Jaji Werema akiachia ngazi. Lakini mjadala huu wa DP umemsikia AG akiibuka kuondoa taharuki iliyopo??Tena angalau hata Mh PM. Hata kama hana cha kufanya, lakini angalau kaonyesha staha kwa watu wenye maoni tofauti.
Hakuna anayepinga uwekezaji kwa vyovyote vile, hakuna aliyetaja rangi,Taifa au dini ya mtu, kinacholeta shida ni terms na condition za mkataba,wajuzi wa sheria wamezielezea, tulitegemea yeye AG, aje na utetezi dhidi ya vipengele vyote vya kwenye mkataba vilivyoibuliwa na siyo kutishia Kuna tuna discourage wawekezaji.
Ameamka baada kuambiwa bubu ? Hahaha kazi ipo bungeni alisinzia ? Mbona Ali mute ? AtupisheMwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi atoa maneno mazito mjadala wa DP World
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.
Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.
"Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna," alisema Feleshi.
Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.
"Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?" Alihoji Jaji Feleshi.
Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.
"Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?" Aliongeza.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.
"Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi," alisisitiza.
Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.
"Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika," alisema.
Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.
"Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari)," alisema.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.
Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Credit: Jambo TV
Kwani anayeupinga uwekezaji ni nani? Sijaona mtanzania hata mmoja anayepinga uwekezaji.JITAMBUEUbaya hamko makini na madai yenu, watu wanasema wanapinga Makubaliano na wakatangaza kuandamana ila hakuna aliyejitokeza kuandamana.
Ukiwambia wanakasirika na kutoa matusi.
Binafsi naunga mkono uwekezaji wa Mwarabu
JPM alisema unapofika wakati wa kusaini mikataba sheria yote uyeyuka.Itakuwa elimu ya mchongo ..hakuna mwanasheria hapo ..ukweli lazima usemwe
Siyo "kujifunza".Ndio ulivyojifunza kwenye somo la historia?
Hawana hoja tena, imebaki kushikilia hayo yasiyohusika. Sijui wanategemea nani ataamini upotoshaji wa namna hiyo tena.Kwani anayeupinga uwekezaji ni nani? Sijaona mtanzania hata mmoja anayepinga uwekezaji.JITAMBUE
Una hoja dhaifu sanaccm ana wabunge kibao ila kufanya mkutano mmoja wa siasa mpaka kila mtu apate buku tano ndio kidogo mkutano unakuwa na viwatu watu, chadema hata mia hatoi ila nyomi kama dunia.,sasa chama gani kimekufa?
Mimi mtu akitoa hoja kama hii napenda na najibu hoja bila kushambuliana. Kwanza tunakubaliana hakuna shida na uwekezaji, wala sio hatuna shida na DP au angekuwa hata mwingine japo ulichosema sio wote wako wanashambulia watu kwa maeneo waliyotoka na wako wako wanaita kwa majina WAARABU kiujumla ni kama vile Tz hii haina waarabu na ni wa Tanzania 100%. Si sawa kama hukubalini na taasisi au kampuni kuita watu mabeberu, wahindi na mengine ni vizuri kuitaja specific hatukubaliani na DP, sasa hao wapinzani angalia kauli zao za chuki huko ni wazi sio hoja ila ni chuki. Rostam kamjibu DR Slaa sababu Dr Slaa kamshambulia kama Rostam badala ya kujikita kwenye issue na yeye kamjibu kama yeye, pili hao unaowaita hata CCM wanapinga ni sawa ni haki yao lakini mtu kabla hujapinga lazima ujuwe unapinga nini? wengi tunadandia kauli za kisiasa tu lakini pia wako wanaounga mkono sasa hatuwezi kukubaliana wote kikubwa majority win. Na wengi hao wana CCM wanaopinga ni wale hawana nafasi tena watu kama kina Warioba ni wazi kuna donge linawauma ndani ya CCM kama always yuko negative wakipewa nafasi tu wana switch utashangaa. Mimi ningependa kusikia ni nini object ya kuweka mwekezaji bandarini halafu tupime tutapata tunachotarajia? issue ya mikataba hatuwezi sote kusoma vifungu sio kazi kila mtu anaweza kufanya ndio maana hata mikataba yetu binafsi tu tunawapa wanasheria lakini leo kila mwanaharakati kama mwanasheria anakuja na tafsiri yake. mkataba utakuja baina ya TPA na DP wanasheria wao ndio wanapitia T&C kabla ya kusign lakini kuna watu wameshaamua wao hawataki, sasa wewe hutaki kama nani? wewe role yako hutaki ni siku ya kuchagua viongozi chagua chama unachotaka lakini CCM wako madarakani kwa ridhaa then wanahaki ku set tone. Kuna watu hawajui hata mchango kiasi gani bandari unachangia na changamoto zake lakini leo ukiwasikia utadhani ni expats. Mimi naunga uwekezaji 100%Sasa kwa akili yako kukiwa na shida kwenye mkataba watakaoteseka ni chadema peke yao? Watu ambao ni ccm kweli na wasomi.walioshika nyadhifa za maana wameyaona mapungufu.
Haya alichokieleza AG kikaeleweka ni kipi? Waliopinga waliweka hoja na vifungu vyenye ukakasi yeye amepanguaje?
Alisema Dr. Nshala, kuwa kiongozi wa Serikali au mbunge hakukufanyi kuwa mwenye akili kuliko wote.
Shida ya wengi hawaangalii hoja wanangalia huyu mtoa hoja ni WA wapi!!
Msikilize Rostam anavyopambana na Dr. Slaa,anarukia eti huyu alikisaliti chama chake, sasa inahusiana nini na hoja zilizoibuliwa.
Hoja imekwenda bungeni mahali ambako huyo AG alipaswa ndio afafanue akaishia kumwachia Spika.
Tumeshuhudia mikataba yote yote yenye ukakasi ilipoibuiliwa bungeni tuliwaona maAG waliopita, walivyosimama na mpaka wengine kupoteza kazi zao.
Kashfa ya Richmond iliondoka na Johnson Mwanyika, ya Escrow tulimuona Jaji Werema akiachia ngazi. Lakini mjadala huu wa DP umemsikia AG akiibuka kuondoa taharuki iliyopo??Tena angalau hata Mh PM. Hata kama hana cha kufanya, lakini angalau kaonyesha staha kwa watu wenye maoni tofauti.
Hakuna anayepinga uwekezaji kwa vyovyote vile, hakuna aliyetaja rangi,Taifa au dini ya mtu, kinacholeta shida ni terms na condition za mkataba,wajuzi wa sheria wamezielezea, tulitegemea yeye AG, aje na utetezi dhidi ya vipengele vyote vya kwenye mkataba vilivyoibuliwa na siyo kutishia Kuna tuna discourage wawekezaji.
Hiyo kazi ya JPM na sio kabambikiwa kuna ukweli na kama ni Mama basi heshima yake Mama maana jamaa mwenyekiti wao kasota ndani walibaki kwenda kumtembelea tu huko ndani. Rais ana huruma tu akija mtu kama JPM au Mungu angempe maisha marefu tu hawa jamaa wangeimba kila nyimbo..Kwani Mbowe alibambikiwa kesi kipindi cha dhalimu, au ni kipindi cha mama wa kambo?
Unajuwa nilikuwa nawaonea huruma wakati wa JPM nikidhani alikuwa tough sana lakini leo hii namuelewa kwanini alikuwa anafanya vile ukianza kumpiga nyani usimuangalie usoni na JPM alijuwa namna ya kupiga. RIP.Dada yake lucas mwashambwa una matatizo aisee
Mama kaja kamtoa tu kwa huruma na kabla hajaenda kwa mkewe akaambiwa kaoge uje upige picha Ikulu na akaenda hizo kazi ya ChumaKwani Mbowe alibambikiwa kesi kipindi cha dhalimu, au ni kipindi cha mama wa kambo?
Bavicha hamsikilizagi Hoja. Bandari imeuzwa hati kaitoa MboweWalioelewa mtuambie mm sijaelewa lolote..Nilitegemea kama AG ungetambaa na ulalo wa Sheria ukichambua issues ambazo wananchi wana mashaka nazo mfano..Useme hii miaka sio milele wala sio mia ila iko hivi na vile..useme pia nchi itafaidika hivi na vile kuanzia mwaka huu mpaka huu...sasa ukianza kusema miradi inakwama kweli bandari ikiendeshwa na DP world ndio miradi haikwami??? miradi gani?? wewe toa majibu ya hoja za wananchi sio miradi imekwama...Nchi hii dah ni ya kuhurumia sana...
Wadanganyika wabaguzi.. wapemba sio watanzania?Mbowe ana nguvu sana kuongea kidogo , mwanasheria katoka mafichoni ...hata ivyo aje afafanue kwa nini mkataba una sahihi ya wapemba watatu
Nyinyi ndo mana hamapati kitu miaka yote wabinafsi sana. Ccm yoyote anakula ukifika muda wake, chadema mkipata nafasi mtarudisha makao makuu ya chama na maendeleo yote Machame. Hamtoboiiii 😆toka hapa we mpemba alishindwa magufuri kuua upinzani ndio ataweza huyu mama? Rudini kwenu uko pemba watanganyija tumeanza kuwaangalia kwa ukaribu
Nyinyi ndo mana hamapati kitu miaka yote wabinafsi sana. Ccm yoyote anakula ukifika muda wake, chadema mkipata nafasi mtarudisha makao makuu ya chama na maendeleo yote Machame. Hamtoboiiii 😆toka hapa we mpemba alishindwa magufuri kuua upinzani ndio ataweza huyu mama? Rudini kwenu uko pemba watanganyija tumeanza kuwaangalia kwa ukaribu